Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Mazoea Yana TABU....

Wako Wanaosema ni SADAKA KWA WANAOKUJA KUMZIKA MAREHEMU kwa kuwa huwajui hali zao walizonazo na walizotoka nazo.
(Ukichunguza ni kweli kwani wako wanaopata habari za msiba wakiwa kwenye mishe zao na hawana kitu ukiacha nauli,wako wale ambao walikuwa wanakaribia kwenda majumbani kwao,wakaghairi na kuja msibani huku wakiwa matumbo matupu Kabisa,wako wale walalahoi ambao habari za msiba zimewafikia na wana nguvu ya kuja msibani na msiba wenyewe UNAWAHUSU,wako vijana wadogo under 18 ambao hawana vipato vya kazi lakini wana ari ya kuja msibani kwa mpendwa wao).

N.B Sijapatapo kuona eti kwa kuwa NYUMBA YA MSIBA haijapikwa ama hawana kitu na kupelekea KUKOSA HUDUMA ZA KUMZIKA MAREHEMU na hata Kukosa ndugu watakaolala zile siku 3 za MATANGA(labda Kama wameamua iwe hivyo).
 
Je, mchungaji aliyekuja kuzika anapochukua sadaka yake kwani ni yeye kafiwa? Yaache yakae yalivyo watu siku hizi hawafikiri zaidi ya pua yao
Ule ni wizi kama wizi mwingine.

Ndio maana tunasema dini ni utapeli kama utapeli mwingine, Mungu hayupo.

Eti kwenye msiba mchungaji ama padri anakusanya sadaka ni mali yake, yaani analipwa kutoa huduma ya kiroho, huduma ya kiroho inalipiwaje hasa kwenye msiba?
 
Huyu hashirikiani na wenzie mtaani anapoishi!
 


Haswa swahibu, ni ukweli mtupu usiokuwa na shaka.100% ✔✔

Utamuona mtu eti anaenda msibani kwa ajili ya kula tu, yeye siku zote ni kuangalia wapi kuna msiba ili ale. Na asiposhiba utamuona akihangaika kupata shani nyingine, akishiba utasikia akisema; "huu ubwabwa mtamu", kasahau kabisa kwamba pale ni msibani na ni jukumu la watu kuwachangia wafiwa rambirambi kama faraja kwao.

Jambo linalotakiwa ni kwa wafiwa kuweka ngumu kupikia watu wa karibu chakula ili somo lizoeleke miongoni mwa jamii zetu, na hakika hili ni fundisho la uisilamu.

Hongera swahibu kwa kutukumbusha jambo hili.✔✔
 
Jomba hujui watu wanakulaga michango yao....
 
Kiuhalisia hili swala linakera.
Juzi nomepakiwa na bodaboda alikua analalamika jana yake wametoka kuzika na familia haikuwa na kitu...ikalazimika kukopa na kuandaa chakula kidogo nacho hakikutosha raia wakaanza kulalamika kuwa hawakushiba!
Halafu kuna mijitu inashinda msibani kuanzia asubuhi hadi usiku yupo tu na anakula chakula bila kuchangia hata senti eti anamfariji mfiwa, wengine wanalalamika msibani unakuta nyumba imejaa watu wanalala sebuleni, vyumbani hadi nje.
Ni utaratibu wa kipuuzi sana, wanatakiwa wabaki watu wachache wa karibu wasiozidi kumi.
 
Uchoyo na roho mbaya vinakusumbua,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…