Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Kwa sasa pale Simba mimi kwa uzoefu wangu wa kufundisha soka kidogo siwezi kumpanga striker mwingine tofauti na Mugalu
Kagere anajua kufunga ila ni much dependent kwa kazi ya team yaani kama mnacheza na watu wachache juu na mnadefend kuzuia kushambuliwa kirahisi hutopata matokeo yake mazuri.Mugalu ile ball control aliyonayo na hata accuracy passing aliyonayo kamzidi mbali Kagere.Kama timu inaweza kupata matokeo kwa advantage ya striker kuwa strong kupigania mipira na washambuliaji wengine wakatumia mwanya wa gaps zilizoachwa wazi kufunga siwezi kumchezesha mchezaji ambaye anasubiri atafuniwe tu yeye anameza maana naweza kupata matokeo kwa njia nyingine ya middle zangu nzuri.

Nimewahi kutumia mbinu hiyo na kupata matokeo mazuri mno , yaani unakuwa na striker mwenye nguvu kazi yake kuwapa kivuli mabeki akina 10 ,8 ,11,7 wanapata urahisi wa kupenya kuichambua timu pinzani tunafunga goli.One match nakumbuka timu tulicheza wana beki mzuri mno (mzee wa kuosha mbele ) nikagundua wao walikuwa flopy kwenye middle so yule beki ndiye tegemeo lao kupeleka mipira mbele nikamwekea njemba inakaa nae kama ni mpira ukija beki anabaki kuhangaishana na njemba njemba anaweka kwenye njia 10 anazunguka anaweka nyavuni.Mipira ikawa haitoki nyuma kirahisi so mabeki wetu wakasogea juu na tukawabana vilivyo tukachukua ushindi mnono wa goli 8 though walikuwa wana awinga wazuri tu na 10 mzuri sana

Simba wanapaswa kutafuta striker mwenye uwezo wa kupiga chenga,kuhold mipira na kufunga , yaani striker ambaye anaweza kukusanya watu wawili hata watatu na kufunga maana ndicho tumekosa pale.Hawa waliopo wana mapungufu tunawatumia hivyo hivyo tu kibabe sasa huwezi kuchukua mtu dhaifu zaidi ukamweka benchi mtu dhaifu.

Kagere alishine kwenye mfumo wa Aussems aliyejiachia na kusahau deffensive roles zaidi ,Aussems aliamini kwenye kucheza tu si kuzuia kufungwa ,bali kufungwa huku tunafunga mwisho tuhesabu nani mshindi ndiyo maana wakati wa Aussems Kagere alishine cos timu ilikuwa inashambulia zaidi na alikuwa na washambuliaji hatari pale mbele na wote walicheza yaani BOKO ,OKWI NA KAGERE by now hatuchezi vile so kubalini tu maana huyu kocha anatafuta matokeo usidhani anatafuta kufungwa
 
Vita wanasema mchezaji aliyewapa shida sana katika mechi ya kwanza ni Mugalu

Kwani kwenye ile mechi Mugalu alifunga goli ngapi?
 
KAGERE anarudia Yale Yale kocha asiyopenda.

Anarudia Sana nyuma,

Hii inasababisha mabeki wa Al ahly kupanda kushambulia.
Na hii ndiyo sababu Mugalu anapewa namba zaidi , hata mimi siwezi kumpanga Kagere mbele ya Mugalu ,never unless nicheze mpira ule wa Aussems
 
Sahihi
 
Hata hapo watabisha ila umeongea ukweli 100%
 
Hii lugha ya Mugalu kuwazuia mabeki wa timu pinzani wasipande sijui imetokea wapi!!
Mechi ya As Vita Vs Simba kule Congo Mugalu alikuepo na wing backs wa As Vita walikua wakipanda kushambulia akiwepo na yule beki wao kile kiandunje Shabani.
 
Hii lugha ya Mugalu kuwazuia mabeki wa timu pinzani wasipande sijui imetokea wapi!!
Mechi ya As Vita Vs Simba kule Congo Mugalu alikuepo na wing backs wa As Vita walikua wakipanda kushambulia akiwepo na yule beki wao kile kiandunje Shabani.
Hao ni washabiki lia lia wa Mugalu.
Uzuri wanakubali kuwa sio mfungaji mahili wa magoli mahili.

Ndio wameamua kumpa cheo cha mshambuliaji Mkabaji.

Yaani yeye jukumu lake ni kukaba pale ndani ya 18. Kuwakaba mabeki wasiokoe mipira.

Sasa sijui akiisha wakaba nini kinafuatia.
 
Kwahiyo Mugalu ni mshambuliaji au Mkabaji.
Maana tunaweza kumlaumu bure kuwa hafungi kumbe sio jukumu lake.
Mkuu naomba ushauri nikusikilize wewe au mosimane?......
Sio kila mfumo unahitaji finisher mzuri afu hajui kulink timu, ndo maana kukawa na mifumo ya mpira kila kocha na mbinu zake.
Kagere kwenye mfumo wa simba wa sasa hafit, anzia kwa Sven pia huyu wa sasa, ina maana wote hawa hawampendi?

 
Oliver Giroud hufunga goli ngapi mkuu?
Kwanini ilikuwa humkosi kwenye kikosi cha France?
 
Hiyo chati yako inasema wazi kabisa kwamba Mosimane anamfagilia Luiz Miquissone. Na ametaja na wasifu wake kwa timu nyingine alizo zichezea.

Mwisho kamtaja Mugalu na Kagere kuwa nao ni washambuliaji wa kuwachukulia kwa tahadhari.

Lakini wewe unasema Kagere hafiti katika timu ya Simba tofauti na alichokitamka kocha Mosimane.

Kocha hapo anamsifia Luiz. Ndio nilivyo elewa na kwakuwa aliwafunga katika mechi yao ya awali.

Sasa labda utufafanulie, hapo Mugalu na Kagere wamesifiwa kwa jambo gani. Kukaba au kufunga ?
 
Ulitaka nicrop ili useme nimetunga? Nilichofanya hapo nimekupa page ...yote usome mwenyewe.
Mshambuliaji wa kisasa ni zaidi ya kusubiri ulishwe, mpira wa hivyo umepitwa na wakati...
 
Ulitaka nicrop ili useme nimetunga? Nilichofanya hapo nimekupa page ...yote usome mwenyewe.
Mshambuliaji wa kisasa ni zaidi ya kusubiri ulishwe, mpira wa hivyo umepitwa na wakati...
Basi nikubaliane na wewe kwamba Mugalu ni Mkabaji mahili, katika eneo la mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…