Suala la Wanaharakati na Manasheria wa Kenya, Je, Tumekosa Wenye Hekima?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Sote tunajua hali ambayo nchi yetu inapitia:
1. Udhulumaji mkubwa wa haki za binadamu kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

2. Uonevu wa ajabu kwa wananchi, kama vile tulivyoshuhudia watu wakipigwa na kuvunjwa mikono na miguu, tena na watu waliotakiwa kuwalinda.

Bahati mbaya sana, mambo haya yanafanywa na watawala na Serikali yao. Nasema ni Serikali yao, siyo Serikali ya wananchi. Ingekuwa ni serikali ya wananchi, ingejishughulisha zaidi na kuwalinda wananchi kuliko kuwadhulumu haki zao.

Cha kusikitisha zaidi ni kuwa Serikali yao imeanza kupeleka huu udhulumaji wa haki za wananchi mpaka kwa watu wa mataifa jirani. Wakati serikali za mataifa mengine zinahamgaika kutafuta fursa za export bidhaa zao kwa mataifa mengine, Serikali yao inafanya export ya udhulumaji wa haki! Inasikitisha sana.

Tukiwa wakweli wa nafsi zetu, wale raia wa Kenya waliokuja Tanzania kusikiliza kesi ya Tundu Lusu, hawakufanya kosa lolote na hawakuvunja sheria yoyote ya nchi yetu. Kuja kusikiliza na kufuatilia kesi ya Lisu lilikuwa ni jambo la kiutu:
Lisu ni mwanachama wa chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki. Mwanachama mwenzao amebambikiwa kesi ya uhaini, hawa wanachama wenzake wa chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki kuja kusikiliza kesi yake, kuna ubaya gani?

Tulivyo na viongozi wa ajabu, waliojaa uwongo, Ndumbaro anawaambia watu kuwa eti walikamatwa kwa sababu walikuja kufanya uwakili bila kibali! Fikiria huyu ni kiongozi, halafu anakuwa mwongo wa kiwango hicho. Hawa hawakuja kama mawakili wa kesi ya Lisu, bali walikuja kusikiliza na kufuatilia kesi ya mwanachama mwenzao wa chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki.

Nafahamu kuna watanzania wameoa na kuolewa Kenya na hata Uganda. Kwa aina ya watawala tulio nao kwa sasa, yawezekana kabisa hata kukitokea msiba, ndugu zako waliopo Kenya au Uganda wakija kwenye msiba, wanaweza kuishia kutekwa, kufichwa, kupigwa na kwenda kutupwa porini ili warudi nchini kwao.

Nchi imefika hatua mbaya ya kutisha!! Wenye hekima wainuke na kusema neno, wananchi tuamke kukemea uharamia huu, na viongozi wa dini wasikose kuendesha maombi maalum, ili MUNGU MKUU atuinulie viongozi wenye hekima katika nchi yetu, ili Taifa liokoke na liondoke kwenye mkwamo huu wa kuogofya
 
Mimi naweza sema maarifa ni Kila kitu hili swala sio swala la ujirani, undugu au rafiki hapa linagusa swala Zima la kiusalama Tena wa Taifa na ukitaka kujuwa vizuri ni nini ninamanisha hiki ninachoandika soma/Fanya tafiti sana ktk maswala ya kijasusi na yanafanyaje kazi hasa ktk swala Zima la kiusalama. Na pia watu wengi Huwa wanaumia kwa kufata mkumbo kwa maswala wasio yajuwa uwalisia ua undani wake halisi, tusifanye mambo kwa mihemko hv jiulize Tanzania ingekuwa kama Sudan au congo Yani ni nnchi yenye machafuko wangekuja kuleta hicho wanachosena ni uharakati kwani mpaka hapa tulipo fika Tanzania Kuna mtu yyote alitoka nnje kuja kutuambia nni chakufanya kwahiyo kwa ufupi tu tunajitambua wapi tulipo na wapi tunapotaka kwenda kwa misingi ya maadili yetu ya kitanzania mshikamano na amani
 
Back
Top Bottom