Suala la Viza ya Marekani na Canada Serikali ya Tanzania ivunje ukimya, foreign affairs watimize majukumu yao

Cha kushangaa Canada hawakuwa na shida kabisa nao wamekuwa wapumbavu kabisa kiasi kwamba consular section yao ni upuuzi mtupu.

Jamaa yangu wamempa viza ya miaka 10, akaingia Toronto then alikuwa US pia, akamaliza issue zake anarudi Toronto then akaja Bongo.

Alishapiga hizi Ingia toka nyingi Bongo Canada Bongo, na hafanyi illegal deal zozote zile, Sasa passport yake ilivyoexpire ameomba Canadian viza wamemnyima, na previous travel record yake iko vizuri sana, sasa sijajywa bado nini kinaendelea kwa hawa mapacha Wawili, is not fair at all.

Binafsi nimecancel trip kwa mwaka huu maana huu utumwa siuwezi kwakweli.
 
Miezi sita viza? Hao hawataki watu waende kwao.
 
Sikushauri ku cancel mkuu, kama trip zako zina umuhimu just waelewe tu. Hizi nchi zao zina mzigo mkubwa sana, hata zile nchi mahasimu wao ndiyo zinaongoza watu wa nchi hizo kukimbilia huko.
Ukiona wameanza hizi mambo, ujue kuna taarifa za kijasusi hivyo wanajaribu kufanya filtering ili ku mitigate risk au wameona fursa zilizopo zinaweza zika vanish very soon na kujikuta into Jeopardy.
Kuwa super power siyo jambo jepesi.
 
Sahihi.
 
Canadian Visa ni simple sana (study Visa and Spouse Visa)

Miezi minne tu umepewa visa

Tourist Visa ndugu zangu kusubiri ni balaa (kwanini)

Kwasababu Canada sasa wao wameamua kwamba ukiwa na Tourist Visa ukifika hapa unaweza kuibadilisha kwenda Work Visa ya Miaka 3 then ukawa na Canadian experience ukaomba PR (Canadian Tourist/Visitor visa ni pathway to PR kwa sasa)

Nchi za dunia ya 3 zinaona hilo gap ni zuri na halipaswi kuacha ndio maana wanakua wagumu kwa hoehae.

Sasa wanawazingatia watu wenye pesa kwanza ambao wanajua wakifika hapa wataacha mpunga.
 
Wao wazungu siyo kwamba hawafanyi cheating, CIA wenyewe wakitaka kusafiri kwa fake identity wanafoji passport za nchi nyingine.

Kuna tajiri nilikwenda kwake Nice France hana hata mfanyakazi mmoja Nyumbani kwake mfaransa mwenzake, ni wa Morocco na wapishi Wabongo na Wabongo anawachukulia tourist viza tu.

Kwahiyo point yangu dunia huu ukikaza sana maisha yanakosa maana, Mimi nawakubali sana Shenghen countries ukitimia documents viza yao hawana mbambambaa, ndivyo inavyotakiwa kuwa, na siyo kama hawa mapacha wanavyotutesa sasa hivi.
 

I hear you. Ni utumwa hakika.
 
Kuna taarifa kuwa baada ya Corona Canada walitowa viza nyingi sana kwa Waafrica na hasa ukanda wetu.

Kuna video clip zilisambaa watu Waafrica hawana shelter na wanafosi Asylum seeker, je kuna ukweli wowote? Na hili limechangia kwa Wacanada kufanya wasieleweke na kubania viza?
 
Hapana mkuu hawa wazungu nawajuwa vizuri, wakianza mawenge wapotezee kwanza.

Nakumbuka kipindi Tony Blair akiwa Pm wa UK, British high commission Dar ilizinguwa kinoma issue za viza mpaka wakawapa uwakala Wahindi Mara sijui viza inatoka South Africa upuuzi mtu.

Mimi nikishaonaga mawenge ya hivyo huwa na Mimi natumbukia nyongo vilevile.
 
Dereva wa bodaboda una hasira sana, ila nakuelewa. Hivi umeshaletewa taarifa kuwa mnatakiwa kuanza kulipia 65,000 kwa mwaka kwa kila bodabodašŸ˜€
Kwenye hilo suala mama ataupiga mwingi muda si mrefu
Habari itakuwa hivi;
"Mama afuta kodi ya bodaboda
Mama ana upendo nani kama mama".

CCM ni mabingwa wa kuanzisha matatizo na taaruki
Baadae wanasema tumezifuta
 
Hayo mambo ndiomaana nkitoka tz lazima nichukue uraia wa marekani au canada
 
Mkienda huko mnafaidika Nini? Mbona hatuoni Mabilionea kutokea US na Canada Bali ni Akina Vunjabei na dai wa hapahapa?
 
Mnalazimsiha kwenda us na canada ni kwa mama zenu kule? Tulizeni rinda bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…