Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Hakuna ukamanda kwenye njaa, Hakuna mwanasiasa wa kupigania maslahi yako
Kwani hawa kina Mdee wana njaa?!!!

Watu walioweza kujikusanyia karibia BILIONI 1 kwa miaka 5....wakiwa hii Tanzania YETU...hiihii!!

Ninaunga mkono wazo la WAO kwenda BUNGENI KUAPA kwani ninawakumbusha kuwa CUF hawakuyatambua matokeo ya mh.Dr.Shein kwa ule UCHAGUZI wa marudio...waliamua kukaa NJE YA baraza la WAWAKILISHI....

Dr.Shein na baraza WALIENDELEA.....

Nina imani kuu ya kwamba ACT WAZALENDO hawatayarudia tena kipindi hiki...
Ninaamini HAWATOSUSA tena BARAZA LA WAWAKILISHI...

Ninaamini WATAYAINGIA MARIDHIANO....

Sasa kwanini akina MDEE na BAWACHA walisuse bunge la JMT?!!!

Muda utaongea.....
 

Kuhalalisha haramu kunasaidiaje kukomaza demokrasia nchini?
 
Kuhalalisha haramu kunasaidiaje kukomaza demokrasia nchini?
Mkuu...

Wabunge wa VITI MAALUM wanatokana na KURA ZA MGOMBEA WAO WA URAIS....

Mh.Tundu Lissu amepata kura 1.9M+...

Iwe hata kama ni kura ambazo NINYI MNAZIDOUBT....

Iwe hata kama ni kura ambazo NINYI MNADAI ZIMEPUNGUZWA...mwishowe "zilizobaki" na kutangazwa ni hizo hapo juu...

Kwani CHADEMA kimefutika?ni kwanini leo hii WABUNGE WA VITI MAALUM(literally hawakupigiwa kura majimboni) WASIENDE BUNGENI?!!!

Hebu BAWACHA wazitendee HAKI kura za HESHIMA alizopewa mh.Tundu Lissu bara na Zanzibar.....

Yaani WAKAE nje ya BUNGE wasubiri uchaguzi Mwingine wa 2025?!!
Kukaa kwao NDANI ama NJE kutabadilisha URAIS wa mh.Magufuli?!!
KUTABATILISHA bunge la JMT?!!!

CHADEMA wajifunze kilichowakuta WAWAKILISHI WA CUF mwaka 2015.....
Katika mazingira ambayo bwana JECHA "alifanya" yaliyoshuhudiwa....hakukufuta URAIS WA MH.DR SHEIN(Leo mstaafu buheri kabisa)...

Katika mazingira ambayo BWANA JECHA "alifanya" yaliyoshuhudiwa....hakukufuta BARAZA LA WAWAKILISHI(wamestaafu na kiinua mgongo juu)....

HARAKATI ni safari ndefu.....
JAZBA NA HISIA hazisaidii katika UTULIVU WA UHALISIA.....


MAENDELEO HAYANA VYAMA.
 
Maandishi wa mitandaoni, wengi wana kazi mbadala. Wanamdanganya nani sasa? Wengine bila siasa hawaendi chooni
 
Ndugu una uthibitisho gani kwamba Halima anahusika? unamjua vzr Halima Mdee? unadhani anatumia utumbo kufikiri kama wengine?....kukataa viti maalum Chadema haimaanishi wengine hawavitaki maana ni fursa na ukikuta jina limeena kwa meneja kampeni wa cccm wee muite mkurugenzi wakutangaza! manake hao sio wanawake wa Bawacha ni wachumia tumbo... habari ya viti maalum ilishakwisha
 
Utetezi unaoweza kutolewa:
1. Hii ni haki yetu wala sio fadhila maana ni sehemu ya kura ambazo tulistahili kupata.
2. Hatuwezi kukubali ruzuku wakati tumekataa ubunge wakati vitu vyote viwili vimetokana na sehemu ya kura tulizostahili kupata.
3. Na chama kitakuwa na wakati mgumu wa kujiendesha, kusimamia kesi bila ruzuku na michango ya hawa wabunge.
4. Tutaendeleza mapambano ndani ya bunge kuwapigania wananchi wetu na kuainisha makosa ambayo serikali watakuwa wakiyafanya kabla hayajatokea.

Vitu ambavyo havitasemwa:
1. Wananchi sio wa kuwategemea. Hawatatuchangia kukiendesha chama pamoja na maneno yao ya kwenye mtandao. Kuendesha chama ni tofauti na kuchangia mara moja faini za viongozi.
2. Wananchi bado hawana muitikio wa mapambano magumu yaliyopo mbele yetu. Mfano ni wao kutojitokeza kwenye maandamano tulioyaita.
3. Hata tusipoenda, C CM watafanya wanalolitaka kama walivyofanya Zanzibar mwaka 2015.

Amandla...
 
Mnataka wasiende nyie mtawahudumia kwny kukidhi mahitaji yao ya kila siku wao na familia zao?!!!Acheni unafiki,juzi tu mmeambiwa na viongozi wenu ingieni barabarani kuna aliyejitokeza?!!!Halafu leo mnapiga kelele mkiwa kwny keyboard zenu,kama fursa ipo kikatiba acheni wakatengeneze pesa ya uhakika mjengoni,YOLO.
 
Hivi inaingia akilini kweli kwa mtu kukimbilia bata Ulaya/Ubelgiji halafu unawakataxa wenzako wasipate mshahara kwa miaka 5?. Familia zao zitajokimu vipi?

Huo ni ubinafsi wa hsli ya juu sana, kwani nani kasema wanawake wakiingia bungeni hawawezi kuwa wapinzani?
 
Inaonekana una Njaa sana wewe Kicheche
 
Hapo ndipo Upinzani wa TZ unapokwama,yaani kila mtu anatafuta shibe,kwa hiyo mtu yupo tayari kusaliti maamuzi ya wenzake kwasababu tu kule kuna msosi,njaa mbaya sana inaondoa hata akili na utu.Nadhani wamekusikia.

Dah...hivi unadhani kuna mwanasiasa yoyote bongo yuko kwa ajili ya wananchi? Hebu tufanye kazi za siasa ziwe za kujitolea uoine hata kama uchaguzi tutauhitaji...jiongeze [emoji2960]
 
Umeandika madini matupu, mihemko na kususa hakujawahigi kuwa solution kwenye jambo lolote
 
Ikiwa hilo litatokea itakuwa ni ushahidi tosha wa kuthibitisha walichokuwa wanapigania sio maslahi ya wananchi bali ni maslahi yao wenyewe na sasa inadhihirika wazi wana njaa kali
 
Kwa vile ni vitu vinavyofanyika chini ya jua ccm wanaweza kufanikisha zoezi hili haramu... na je kwa nini wanawahitaji wapinzani sasa kuliko wakati mwingine wowote? haya mapenzi mema ya ccm yametokea wapi?
Kama chama chenu kinahubiri kuwa haki haiombwi bali huchukuliwa, basi nao waacheni wachukue haki yao.
 
Kwani maslahi ya umma ni kukataa kwenda? hizo nafasi ni kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo, hopefully kwa idadi ya kura za urais!!
 
If possible wafukuzwe kabla hawajaenda wanaharamu hawa yaani watu wauwawe wamwage damu za watu , halafu Halima Mdee na kundi lako muende mkabaliki mauaji waliyoyafanya ccm .
 
1. Hii siyo haki yao, haki haipatikani katika haramu, ingekuwa ni haki yao kama hizo nafasi zingepatikana katika uchaguzi wa haki siyo katika hili zoezi haramu la kijambazi

2. Hata kama ingebidi wabunge wa viti maalum waende huko bungeni, sharti ni kuwa majina lazima yapelekwe NEC na katibu mkuu na si wao wenyewe kujipeleka

3. Kuhusu ruzuku, hakuna ruzuku itokanayo na uchaguzi mkuu huu ambayo imeshapekekwa Chadema. na hili Chadema naamini watalifanyia kazi

4. Hata wakienda CCM wataendelea kufanya wanalolitaka.

Bottom line ni lazima kuprotest haramu ili uwe na moral authority ya kutaka haramu iondoke kwa ajili ya manufaa ya chaguzi zijazo. Kushiriki vikao vya kula nya ma za watu huku ukijifanya unapiga vita kuua watu ni unafiki, na wachawi wenzio hawatakuchukulia serious.

Kupambana na udhalimu inahitaji subira na uvumilivu na persistence siyo kusurrender kirahisirahisi kwa mtindo wa if you can't beat them, join them!
 
Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Hakuna cha kuelewa hapo! hapo ni U-ccm tu unawasumbua, yaani kwanini wao wakapate hiyo posho!! Waacheni waende kama ambavyo waliishachaguliwa!! Kama uchafuzi uliisha hesabiwa kuwa umeisha, maisha yaendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…