Sudan Kusini itabadili muda kwa saa 1 kwa kuhama ‘time zone’

Sudan Kusini itabadili muda kwa saa 1 kwa kuhama ‘time zone’

Umejifunza Africa mashariki jifunze Tanzania sasa[emoji16]
Kwa hiyo unadhani Tanzania iliyopo Afrika Mashariki ina Longitude yake inayojitegemea?

Usisahau kuwa Afrika Mashariki inatumia Longitude 45° katika kuhesabu masaa
 
Hata dar na Bukoba unatofautiana, ukiwa Bukoba saa 12 bado giza kabisa ila Dar tayari kumekucha, Halafu saa kumi na mbili jioni bado kuna mwanga wakati dar giza lishaanza nyemelea
Dah!...
 
Ina maana Rwanda Burundi ziko tofauti na Tanzania?
Hakika, hata Kagera na Kigoma zilitakiwa kuwa muda sawa na Rwanda na Burundi.

Kiuhalisia Tanzania ilitakuwa kuwa na kanda tatu mstari nyoofu tokea Kaskazini hadi Kusini Mashariki, Kati na Magharibi.

Dar es Salaam (Mashariki) 12:00 Singida (Kati) 11:45 Bukoba (Magharibi) 11:30.

cc. Nafaka
 
Sijutii kuzaliwa Africa aisee yasiyowezekana wote tunaweza na ugumu huu mwakani tunaingia uchumi wa juu Kati kaskazini
 
Hata dar na Bukoba unatofautiana, ukiwa Bukoba saa 12 bado giza kabisa ila Dar tayari kumekucha, Halafu saa kumi na mbili jioni bado kuna mwanga wakati dar giza lishaanza nyemelea
Sio kila siku hali hiyo.Inatetegemeana na mzunguko wa dunia kulizunguka jua ambapo Jua miezi kadhaa linakuwa upande wa kaskazini mwa Latitude na miezi kadhaa kusinimwe.Kwa maana hiyo zipo siku Bukoba na Dar wanaweza kukaribiana sana kihali za mwangaza wakati wa magharibi na asubuhi.
 
Kumbe hii time zone ni kujiamulia tu.sio kulingana na mahali nchi imekaa kwenye latitude
Mkuu hayo mambo mbona ni mitambo tu.

Kuna vitu naturally huwezi kuvibadili,watabadili haya waliyoyabuni wao.

Matukio ndio msingi wa kila kitu.

Mfano sasa hivi canada wao ni saa 2 asubuhi kuna mtu anapiga mswaki wakati tz ni saa 10.

Hivyo tukio la mkanada kupiga mswaki linatokea sasa hivi saa kumi kwa Nchi yangu na kwa nchi yake ni saa 2 lakini mimi nitasema kuwa sasa hivi mkanada anapiga mswaki huko kwao sasa hivi yaani ambayo kwangu itakuwa saa 10 sasa hivi na kwake itakuwa saa 2 sasa hivi.

Kwa hyo mkuu ishu ni matukio na sio haya mambo mengine sijui ya kuseti time na mambo kibao.
 
Miaka fulani hapo nyuma niligundua hii kitu italy iliamua kurudi nyuma kimuda na yenyewe.
 
Badala wabadili mentality waache ngumi za kila siku wanabadili time zone!
 
Basi muda wa Dar na Kigoma utofautiane kama muda wa jua kuchomoza au kuzama unavyotofautiana.

Nilichojifunza kuanzia Shule ya msingi(Maarifa ya Jamii) hadi Sekondari(Geography), saa zinatofautiana kwa kila 15°.

Kila sehemu iliyopo degree fulani, mathalani sisi(45°) muda wake utakuwa sawa, ndio maana jua linawahi kuchomoza Dar na kuchelewa Kigoma lakini muda ubaki ule ule Dar na kigoma(kama ni saa moja Dar, na kigoma ni hivyo hivyo hata kama bado giza Kigoma).

Ndivyo hivyo nilijifunza muda unapangwa kulingana na Longitude ya sehemu husika, ambapo Afrika Mashariki ipo Longitude 45° Mashariki mwa Longitude kuu(Greenwich, 0° iliyopo Ghana).

Sasa unapohoji nchi kuwa kwenye degree 45°, ebu nifafanulie wewe unahisi ipo kwenye degree ipi na ipi maana mimi nilijifunza ipo degree 45° ambapo ndio tunapohesabia masaa yetu(Kijografia, ingawa kisiasa nimeisikia leo)
We jamaa Greenwich ipo GHANA tangu lini?
 
Back
Top Bottom