jambo ambalo halijathibitishwa ni kwamba, hata kama alikuwa navyo mkononi au mfukoni, hizo ni mali zake ametoka nazo nyumbani kwake, hakuna uthibitisho kwamba wakati akitoa ushahidi alikuwa anasoma, na kusoma haikataliwi kama ataiomba mahakama ili arefresh, huwa inaruhusiwa, sema hakuomba kurefresh na hakusoma. kwahiyo kuishika tu wakati huwa kunakuwa na nafasi ya kuomba kurefresh kama atakubaliwa, sio kosa. sasa ninyi wanasheria wa dcm msio jua kitu mnaona kama ndio mmeshashinda kesi, na mawakili wenu hawawaelekezi vizuri wanaendesha kesi kisiasa. kushika tu diary kuna kosa gani? pale ni open court, kuna watazamaji kibao, makarani, wafuasi wa chadema, waandishi wa habari, point of focus muda wote ipo kwa shahidi watu wote macho kodoo kw a shahidi kwasababu ndiye anayeulizwa maswali na kuyajibu, pia mawakili wa utetezi wapo wanamwangalia muda wote ili wapate wapi pa kumwuliza, hawajamwona anasoma diary wala kusoma msg za simu....uutasema kuna kosa gani limetendeka hapo?
halafu, shahidi yeyote, awe wa jamhuri au shahidi wa mshitakiwa, kabla hajaingia pale kizimbani huwa kuna nafasi ya kwenda kuendaliwa. hata mashahidi wa mbowe kabal hawajaingia kizimbani watachukuliwa na kina kibatala kwenda kwenye chumba cha siri wakamwandae pre-trial, kwa hiyo kwa akili zenu mnafikiri kwa ushaidi wa askari polisi kutakuwa na kitu kama walikuwa na nia ya kumfundisha watakuwa hawakumfundisha hadi aingie kizimbani? mbona mna akili finyu sana ninyi?