Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Yaani hapo ulitakiwa utembee 650km..lkn jaribu kurekebisha nozzles au kusafisha labda zina matatizo..na pia km unatumia a/c safisha radiators kwa maji ya pressure
 
Kwa upande wangu nakushauri ukitaka kununua kitu Jaribu kufanya Utafiti kwanza ,Mbona sikuhizi kunasorce nyingi sana za information..pole sana kaka..
 
Mnashangaa nini, watu asilimia kubwa wanaendesha magari mabovu na ndiyo kundi kubwa la wasio na kipato cha kutisha.unategemea gari ina miaka 20 unaweza pata hata 7km per litre? never. hivyo hutakiwi kushangaa kaza buti au nunua pikipiki. masikini ndiye consumer mzuri wa mafuta kwa taarifa yako
 
Nineweka full tank lita 65 ajabu nimetembea km 350 mafuta kwishney leo nimejaza tena

Yes the car is delusion, kwani hujajiuliza kwa nini mjapan anauza bei hiyo wakati suzuki Jimny iko juu. Pia kumbuka inawezekana ulikwenda mwendo wa 160KM/HR maana ukienda speed hiyo lazima utalia eti.
 
kwa magari yanayokunywa mafuta 65L ni half tank!gari yangu inabeba 80L full tank na siiweki kwenye fuel guzzlers category....angalia uendeshaji wako...kama wewe ni racer lazima uumie....drive between 120-130km/hr uone kama itakunywa mafuta....inashangaza ulinunua Subaru bila kujua ni gari ya aina gani....
 
U dereva sio kunyoosha barabara...kuna hadi ku accelerate, angalia RPM n control ...Subaru yenye turbo zina perfomance so its obvious ratio ya mafuta inakuwa in between 6-8km/lt..cha zaidi fanya service yaweza kuwa airmass imekufa .
 
Ndio maana mimi nimejinunulia Toyota MarkII 4CILENDER MANUAL lita tano za mafuta natembelea wiki!
 
subaru ina umadhubuti na muundo wa kipekee nilinunua moja second hand na ilikuwa na km 80,000. niliitumia kwa miaka 12 haikuwa na tatizo lolote mpaka nilipopata ajali nikashindwa kuitengeneza kwa gharama kubwa kulinganisha na umri wa gari
subaru inategemea na uendeshaji wako na ukubwa wa machine yake, ni gari nzuri bado nina matumaini ya kununua nyengine ikiwa kwenye hali nzuri, unywaji wa mafuta sio tatizo ila ni muundo wake
Huwezi nunua suti nzuri ukavaa na kanda mbili
 
Vijana wengi wa Arusha wamenunua Subaru wakifurahia ule mlio wake lakini wamesahau ufahali nyumba ya umaskini hasa kama hela yenyewe ya kujichanga changa!

Subaru haifai kwa kiwese.

Wana ka-umoja chao wanajiita subaru kaskazini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wee umeacha Corolla iliyo ndani ya uwezo wako ukakimbilia Subaru usiyokuwa na uwezo wa kui-maintain. Uza ukanunue Corolla waachie wenye uwezo waendeshe Subaru. Acha kulalamika bila sababu za msingi.
 
Wapi naweza pata mtu wa kuifanyia diagnisis hii gari maana ulaji huu ni sawa na 1ltr kwa 5km ni sawa kweli?msaada pse
 
Wapi naweza pata mtu wa kuifanyia diagnosis hii gari kwa computer maana ulaji huu ni sawa na 1ltr kwa 5km ni sawa kweli?msaada pse
 
Mkuu watu wananua magari bila kujua matumizi yake.
Nimetumia Subaru matoleo mawili sasa, ya '98 na ya 2002.
Hizi gari hazikukopeshi, ni brilliant perfomers. Engine zake ni sports, hazikutengenezwa kubania mafuta bali ku-out perform.

Nilijaribu hilo katika mbuga za Makambako-Iringa.
Cruiser moja ilinipita kwa fujo, nami nikaamua kukanyaga mafuta.
Spidi zikifika zaidi ya 140km/hr. valves zinazibuka na kamnyama haka ka Subaru kana paa kirahisi sana hadi 180km/hr na mashine wala haipandishi temperature wakati wa high revs.
Kwa kifupi ile Cruiser nami tukawa ngoma droo hadi Iringa, na dereva mwenzangu wa Cruiser ilibidi akubali.

Hala hala lakini, kamchezo hako ni kwa wazoefu tu na pochi ikiruhusu.

Mkuu ni kweli kuna siku jamaa mmoja alinitesa sana Mbwewe mpaka Manga njia ya Tanga wakati mimi nilikuwa na gari yenye engine ya 1G,nilimuiliza jamaa yangu performance za Subaru akaniambia achana nazo kwa gari hizi za kawaida,ilibidi nitafute nikapata Legacy touring lakini mbona kwenye mafuta sio kama anavyolalamika huyu bwana au kuna kasoro kwa sababu haina tofauti kubwa sana na gari ya cc 2000.
 
Back
Top Bottom