Suala la watu 87 kati ya 100 Tanzania kuwa tegemezi linavunja moyo sana wakuu

Suala la watu 87 kati ya 100 Tanzania kuwa tegemezi linavunja moyo sana wakuu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Hii taarifa tangu nilipoiona, kama inaukweli basi nchi yetu ni masikini wa kutupwa.

Inaonuesha uhalali wa kupigwa mizinga popote utakapopita.

Inaonyesha vuguvugu la uchawa ni harakati za watu waliolemewa na utegemezi wa kifikra uliokithiri.

Hali hii wenda ndio imepelekea ongezeko la ukahaba, wacheza kamari, mashoga, machawa na kunguni, ombaomba, vibaka.

Kama kauli hii ya kusema karibu asilimia 87 ya watanzania wote ni tegemezi itaeleweka kwa kina kwa kila mtu itawavunja moyo wengi na kubaki wanatarajia msaada na kuombaomba.

Hii inasikitisha kwa sababu inaonesha tangu uhuru sisi tunazidi kudidimia. Tunazidiwa kabisa na Watanzania wa miaka ya zama za mawe ambao walijitegemea kiakili na kimwili wakati wakiwa sio welevu kama sisi.

Inaonyesha ongezeko la vyuo halijasaidia, mashule hayajasaidia,

Unadhani nini kifanyike?

Mimi napendekeza itangazwe siku moja ya mapumziko na taifa zima watu wabaki majumbani watafakari wanakwama wapi.

Na wanaoongoza nchi waje na blue print mpya ya kututoa hapa. Hii taarifa binafsi imenifanya nipne aibu sana.

Ni hayo tu.
Screenshot_20241104-185815_Chrome.jpg

KAMATI ya Bunge ya Bajeti imeshauri serikali kuhakikisha ongezeko la watu linaendana na ukuaji wa uchumi kwa kuwa kwasasa kati ya watu 87 kati ya 100 ni tegemezi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Oran Njeza ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akisoma maoni ya kamati kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26 pamoja na mapendekeo ya mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya serikali kwa Mwaka 2025/26.

Amesema kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022, idadi ya watu ilikuwa ni 61,741,120 Mwaka 2022 na inakadiriwa kuwa 87,509,630 ifikapo Mwaka 2035 kutokana na ongezeko la watu la asilimia 3.2 kila mwaka.

Njeza amesema ongezeko hilo la idadi ya watu nchini haliendani na ukuaji wa uchumi.

Pia soma: Bunge: Hali ya Utegemezi Nchini inatisha. Katika Watu 100, watu 87 ni Tegemezi
 
Hii taarifa tangu nilipoiona, kama inaukweli basi nchi yetu ni masikini wa kutupwa.

Inaonuesha uhalali wa kupigwa mizinga popote utakapopita.

Inaonyesha vuguvugu la uchawa ni harakati za watu waliolemewa na utegemezi wa kifikra uliokithiri.

Hali hii wenda ndio imepelekea ongezeko la ukahaba, wacheza kamari, mashoga, machawa na kunguni, ombaomba, vibaka.

Kama kauli hii ya kusema karibu asilimia 87 ya watanzania wote ni tegemezi itaeleweka kwa kina kwa kila mtu itawavunja moyo wengi na kubaki wanatarajia msaada na kuombaomba.

Hii inasikitisha kwa sababu inaonesha tangu uhuru sisi tunazidi kudidimia. Tunazidiwa kabisa na Watanzania wa miaka ya zama za mawe ambao walijitegemea kiakili na kimwili wakati wakiwa sio welevu kama sisi.

Inaonyesha ongezeko la vyuo halijasaidia, mashule hayajasaidia,

Unadhani nini kifanyike?

Mimi napendekeza itangazwe siku moja ya mapumziko na taifa zima watu wabaki majumbani watafakari wanakwama wapi. Na wanaoongoza nchi waje na blue print mpya ya kututoa hapa. Hii taarifa binafsi imenifanya nipne aibu sana.

Ni hayo tu.
View attachment 3143478
Fikiria wanawake wote wenye elimuz wenye kazi na wasio na elimu wala kazi wote ni wategemezi plus watoto na walemavu.

Ndio maana hata wizara maalum huwa inaunganisha haya makundi pamoja.
 
31m ya watanzania(53%) ni watoto wa umri 0-19.

Bado kuna marika ya chuo, nayo ni tegemezi.

Hili nadhani ni tatizo la bara zima, Africa ndo bara linalokua kwa kasi zaidi.

Suluisho ni tupunguze kuzaa ovyo.
Kuzaa sio tatizo , tatizo kubwa ni kubadili mfumo wa maisha na elimu kwa watoto haiwezekani mtu anafika miaka 27, mtu mzima huyu bado anasomeshwa eti degree na hata wenye hizo degree mindset zao hazipo huru, tatizo linaanzia hapo
 
Inawezekana, nchi yetu ni kwa vile sembe, mihogo, mchicha na dagaa ni bei rahisi, lakini kiwango cha umaskini bado ni kikubwa sana
 
Inawezekana, nchi yetu ni kwa vile sembe, mihogo, mchicha na dagaa ni bei rahisi, lakini kiwango cha umaskini bado ni kikubwa sana
Tuko nyuma sana aisee. Kazi ni kubwa.
 
Back
Top Bottom