Viongozi siyo wa kuwaamini hata siku moja, Unaweza ukafikri kuwa Majaliwa ndiye mrithi sahihi wa kuendeleza yale ya Magufuli kumbe na yeye anayake moyoni mwake.
Siku akipewa urithi wa nafasi ya urais ndo anafungua makucha yake kwa kutoa kile cha rohoni mwake mpaka watu wanamshangaa kuwa ni Majaliwa yule waliyekuwa wanamfahamu au ni Majaliwa wa kuchongwa?.
Ndipo yanapoweza kujitokeza kama yale ya Zambia ya Chiluba kumwandaa mrithi wake akitegemea kuwa ndiye atakayekuja kumlinda na kuendeleza mambo yake kumbe ndiye aliyekuja kumkamata na kumtia Lupango.
Mwingine ambaye wapinzani wanajuta kumfahamu ni yule aliyesema nichagueni nitakuwa rais wa watu wote na sita wa bagua kwa vyama, baada ya kupita kilichofuata baadae sitaki fyoko, Wapinzani wakikoa lupango, Wakitaka kugombea nafasi yoyote ya kiserekali lupango, Wananchi wakimchagua kiongozi wanayemtaka wanalazimishwa kuongozwa na kiongozi wa rangi ya kijani ambaye hawakumchagua.