Suala la Viza ya Marekani na Canada Serikali ya Tanzania ivunje ukimya, foreign affairs watimize majukumu yao

Siyo kweli. 1995 UK ilikuwa tayari unahitajika kuwa na Visa kabla hujaenda.

Tuliharibu miaka ya 80's

Labda ndege walikupakia kimagendo.
Punguza ujuwaji, walioharibu Uingereza ni wapemba baada ya Maalim Seif kuporwa ushindi na Ccm kwenye uchaguzi wa 1995 wapemba wengi na vijana wajanjawajanja wa kariakoo walikimbilia Uingereza na claim yao wote ilikuwa ni political asylum.

Watu wengi walioingia Uingereza kipindi hicho ninaowafahamu Mimi wote sasa hivi wana Uraia wa Uingereza, hii ndio sababu kubwa ya sisi kufutiwa airport entry wakabaki Malawi nadhani na Kenya.
 
Mkuu kama hujuwi kwa sasa Canada inatoa viza kulingana na expire date ya passport yako.

Jamaa wanatoa viza miaka 10 au 7 kulingana na PASSPORT yako inaisha lini.

Ktk kipindi ambacho Canada wameruhusu kutoa viza ni sasa.

Ni kwl wanaweka appointment muda mrefu Ila ukiingia maombi unakula viza miaka 10 tena multiple.
Kwamba unaingia na kutoka utakavyo.

Jamaa wapo vzr,,Sana,,

Nyooka na documents zako tu.

Passport date of expire 30/3/2033
Na viza inawekwa hadi 2033 kuanzia siku unawekewa viza hadi 2033 inaexpire date.
 
Jambo lakushangaza sana pamoja na kuishi kwenye nchi tajiri ccm wameuza uridhi wetu na kututumbukiza kwenye dimbwi la umasikini kwaujinga wetu wenyewe,leo hii maisha magumu ukitaka kukimbia unakutana na vikwazo vya visa, ccm watuambia ni wavivu tunadeka tujiajiri.
 
Unafikiri Kwanini watanzania tuchukuliwa kama katuni na developed countries?
 
usiandike uongo
 
Raia wa Us akienda Tanzania anaomba visa na anailipia mkuu. Canadians ndio wanagonga entry
 
Raia wa Us akienda Tanzania anaomba visa na anailipia mkuu. Canadians ndio wanagonga entry
Hata kama wanalipia lakini kwangu kama msafiri naona ni nafuu na rahisi kuliko sisi kutoka huku kwenda kwao.
Ila katika international travel kinacho matter ni Passport yako na sio mfuko wako.
 
Hata kama wanalipia lakini kwangu kama msafiri naona ni nafuu na rahisi kuliko sisi kutoka huku kwenda kwao.
Ila katika international travel kinacho matter ni Passport yako na sio mfuko wako.
Yeye alisema hawahitaji visa ndio maana nikamfafanulia hayo. Sikuongelea urahisi wala ugumu.

Hizo passport zimekuwa bora sababu ya nchi zao kuwa vizuri. Na sio uzuri wa majengo tu ni pamoja na uchumi na ndio maana hakuna nchi maskini yenye passport yenye nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…