Hii nayo ni tabia ingine inayopaswa kupigwa vita,yani huoni huruma mtu kafiwa na mumewe yuko mnyomge anahuzunika na majonzi moyoni alafu hapohapo unachukua pesa kweli ?Je, mchungaji aliyekuja kuzika anapochukua sadaka yake kwani ni yeye kafiwa?
YES SASA HUU NDIO UTARATIBU NZURI SANA WA KUFUATWA.Kwa sisi wanyakyusa msiba ni ibada ya shukrani. majilani na ndugu huja na vyakula vyao msibani na kuweka kambi hapo mpaka matanga ya ishe.
Yes mkuu ukifa huna uwezo wa kusimamia msimamo wako,utasimamiwaNilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.
Mii nimependa huu ubeti... Kwa jinsi ulivyo jitoa, Ya kwamba nikifiwa! Na sio nikifa!
wapi hiyo mkuuJe, mchungaji aliyekuja kuzika anapochukua sadaka yake kwani ni yeye kafiwa? Yaache yakae yalivyo watu siku hizi hawafikiri zaidi ya pua yao
Uzi wangu unasema suala la wafiwa kuandaa chakula..Mkuu chakula msibani ni mila ya kiafrika na ipo karne nyingi.
Kimsingi wafiwa wao hawapiki wao wenyewe kwa ajili ya msiba bali jamii inayo mzunguka mfiwa.
Nia ya mila hii ni kuwapunguzia wafiwa ukiwa na kuufanya msiba uwe wa jamii nzima.
Ukiitazama juujuu utafikiri msiba na kulisha waombolezaji ni jukumu la mfiwa, la hasha.
Tatizo linakuja pale mfiwa akiwa hana uhusiano mzuri na jamii inayomzunguka au hahudhurii misiba ya jamii yake.
Hapo mfiwa anaipata fresh.
Mila ya kuwapa waombolezaji chakula kabla ya mazishi ina ujumbe mzito zaidi. Kulisha watu ni kuwatakia heri ili maendeleo kimaisha yasikome, ni kama aliyefariki anawatakia heri wale waliobaki.
Huko Ulaya kuna jamaa yangu akiwa jirani na mzungu mmoja, apartment mlango huu unafuatana na mlango wake.
Kuna siku akapita jioni akitoka mishe zake akaona mlango wa jirani mzungu uko wazi na macho hayana pazia, kwenye kiti akamwona mke wa jirani yake kawasha mshumaa anaitazama picha ya mumewe huku machozi yakimtiririka.
Taratibu jamaa akaingia na kumuuliza mke wa jirani yake kulikoni?
Yule mama akamjibu kuwa mumewe amefariki mchana ule na hajui afanye nini maana amechanganyikiwa.
Huyu jamaa yangu akashituka, na akasikitika sana.
Lakini haraka akawaita waTanzania marafiki waliokuwa karibu.
Wakanunua vyakula na vinywaji na wakampa kampani yule mama hadi mazishi yalipofanyika.
Wazungu walioshiriki walikuwa wachache sana lakini waafrika walikuwa wengi.
Yule mama mfiwa kwa kweli alichangamka. Na baadaye alikiri kuwa waafrika wana moyo wa pekee duniani maana alikiri vile vile kuwa siku ile aliyomkuta akilia peke yake alikuwa akihisi kuchanganyikiwa na kutaka kujiua!
Alishukuru sana kwa kusaidia kubeba mzigo wa stress na kusema kuwepo kwao kulikuwa faraja kubwa.
Huu ni mfano ambao unaoonyesha jinsi sisi waafrika tumejaaliwa na Muumba namnaya kukabili misiba inayoleta matatizo makubwa kifikra kwa wafiwa.
Mkuu penginr haukuelewa lengo la uzi wangu.mkuu msibani si kuna michango alafu mfiwa huusiki kupika kwa uzoefu wangu wamama ndio huwa busy kuchakata mambo ya chakula kupitia michango labda kama wewe huwa hushiriki misiba ya wenzako so wanakususia alafu kuna utaratibu familia hujiwekea kama sisi mchango minimum ni elfu 50 labda uwe na kipato cha chini sana na tunajua kweli huna
Ndio maana watu wanatoa rambi rambi, maana yake kusaidia matumizi ya hapa na pale ikiwemo chakula kwa wale wataokuja kuzikaTamaduni mbovu kabisa isiyopaswa kuigwa na vizazi vijavyo.
Wanaopaswa kuchangia chakula ni wanaokuja kzuika na sio wafiwa.
Kwa nini iwe lazima wale,kabla ya msiba walikula wapi ?Mkuu tatizo la watu wengi hawajui misiba haiitaji pesa inahitaji watu na watu lazima wale chakula
Wanamfariji wanamtia stress tuHalafu kuna mijitu inashinda msibani kuanzia asubuhi hadi usiku yupo tu na anakula chakula bila kuchangia hata senti eti anamfariji mfiwa, wengine wanalalamika msibani unakuta nyumba imejaa watu wanalala sebuleni, vyumbani hadi nje.
Ni utaratibu wa kipuuzi sana, wanatakiwa wabaki watu wachache wa karibu wasiozidi kumi.
Wataamua wafiwa wafanye vipi,sio umeacha milioni za ubwabwa alafu huku unadaiwa milioni mbili,hakuna ubwabwa hakuna niniVipi kama marehemu aliwekeza hela za ubwabwa kwaajili ya mazishi yake?
Kaka mokaze nimefurahi kukuona hapa,nimemiss sana mahojiano yako na mzee zurri mnavyosokotana aisee.Haswa swahibu, ni ukweli mtupu usiokuwa na shaka.100% ✔✔
Utamuona mtu eti anaenda msibani kwa ajili ya kula tu, yeye siku zote ni kuangalia wapi kuna msiba ili ale. Na asiposhiba utamuona akihangaika kupata shani nyingine, akishiba utasikia akisema; "huu ubwabwa mtamu", kasahau kabisa kwamba pale ni msibani na ni jukumu la watu kuwachangia wafiwa rambirambi kama faraja kwao.
Jambo linalotakiwa ni kwa wafiwa kuweka ngumu kupikia watu wa karibu chakula ili somo lizoeleke miongoni mwa jamii zetu, na hakika hili ni fundisho la uisilamu.
Hongera swahibu kwa kutukumbusha jambo hili.✔✔
Wataamua wafiwa wafanye vipi,sio umeacha milioni za ubwabwa alafu huku unadaiwa milioni mbili,hakuna ubwabwa hakuna nini
Kaka mokaze nimefurahi kukuona hapa,nimemiss sana mahojiano yako na mzee zurri mnavyosokotana aisee.
By the way kweli bora kuweka ngumu somo lizoeleke katika jamii
Naweza kuja kutoa rambi rambi na siku ya kuzika au muda wa kuzika nisiwepo, na mwingine anaweza kutoa rambi rambi na siku ya kuzika au muda wa kuzika akahudhuriaAnaetoa rambirambi ni nani na anaekuja kuzika ni nani ?