imetokana na ugomvi binafsi wa Watu wawili tu kwa Udikteta wao wa kutaka madaraka.
Ilianza udini, nchi kubwa ya Sudan ikagawanyika vipande, na kuzaa nchi mbili moja kongwe kipande Sudan na mpya ya South Sudan .
Laana ya ubaguzi wowote wa kikabila kidini, kimapato, kundi la walio nacho na wasionacho, nasaba n.k haiishii hapo, sasa kuna mmoja anajiona mwarabu zaidi kuliko mwenzie mlugaluga mwarabu hivyo wanazichapa tena.
Wakimalizana lazima tukio jingine litajijenga (manifestation), wataaendelea kuzua mgogoro wa aina nyingine.
Bara la Afrika wanaonea huruma na kufuatilia mambo ya Ukraine, Jerusalem, Madina, Roma, Gaza, Marekani na Ulaya.
Mambo ya bara hili la Afrika ya DR Congo, Burundi, Sudan, Mali, Mauritania hatuyafuatilii kwa ukubwa ule ule kwa kuwa hatuoneani huruma wale wanaofanana nasi kwa rangi umasikini, maradhi na ujinga.