Mkuu chakula msibani ni mila ya kiafrika na ipo karne nyingi.
Kimsingi wafiwa wao hawapiki wao wenyewe kwa ajili ya msiba bali jamii inayo mzunguka mfiwa.
Nia ya mila hii ni kuwapunguzia wafiwa ukiwa na kuufanya msiba uwe wa jamii nzima.
Ukiitazama juujuu utafikiri msiba na kulisha waombolezaji ni jukumu la mfiwa, la hasha.
Tatizo linakuja pale mfiwa akiwa hana uhusiano mzuri na jamii inayomzunguka au hahudhurii misiba ya jamii yake.
Hapo mfiwa anaipata fresh.
Mila ya kuwapa waombolezaji chakula kabla ya mazishi ina ujumbe mzito zaidi. Kulisha watu ni kuwatakia heri ili maendeleo kimaisha yasikome, ni kama aliyefariki anawatakia heri wale waliobaki.
Huko Ulaya kuna jamaa yangu akiwa jirani na mzungu mmoja, apartment mlango huu unafuatana na mlango wake.
Kuna siku akapita jioni akitoka mishe zake akaona mlango wa jirani mzungu uko wazi na macho hayana pazia, kwenye kiti akamwona mke wa jirani yake kawasha mshumaa anaitazama picha ya mumewe huku machozi yakimtiririka.
Taratibu jamaa akaingia na kumuuliza mke wa jirani yake kulikoni?
Yule mama akamjibu kuwa mumewe amefariki mchana ule na hajui afanye nini maana amechanganyikiwa.
Huyu jamaa yangu akashituka, na akasikitika sana.
Lakini haraka akawaita waTanzania marafiki waliokuwa karibu.
Wakanunua vyakula na vinywaji na wakampa kampani yule mama hadi mazishi yalipofanyika.
Wazungu walioshiriki walikuwa wachache sana lakini waafrika walikuwa wengi.
Yule mama mfiwa kwa kweli alichangamka. Na baadaye alikiri kuwa waafrika wana moyo wa pekee duniani maana alikiri vile vile kuwa siku ile aliyomkuta akilia peke yake alikuwa akihisi kuchanganyikiwa na kutaka kujiua!
Alishukuru sana kwa kusaidia kubeba mzigo wa stress na kusema kuwepo kwao kulikuwa faraja kubwa.
Huu ni mfano ambao unaoonyesha jinsi sisi waafrika tumejaaliwa na Muumba namnaya kukabili misiba inayoleta matatizo makubwa kifikra kwa wafiwa.