Suala la Viza ya Marekani na Canada Serikali ya Tanzania ivunje ukimya, foreign affairs watimize majukumu yao



Huna haki yeyote ngozi nyeusi, bora ujue mapema.
 
Tatizo la wabongo mnachagua ccm mnataka mkibilie us na Canada tulia hapa mkale matunda ya kazi yenu,wao wangekuwa wavivu nchi zao zingekua hivyo,au kama vipi omba visa ya Urusi ni rahisa sana kuipata,Jana wamezindua bomu kubwaaa la masafa marefu kuwaitokea.
 
Sijawahi kuonaga mtu mzima kichwani aliyetoka Urusi, refer Dr Shika.
 
Acha fikra potofu,wewe Kama umekubali kusubilia kifia bongo tulia,hii inshu inatuusu tunaojielewa
Badala upambane unawaza kukumbia tulia, katika ile mitano bado miwili Kisha mitano tena.

Jiulie swali kwanini raia wa us na Canada wakitaka Kuja bongo wanagonga free entries kwanini isiwe sawa na kwetu kwenda USA na Canada? Wabongo tutulia tule matunda ya mitano tena ndio aya.
 
Shirika la Human Rights Watch na Amnesty International wanasema Canada inawashikilia maelfu ya waomba hifadhi kila mwaka katika mazingira ya unyanyasaji ambapo watu wenye rangi tofauti (hususani weusi) wanaonekana kushikiliwa kwa muda mrefu mahabusu wakiwa wanasubiri vibali vya kuishi nchini humo.

Kwa lugha nyepesi, baada ya kupata Visa hapa Tanzania halafu ukaenda huko kutaka kuzama, utakamatwa na kuwekwa kizuizini/mahabusu mpaka kieleweke.

Watanzania msidanganywe kwenda kutumika huko!
 
shida ya Kwanza ni ngozi yetu,shida ya pili nchi yetu+viongozi wetu.anyway ila Mimi nitatoka tu.ila wewe uko wapi?
 
Wakenya hao waliingia wengi na kuomba asylum,wacanada wameshtuka ndio maana wanabana kutoa visa
 
Atake asitake ni mitano tena.😀😀
 
Siyo kweli, tusidanganyane. Hakuna "free entry" kwa raia wa US na Canada kuingia Tanzania. Wanalipia visa, tena inategemea anakuja kufanya nini. Sema wao hawasubiri kupata,wanagongewa kabla au wanapoingia, siku hizi kuna e visa, kwa mtandao tu. Sio kama sisi tukitaka kwenda kwao tungoje.

Jionee gharama za visa wanazolipia wao:

 
Siyo Canada tu, hata Uingereza nimekweda bila viza 1995.
Siyo kweli. 1995 UK ilikuwa tayari unahitajika kuwa na Visa kabla hujaenda.

Tena walianza kuwa strict 1992/3 kwa Wimbi la wasomali lililokuwa linakwenda, Tanzania tulikuwa tunawapa passport wasomali kama njugu, baada ya kupinduliwa Siad Barre 1991.

Tuliharibu miaka ya 80's

1995 Labda ndege walikupakia kimagendo bila visa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…