Hatua tuliyofika CCL kwa sasa (robo na nusu fainali),ni hatua inayohitaji wingi wa magoli zaidi ya point 3,Ili kijihakikishia nafasi ya kusonga mbele ila siyaoni hayo magoli kwa Mugalu. Ukweli ni kwamba kwa asilimia kubwa, Simba inashinda kwa skills na magoli ya midfielders na sio uwezo wa Mugalu kutulia na mpira akisubiri timu ipande, kama ni hivyo tungeona ana idadi kubwa ya assist lakini hana. Sasa kama hafungi, hana assist za kutosha anafaida gani mbele? Kama sifa yake kubwa ni kukaba, basi yule no beki na sio mshambuliaji kama yalivyo majukumu yake.
Kuna wengine hapa wanasema sijui mfumo sijui nini, angalieni hata mechi za Ligi kuu, Tangu Gomez awe mocha mkuu, na kumtumia Mugalu mtagundua kuwa kuwa Asilimia kubwa ushindi wa simba umekuwa ni wa Goli moja moja licha ya kutengeneza nafasi nyingi, ambazo mwisho wa siku Mugalu huzigeuza kuwa kosakosa langoni mwa wapinzani. Utakuta wafungaji ni akina Chama, Morrison, Miqiusone ambao wote hao ni mamidfilder. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa huyo anaesifiwa kuhold mipira kwenye 18,hahusiki sana kwenye hayo magoli ya hao mamidfilders[emoji23].
Ukweli usemwe bwana, Simba Sc inakosa mshambuliaji wa maana pale mbele. Kule kwenye page za Caf wanatamba Miqiusone Na Chama na hata kwenye kikosi cha wiki wanaingia hao , inamaana wao hawaoni uwezo wa Mugalu kukaba kama nyinyi mnavyopiga kelele humu,au wao hawajui hilo soka la kisasa,kwamba nyie ndo mnalijua sana [emoji1][emoji1][emoji1]? Na hata asilimia kubwa ya mashabiki wa Simba utawaona wanajivunia Chama,na Miqiusone na sio Mugalu. Leo hii watu wamemsahau Okwi na mkude kwasababu ya performance ya Miqiusone na Lwanga,ila bado wanamiss Fraga ambae ni majeruhi ,kwa sababu hilo garasa Mugalu Galina chochote cha ku-offer kwenye team.
Huyu Mugalu atakuwa kawaroga,sio bure.Ile mechi na As vita kwa mkapa,kama tungefungwa na kutolewa, kwa zile nafasi alizopoteza,sidhani kama mngekuja na huu utetezi wenu. Nilichogundua ushindi wa Simba sc ndio unaowapa upofu.
Sent using
Jamii Forums mobile app