Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Nineweka full tank lita 65 ajabu nimetembea km 350 mafuta kwishney leo nimejaza tena

We unanunua perfomance car kwa ajili ya kwendea kazini halafu unamlaumu "SUBARU" atakufilisi? Subaru ni mashine za kweli kwa waendao mbio, zina nguvu ya kutosha hata kwa base grade bila upgrade zozote, kama wewe uliona vijana wa arusha na wenye asili ya kihindi na kiarabu wakiendesha Subaru ukapenda Mlio jaribu ujipange upya, uza Subaru ununue IST. Btw, ni Subaru gani hiyo? Wateja wako wengi tu, ukitaka kuiuza faster ingia Subaru Fans of Tanzaia.
 
Pole sana mkuu. Badili usafiri karibu kwetu Vitz haaaa sina shida mie. Kila kona utanikuta napiga misele tu......Safari ndefu nakipaki nakula basi kwa raha zangu na kipato changu. Kama na wewe kipato kipo chini usijilazimishe njo kwa VITZ hutojuta.
 
kaka kuna gari za watumiaji wa kipato kidogo na kipato kikubwa,ni kama kama huna biashara za safari ndefu za mara kwa mara unanunua prado v8 huku maisha yenyewe ni ya kuungaunga,utailaumu gari kumbe kosa ni lako kutokufanya uchunguzi mapema.Gari yako hiyo hiyo ipige long safari uone kama hujaifurahia kama wewe ni dereva lkn.
.
Aaah kumbe kwenye long safari haili mafuta sana eeh!?
 
kaka kuna gari za watumiaji wa kipato kidogo na kipato kikubwa,ni kama kama huna biashara za safari ndefu za mara kwa mara unanunua prado v8 huku maisha yenyewe ni ya kuungaunga,utailaumu gari kumbe kosa ni lako kutokufanya uchunguzi mapema.Gari yako hiyo hiyo ipige long safari uone kama hujaifurahia kama wewe ni dereva lkn.
.

Mkuu watu wananua magari bila kujua matumizi yake.
Nimetumia Subaru matoleo mawili sasa, ya '98 na ya 2002.
Hizi gari hazikukopeshi, ni brilliant perfomers. Engine zake ni sports, hazikutengenezwa kubania mafuta bali ku-out perform.

Nilijaribu hilo katika mbuga za Makambako-Iringa.
Cruiser moja ilinipita kwa fujo, nami nikaamua kukanyaga mafuta.
Spidi zikifika zaidi ya 140km/hr. valves zinazibuka na kamnyama haka ka Subaru kana paa kirahisi sana hadi 180km/hr na mashine wala haipandishi temperature wakati wa high revs.
Kwa kifupi ile Cruiser nami tukawa ngoma droo hadi Iringa, na dereva mwenzangu wa Cruiser ilibidi akubali.

Hala hala lakini, kamchezo hako ni kwa wazoefu tu na pochi ikiruhusu.
 
Kwa foleni za Dar mbona lita 65 kwa km 350 kawaida sana .... yaani 5.4km/litre !!! Ahaaaaaa, wenzio wa Morogoro Rd, from Ubungo - Posta tena ndani ya kitu cha Daihatsu terios Kid (650cc) sometimes mpaka 5 km/litre?! Karibu Dar ujionee maajabu ya foleni ....
 
kaka kuna gari za watumiaji wa kipato kidogo na kipato kikubwa,ni kama kama huna biashara za safari ndefu za mara kwa mara unanunua prado v8 huku maisha yenyewe ni ya kuungaunga,utailaumu gari kumbe kosa ni lako kutokufanya uchunguzi mapema.Gari yako hiyo hiyo ipige long safari uone kama hujaifurahia kama wewe ni dereva lkn.
.[/QUOTE
Ushauri nzuri, japo maisha ni kujipanga na kuchagua lazima pia uzingatie future yako. uza hiyo gari nunua size yako mkuu.
 
Ukiwa limbukeni siku zote mwisho wake ni kujilaumu. nunua gari size yako mkuu!
 
Hapo ni kwenye wese,just wait spare zianze kuchoka
Mkuu hii gari ime evolve kutokana na gari za sports za Subaru. Ni gari ngumu mno kuharibika ingawaje kweli vipuri vyake ni ghali sana.
Waswahili wasema kipendacho roho hula nyama mbichi.
 
Nineweka full tank lita 65 ajabu nimetembea km 350 mafuta kwishney leo nimejaza tena
Hiyo gari ulinunuliwa na sugar mami nini? Kama ulinunua kwa akili yako timamu basi na wewe ikomalie tu kwa kuinyima mafuta.
 
We unanunua perfomance car kwa ajili ya kwendea kazini halafu unamlaumu "SUBARU" atakufilisi? Subaru ni mashine za kweli kwa waendao mbio, zina nguvu ya kutosha hata kwa base grade bila upgrade zozote, kama wewe uliona vijana wa arusha na wenye asili ya kihindi na kiarabu wakiendesha Subaru ukapenda Mlio jaribu ujipange upya, uza Subaru ununue IST. Btw, ni Subaru gani hiyo? Wateja wako wengi tu, ukitaka kuiuza faster ingia Subaru Fans of Tanzaia.
Shemeji yenu kaninunia kisa anataka Hii Subaru.
Anadai kaipenda sana, na vile ni 4WD basi simuelezi kitu. Anadai mafuta atajua mbele kwa mbele jinsi ya kuyapata, lakini kwanza Subaru kwanza ije nchini ndio amani irudi.

Uwezo wa kununua upo, maana hesabu za haraka haraka 10Mil ni tosha kabisa kwa hii gari, Ushauri wenu please unahitajika maana huo mnuno nliopewa na hii baridi ni balaa!!
 
Back
Top Bottom