Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Sina chuki kwa Mugalu ila hoja yangu ni kwamba, kwasasa Simba Sc haina strikers wa maana, sio Mugalu wala Kagere. Kama unaitakia meme Simba Sc huwezi taka iendelee kuridhika na kiwango hiki cha Mugalu. Atafutwe striker mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Inaonekana mkuu kwa uelewa wako ni kwamba full backs anacheza kutokea kwenye boksi lake.
Maana effect ya Mugalu ilikua ni kuwa-pig together mabeki wa kati wa AS Vita, hold the ball, supply to midfielders and create chances.
Mwenzetu umekuja na Shaban DJUMA, a full back, kuthibitisha kwamba hoja yetu haiko sawa.

Daaah, una maajabu mkuu.
 
Ok mkuu, nimekubali Mugalu ni striker bora sana kuwa Sasa kwenye ligi ya Tz na kimataifa. Na simba haina haja ya kuhamgaika kutafuta mbadala wake. Mugalu ni striker hatari sana, kiasi kwamba atakuja kuoffer kitu kikubwa zaidi ya alicho offer Kagere tangu aingie Simba.Nimekubali [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliangalia.
Kwahiyo unataka kutuambia kule Misri angeanza Mugalu, tungetoka na matokeo mazuri zaidi ya yale ?

Kwako #Mwanamaji
Tusikite kwenye ''ange'' - ''ninge''.
Uliionaje ile build-up Kagere akiwa pale Mbele ?

Mimi niliona kama system inamtesa Kagere, anaonekana kama anazunguka huku na kule, kitu ambacho kwa maoni sioni kama ndivyo inapaswa kuwa.

Kama wewe unaona vile ndivyo build-up inavyopaswa kufanyika basi sawa.
Tukubaliane tu kwamba tuna mtazamo tofauti juu ya jambo hili.
 
Umeongea mambo mengi sana katika maoni yako. Kuna mengine nakubaliana nayo, mengine sikubaliani nayo. Ila niseme tu kwamba nayaheshimu maoni yako yote kama ulivyoyawasilisha.
 
Kumbe kazi ya Mugalu ni kuwa-pig mabeki wa Kati wa timu pinzani sio kufunga, kwamaana hiyo nafasi yake inaweza zibwa hata na beki,kwasababu beki atawa-pig vizuri kuliko mshambulijai[emoji23].

Nimekubali, Mugalu ni striker bora kuwahi kutokea Simba [emoji23].Simba inapaswa kumuamini, wala haina haja ya kushugulikia safu ya ushambuliaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli ana kosa magoli, ni kweli ni butu, ni kweli uwezo wake ni wa kawaida, tunatakiwa tutafute striker mwingine lakini kwa Washambuliaji waliopo na mfumo unaotumika yeye anabaki kuwa bora.
Kocha nayempanga sababu aliyotoa ni hii...

 
q


Mkuu, ina maana hujawahi kuona Aguero anakaba ?
Unajua kuna baadhi ya mambo humu tunatakiwa tuache kujadili bali tuanze KUFUNDISHANA
Mimi kuna vichwa humu naona hata kufundishika havifundishiki [emoji23][emoji119][emoji23][emoji119]
 
Mechi ya Al-Ahally na Simba pale Misri. Ni kati ya mechi bora kabisa na iliyochezwa kwa ustawi wa juu sana katika mwaka huu 2021 hapa Afrika na haikuwa na rafu nyingi.
Kumbuka Al-Ahally walikuwa nyumbani na wakaitumia faida ya nyumbani.
Wacheza wote wa Simba walicheza katika kiwango cha juu kabisa.
Hapo hata angekuwa huyo Mushimba asingefanya chochote zaidi ya hapo sana sana tungeweza kufungwa magoli mengi zaidi kwakuwa Mugalu hakabi, Kagere anakaba.
 
Umeongea mambo mengi sana katika maoni yako. Kuna mengine nakubaliana nayo, mengine sikubaliani nayo. Ila niseme tu kwamba nayaheshimu maoni yako yote kama ulivyoyawasilisha.
Kwahiyo Ikitokea umeulizwa kutoa maoni bila kuweka siasa (ambazo naona zimekukaa sana), juu ya eneo gani ambalo Simba inapaswa kulifanyia kazi Kati ya Safu ya mabeki,Kiungo na ile ya Ushambuliaji utagusia Safu ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona mapungufu yake yanajadiliwa kila mahali sijaona mtu anayekataa kujadiliwa.

Sijui unalalamika nini
 
NAUNGANA NA WEWE unaekubali madhaifu yake,na kukubali kwamba tunatakiwa tutafute striker mwingine. Kwahayo maelezo ni kwamba, inamlazimu kocha kumpanga kwakua hana mbadala. Ndomaana hata mimi nasema Simba haina Safu bora ya Ushambuliaji, yaani sio Kagere wala Mugalu wote ni magarasa tu.Kwa Asilimia kubwa Team inafunga kupitia mamidfilders na Wings.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi tukubaliane kutokukubaliana hivi,Magulu ajirekebishe anapopata chance tatu za kufunga angalau kama sio nafasi mbili basi hata moja aitumie vizuri kwa kufunga.
Isiwe sifa yake ya kuwazuia mabeki wasipande lakini akipata nafasi zaidi ya mbili yeye na kipa anakosa tena kwa mechi ziadi ya mbili,hii haitakaa poa.
Mashabiki wa soka siku zote tunapenda matokeo na kila mchezaji atimize majukumu yake kama ni striker basi akipata nafasi mbili ama tatu afunge.
Kama ni defender pia atimize majukumu yake kama mlinzi.
 
Unamuita Mugalu, Galasa.

Subiri wanakuja kukushambulia muda si mrefu.
Mugalu ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kuhold mipira inayotokea mbele kurudi nyuma.
Ndio maana mabeki wetu wanapumzika.
Mwisho anawasambazia mipira ma mido kama Chama na Wanafunga kirahisi.
Hii ndiyo shughuri ya Mugalu.
 
tuma CV yako kwa barbara
 
Asee kumbe bora umenisaidia kitu... ishu ya mkude... niliongea na watu adi nkajiona kwa vile mi sio mchambuzi na sijui sana mpira... mkude hakufanya majukumu yake ipasavyo.

Hata hivyo jaribu kuangalia comments za wengi hata ktk maswala mengine.... huwa kuna watu wakishacomment, inachukuliwa km ilivyo na comment inakua kwa mtindo huo huo kwa kila anaekubaliana nae.
 
Hicho ndo tunataka, sio habari za ukabaji alafu Kati ya nafasi 5 za wazi hapati hata moja, zote anazigeuza kosakosa. Hii hatua tuliyofika ni hatua inayohitaji zaidi magoli zaidi hata ya point 3,tukiendelea kwenda na hoja za ukabaji hatuwezi toboa.Jaribu kufikiria tumefungwa mbili kavu ugenini, alafu kwa mkapa sehemu ambayo tunahitaji kupindua matokeo ,tunatengeneza Zaid ya nafasi 5 za wazi ila hatugungi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yoyote atakae taka nikubaliane na hoja ya kwamba Mugalu anawasambazia mamido mipira Ili wafunge, aniambie kwanza huyo Mugalu ana assit ngapi kwenye ligi na kimataifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…