Suala la Mishahara kwa watumishi wa Umma liangaliwe upya, tena kwa macho manne

Suala la Mishahara kwa watumishi wa Umma liangaliwe upya, tena kwa macho manne

Kwani walimu wakiendaga kazi maalum kama kusahihisha mitihani hawalipwi? Au seminar? Hizo ndio maana ya per diem. Hakuna maana nyingine.
Hivi per diem mbona IPO sawa kwa watumushi wore was serikali pale wanaposafiri nje ya kituo cha kazi?? Maana ya per diem no pesa wanayolipwa ili kujikimu nje ya kituo cha kazi.sasa ukisema walimu hawalipwi no jambo LA kushangaza Fanya tafiti kidogo. Luna watu wanafanya kazi Massa mengi Vila lipwa Ziada sababu ni ratiba za ofisi zao zipo hivo na likizo wengine wanaenda Mara mbili kwa mwaka wengine Mara moja.Luna watumishi was umma wengine kazi zao zina risk kubwa kimaisha mpaka hata kujichanganya na jamii kwao ni ngumu.kuna taasisi zingine mtumishi kufukuzwa kazi ni muda wowote.
 
Amani iwe juu yenu.

Jambo la mishahara ni kitu muhimu sana kwa mtu ndio maisha yake na ndio uhai wake. Kuna mtumishi namba moja aliyepita alipata kusema "Asiyefanya kazi na asile na maana yake afe" hivyo kila mtu hufanya kazi ili aishi yeye na familia yake.

Unyeti wa mshahara ndio umefanya mimi leo niandike hii mada, Nchi yetu bado ina unyonyaji ambao tunafanyiana sisi kwa sisi. Tumejitengenezea matabaka kwenye ofisi na taasisi zote za umma. Tumefanya aina fulani za kazi zikimbiliwe na watu wengi (ubunge) na zingine zikimbiwe (na matajiri) zikimbiliwe na maskini mfano UALIMU.

Ili Nchi yoyote iendelee kwanza jambo la usawa ni muhimu sana na kada za kuendeleza Nchi ndio hupewa kipaumbele Mf: Elimu, viwanda na technology. Nchi hii wanaozalisha hulipwa kiduchu na wafanyamaamuzi hulipwa pesa mlima its contrary the opposite.

Hivi ni kwa nini wanaofanya kazi TRA, BOT, TPA, TASAC na n.k hulipwa zaidi kuliko Walimu na Manesi na Polisi na Majeshi yetu? Bado wana posho, marupurupu na per diem? Hivi kwa nini Mwalimu wa Degree anachukua mshahara laki tano au sita kwa mwezi na hana posho wala per diem mwaka mzima. Halafu mtu mwingine mwenye kiwango sawa cha Elimu anayefanya kazi BOT analipwa 1.8M kwa mwezi? Aiseee!

Mtumishi namba moja aliyepita awamu ya tano alipata kujiuliza kitu ambacho hata mimi najiuliza, "KWANI WALISOMAJE HAWA" mpaka mtu alipwe 25M au 30M kwa mwezi? Mwisho wa kunukuu.

Nchi hii kuna kazi za watoto wa maskini mfano UALIMU, UNESI, UDAKTARI, UFUNDI na n.k pia kuna kazi za watoto wa vigogo (wazee wa kujipangia mishahara yao) na huu mfupa ni mgumu sana kwa sababu hata watoto wa maskini wanaofanikiwa kufika juu kama Magufuli na Samia hushindwa kuuondoa na kuweka usawa ili nchi Iendelee.

Maendeleo ya Nchi tutayasikia kwenye bomba tu kwa aina hii ya unyonyaji isipokuwa mwenye nacho ataongezewa (be rich to get rich)

Kazi njema wajameni nilikuwa na frustrations zangu tu baada ya kupata report ya BOT.

"TUSIDANGANYWE TENA NCHI HII HAKUNA MZALENDO HATA MMOJA LABLA MIAKA 100 IJAYO NDIO WATAZALIWA."
Thanks kwa yote isipokuwa kwamba hakuna wazalendo,no.Hao uliowaorodhesha yaani Waalimu,Madaktari/Manurse ndiyo wazalendo na watunga sheria,Sera na wawakilishi katika vyombo vya maamuzi siyo wazalendo.
Wenye mishahara minono licha ya kujipangia mishahara yao hawalipi PAYE,hawachangii mifuko ya hifadhi ya jamii wala NHIF lakini pension (gratitude) kila baada ya miaka mitano.
 
Mmi napinga kabisa unajua izo sekta hazitegemi ruzuku tofauti na walimu na watu wengi kwanza mpo wengi mnafakazi masaa 6.

Alie nacho aongezee pambana ufike ulitumwa kusomea ualimu.
Kazi yoyote halali ilipiwe mishahara stahili,ukitaka waalimu waache kazi nao wakagombee udiwani,ubunge ama Urais mtaenea?Watoto mlioambiwa fyatueni watafundishwa na nani?Wagonjwa wa CORONA,TB,HIV,Malaria,Pneumonia wave kwa kukosa tiba?Hospitali zilizojengwa ziwe mapango ya wanyang'anyi?
Suala la mishahara ni nyeti na tusibeze kazi zifanywazo na Watanzania ili kuhalalisha uonevu na ubinafsi wa watawala.
 
Kuna watumishi ngazi ya degree wanapokea 180,000 kwa mwezi kama mshahara.
Usitarajie mtu huyo akaleta tija wala huduma kwa wahudumiwa
 
Uko sahihi ila angalia na uhalisia hilo swala mother mei mosi alishindwa kuongeza kutokana na hali halisi ya nchi na uchumi walimu ni wengi mno na hyo mishahara mikubwa kwani ilianza leo jpm na ubabe wake wote kashindwa ualimu ni wizo na uzalendo ukilala kuna watu wako nje ya game hawajaajiriwa ni wengi unaacha kuongela wabunge wa la saba wanalipwa na mpesa kibao unaongelea hao vi million 1.8

Walimu mnashindwa kwenda kweny point kwamba muongezewe kima fulani sio mbona wale wako ivi kuongezewa ni haki yenu kutokana maisha halisi na balaa lipo zaidi kidogo warudishe ada itasaidia kuongeza hata viposho kwa shule husika ishu imejawa na siasa ni mchi chache walimu na manurse yaani tabata kubwa la wafanyakazi wa umma wanalipwa pesa ndefu
Kazi yoyote halali ilipiwe mishahara stahili,ukitaka waalimu waache kazi nao wakagombee udiwani,ubunge ama Urais mtaenea?Watoto mlioambiwa fyatueni watafundishwa na nani?Wagonjwa wa CORONA,TB,HIV,Malaria,Pneumonia wave kwa kukosa tiba?Hospitali zilizojengwa ziwe mapango ya wanyang'anyi?
Suala la mishahara ni nyeti na tusibeze kazi zifanywazo na Watanzania ili kuhalalisha uonevu na ubinafsi wa watawala.
 
MH. Raisi mwakani siku ya mei mosi tunaomba skeli ya mishahara ya watumishi ivunjwe ipangwe upya watumishi asilimia kubwa wanastaafu katika hali ya ufukara sana kwa kuwa kuna watumishi wameshaonekana wao ni wa mishahara ya chini wakiwemo walimu, sekta ya afya na kwengineko lakini kwa elimu hiyo hiyo aliyekuwa nayo huyo mtumishi anayeishi kwa shida kuna watumishi shida hawazijui kabisa kama waliopo kwenye mashirika ya selikari na viongozi yaani mtu anachukua 20ml kwa mwezi halafu kuna mtumishi anasuburi mshahara wa laki tatu kweli ina make sense tuwe wakweli jamani.
Mnaajiriwa bila usaili afu unataka usawa na aliyechujwa? Haipo hiyo
 
Yaani unacompare kama sio upumbavu huoni tabata we na ualimu wako wa degree usijifananishe na mfanyakz wa BOT hata diploma kwani huoni wanavyokula pesa na wataendelea milele

We pambana na ualimu mbona watu wanajivunia ualimu na wameridhika we unaleta shobo
Andika kiswahili kinachoeleweka, mbona unaandika kikwenu!
 
Hehehe, yaani mtu anayelipwa, say, 3m ndo huyo huyo mwenye marupurupu, posho na nyumba anapewa.

Na huyu anayelipwa 500k ndo hana cha marupurupu, posho na nyumba apange kwa kumega hiyo hiyo 500k yake kwa kiwango cha elimu kile kile.

Hii mifumo sijui imerithiwa kutoka wapi.

SUKAH
dah, nipo katik kundi hilo la wasio na marupurupu na mishahara midogo....

cha kusema tu hapo ni kuwa maisha hayajawahi kuwa sawa na kamwe hayatokuwa. inaumiza sana lakii ndiyo hivyo tena!
 
Pesa nyingi nchi hii inaenda kwa wanasiasa na watawala.
 
Cc. Wizara Ya Fedha..
😂😂😂😂😂
Kuna ofisi tamu jamanii....
 
Wakuliangalia hilo na kulifanikisha ndiyo hawa hawa wa kulipana posho kwa kila sentensi watakayoandika...
 
Kumbe tunajadiliana na mpumbavu!
Bora umelijua Hilo mkuuu,yaan Kuna vilaza wa kutosha hapa nchini ,ajabu Sasa anadharau BAED hapo hapo anasahau kuwa kafundishwa na huyo huyo wa BAED kuanzia form one had six hadi chuo kikuuu.

Watu wa namna hii ndio wale huwadharau wazaz wao baada ya kufanikiwa kuwa na familia zao .

Watu kama hawa ndio wale husahau kabisa wapi wametokea na wamesaidiwa na akina nan had walipo.

Watu kama hawa nao wanasimama mbele za watu et ni educated kumbe ni incompitent wa kutupwa.
 
We unashindwa kuelewa unacompare BAED na misuli ya uhasibu sasa we umesoma ualimu pale BOT unaenda kufit wapi kwa mfano na ujue ualimu ni wito na heshima kubwa kwa jamii despite ya kupata pesa ndogo wanapoforce kufananisha na wengine ndo jambo haliwezekani education kwa wanafunzi wengi ni last priority kuhofia kukosa mkopo iko wazi kabisa mtu ana one ya PCB anaenda kusoma ualimu utamlaumu nan na anajua angalau angesomea engineering akibahatika kufanya kazi na kupata kazi anashika pesa ndefu uliko ualimu

Sisi mwaka tunamaliza watu waliandika kozi tofauti kusoma chuo ila walikuaa kubadili ili wakasome ualimu ukiandika nyingine unachekwa 😥😥😥na kusemwa ju 90% wote ualimu fikiria
Bora umelijua Hilo mkuuu,yaan Kuna vilaza wa kutosha hapa nchini ,ajabu Sasa anadharau BAED hapo hapo anasahau kuwa kafundishwa na huyo huyo wa BAED kuanzia form one had six hadi chuo kikuuu.

Watu wa namna hii ndio wale huwadharau wazaz wao baada ya kufanikiwa kuwa na familia zao .

Watu kama hawa ndio wale husahau kabisa wapi wametokea na wamesaidiwa na akina nan had walipo.

Watu kama hawa nao wanasimama mbele za watu et ni educated kumbe ni incompent wa kutupwa.
 
dah, nipo katik kundi hilo la wasio na marupurupu na mishahara midogo....

cha kusema tu hapo ni kuwa maisha hayajawahi kuwa sawa na kamwe hayatokuwa. inaumiza sana lakii ndiyo hivyo tena!
Heheh yaan acha tu, hapo ndo linapokuja suala la kujiongeza.
Wengine wanapitia njia ngumu na wengine wanapitia njia mdebweeedo kula keki ya taifa.

SUKAH
 
Hili suala so rahisi sana. Mishahara haiamuliwi na serikali pekee kwa kuwa si mwajiri pekee.

Sekta nyingi zina ajira pia upande wa sekta binafsi. Haya magap hata huko sekta binafsi yapo. Iwapo serikali itaamua graduates wawe na mshahara sawa basi italazimika kukubaliana na hali ifuatayo;

1. Kama kuna sekta zinalazimika kulipa watu wabunifu na wachapakazi, watumishi wa serikali wataondoka kwenda sekta hizo sekta binafsi ili walipwe kwa kadili ya ubunifu wao.

2. Hoja ya mishahara kuwa sawa haina mantiki. Mishahara inatakiwa kulipwa kwa uzalishaji na ubunifu. Kimsingi hata walimu wote kulipwa mshahara mmoja si sawa. Ilitakiwa mshahara uzingatie mazingira na idadi ya watoto wanafundishwa na kufaulu.

3. Mishahara ikiwa sawa kwa watumishi wa ngazi moja serikali yote tutazalisha tatizo kubwa zaidi. Nani atataka kufanya sekta ambazo zinahitaji nguvu na akili nyingi wakati kuna sekta mteremko? Ni jambo la fedheha kumlinganisha mtu wa policy and economic analysis wa BOT na Mchumi wa Halmashauri ya miji kwa kuwa tu wote ni wachumi.

Hawafanani majukumu na nguvu ya kuchakata taarifa za msingi inayotumika ni tofauti sana, na kama haitoshi athari za ubovu wa maamuzi kati ya hawa wawili kwa taifa hazilingani.

4. Mtu mwenye uwezo hana haja ya kulalamika uwezo wake unatosha kumhamishia taasisi inayolipa zaidi au hata kulipwa zaidi sekta binafsi.

Mara nyingi hatutambui uzito wanaobeba watumishi wengine.
 
Well said inauma ila ndo ukweli
 
Heheh yaan acha tu, hapo ndo linapokuja suala la kujiongeza.
Wengine wanapitia njia ngumu na wengine wanapitia njia mdebweeedo kula keki ya taifa.

SUKAH
hahahaaaa, kwakeli. cha kuchekesha tu ni kuwa hao wenye kikubwa ndiyo hao pia wenye mdebwedo katika kujiongeza
 
Back
Top Bottom