Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Nchi hii ni Tanzania, alikuwa Rais wa Zanzibar na wa JMT. ANGEWEZA KUZIKWA sehemu yoyote ndani ya JMT
 
Ni 'suala'
Siyo 'swala'-mnyama

Hilo moja; la pili umeandika utumbo mkuu!
 

Kumbe huna facts, umeweka hisia, sasa usisimange wenye hisia wenzako.
 
Kwani ndugu zake wengine walizikwa wapi? Biladhaka alikuwa na kaka, wadogo zake, baba mdogo nk
 
Rais Samia Hassan na Wenzake kwenye hili la kumzika Hayati Mwinyi Zanzibar tunawaombea Mungu ashughulike nao kwa haraka na wepesi mkubwa na mzito
 
Tatizo hujaja na facts bali hisia ambazo hazileti mantiki.
 
Jana nilikuwa Unguja,huu Msiba tunasikitika wabara tu,wazenji hawana habari na sijui hapo Amani leo itakuaje,ila kama mtu alisema azikwe Mkuranga,kumpeleka kisiwani ni kukiuka wosia
 
Umeelezea vizuri ndugu kina nani kwanza hao wanaolilia azikwe mkuranga? WAPUMBAVU tu hao
 
wewe kwenu ni bara?
Mimi m'bara original mkuu. Kuwa na mawazo tofauti haimaanishi kuwa mtu sio m'bara. Maana hata Hussein Mwinyi kwao bara, lakini kaamua baba yake azikiwe Zanzibar.

Kuna watz wengi walitoka mikoani kuja Dar, na bado wakifariki wanazikiwa hapa hapa Dar sio mikoani kwao.
 
Ndugu hao vijana wanabisha mambo wasioyajua. Huyo anaekwambia kuzikwa kifamilia huko kijiji ni jambo la mila na desturi. Anajifanya hajui kuwa 70% ya watu waliotoka mikoani kuja kutafuta maisha Dar huzikwa hapa hapa Dar es salaam na sio mikoani kwao.

Mbona hajawahi kubisha au kushangazwa na hilo?
 
Angezikwa Mkuranga, Dr. Mwinyi urais wake Zenji ungekoma 2025.

Mkakati ni mkakati....
Raisi na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Zanzibar uraisi wake ukome 2025 tena kwa serikali hii ya CCM πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hata kura aliiba na hakuna kilichofanyika dhidi yake. Yuko ikulu anakula bata.

Nafikiri unatania tu mkuu wala haukumaanisha...
 
Jana nilikuwa Unguja,huu Msiba tunasikitika wabara tu,wazenji hawana habari na sijui hapo Amani leo itakuaje,ila kama mtu alisema azikwe Mkuranga,kumpeleka kisiwani ni kukiuka wosia
Tatizo hizi zote ni tetesi tu, hakuna mtu aliesikia wala kuona Mwinyi aki usia kuwa akifa azikiwe Mkuranga.
 
Umeelezea vizuri ndugu kina nani kwanza hao wanaolilia azikwe mkuranga? WAPUMBAVU tu hao
Wapo humu humu na wameanzisha uzi toka juzi usiku baada ya kusikia serikali imetangaza kuwa mzee Mwinyi atazikwa Zanzibar.
 
Umeandika vizuri na kwa ustadi mkubwa. Nafikiri wengi wakisoka andika lako watakubali kuwa wewe ni mtu mwenye akili kubwa humu jukwaani.
 
Unaishi njombe huko ndani ndani hujui mwinyi tangu kastaafu anaishi mikocheni !


Tuma ndugu zako walioko dar waende sehemu inaitwa mikocheni Kwa mwinyi
Hii mada ukiwa mlevi na unaisoma umelewa, hauwezi kuelewa kilichoandikwa.

Ndomaana nimeku quote leo maana najua pengine pombe za jana zimeshakutoka. Haya rudi tena kasome uzi uelewe nilichoandika.
 
Nchi hii ni Tanzania, alikuwa Rais wa Zanzibar na wa JMT. ANGEWEZA KUZIKWA sehemu yoyote ndani ya JMT
Sasa kama angeweza kuzikwa sehem yoyote ndani ya JMT mbona kuna watu wanalalamika yeye kuzikiwa Zanzibar? Kana kwamba Zanzibar sio sehemu ya JMT!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…