Sudan Kusini itabadili muda kwa saa 1 kwa kuhama ‘time zone’

Sudan Kusini itabadili muda kwa saa 1 kwa kuhama ‘time zone’

Ipo wapi mkuu? huenda niliingizwa chaka na walimu wangu
GMT au Prime Meridian Time inaanzia Greenwich, UK inakatiza Algeria, Burkina Faso, Mali, Ghana na St. Helena.

Roughly kuna mida (Time Zones) 25 ikitengwa kwa wastani wa saa 1, Kila baada ya kipeuo cha nyuzi 15 za longitudo unatokea muda mwingine (Time Zone).

China au Tanzania zilikuwa zinaweza kutenga muda kwa wastani wa 15, 30 au 45 dakika lakini zinatumia muda mmoja wa kitaifa. Mataifa kama Australia, Iran na India yametenga muda kwa kipeuo cha dakika 30 kikanda.

Nyakati za kiangazi (Summer Time) baadhi ya mataifa ubadili saa kwa kusogeza mbele, mfano;- Uingereza usogeza saa moja mbele alkadhalika Uswissi. Hii hufahamika vyema kama 'Daylight Saving Time'.

Katika mfumo wa kalenda na muda Prime Meridian Line ndio kipimo cha saa na siku, mstari huu unapita eneo la bahari ya Pasifiki. Ukiwa upande wa Magharibi utakuwa masaa 24 mbele ya wa Mashariki.

Ukisafiri kutoka Mashariki kwenda Magharibi unapoteza siku na kutoka Magharibi kwenda Mashariki unaongeza siku.
 
We jamaa Greenwich ipo GHANA tangu lini?
Njoo uone jibu hapa

1612114723468.png

kwa wale waliopitia Elimu ya Msingi na hata sekondari ya kawaida wataelewa vema na kwanini Sudan Kusini anataka kuhama
Hii Time Zone ipo current /live ukipoint Dsm itakuonesha ni usiku saa 2 Jumapili wakati ukigusa China itakuambia tayari (1:17) saa 7 usiku Jumatatu
 
Wanajipunguzia masaa ya kuteseka lakin mateso yapo palepale
 
Maswali ya Jiografia kutafuta muda sasa hayana maana kule shule za msingi.

Hata hivyo, ukiwa baadhi ya maeneo ya Karagwe mkoa wa Kagera unatumia muda wa Rwanda kwa maana ya Africa Magharibi.
Miaka ya nyuma kidogo(sijui sasa) baadhi ya mitandao walikuwa wanakutumia ujumbe kukutakia maisha mema (..… Tanzania wishes you a pleasant stay in Rwanda).
African Magharibi!? au Africa ya kati?
 
Sudan Kusini imepanga kubadili muda kuanzia Februari 1 ambapo itakuwa saa moja nyuma ya saa za Afrika Mashariki

Wanarudi kwenye ukanda wa muda wa UTC +2 ambapo kwa sasa wapo UTC +3. Katibu wa Kazi Hillary Wani Pitia amesema kijiografia UTC +2 ndio sahihi kwa Sudan Kusini.

Nchi inaweza kuseti muda wake kutokana na sababu za kisiasa ili kufanana na majirani zake. Sudan Kusini watafanana muda na DR Congo, Rwanda, Burundi, Afrika Kusini na Misri.

Mabadiliko ya Muda yamepitishwa na Baraza la Mawaziri wiki mbili zilizopita, japo raia walikosoa hatua hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
===
South Sudan plans to reset its clock, moving back one hour on February 1.

The change, which moves the country an hour behind its key trading partners Uganda and Kenya, is meant to align it to the time zone based on its geographical location.

“The National Ministry of Labour informs all the civil service institutions, commissions, diplomatic missions, UN agencies, international/non-governmental organisations and the public at large that South Sudan has changed its official time from UTC +3 to UTC +2, which is based on South Sudan’s real location on the globe,” the Labour undersecretary Mary Hillary Wani Pitia said in statement on Friday.

The Coordinated Universal Time (UTC) is a time standard by which the world regulates clocks and time. It is often interchanged with Greenwich Mean Time (GMT), but while there is no time difference between UTC and GMT, the latter is a time zone used in some European and African countries.

The dateline – an imaginary longitude 180o that runs from pole to pole – zig zags east and west to accommodate the needs and demands of countries along its route. Most countries use hourly offsets from GMT.

Countries can, however, set their own time for political reasons or to keep the same time zone with border countries.

The switch by South Sudan will see it move from the East African time zone (GMT +3) – observed by Uganda, Kenya, Ethiopia, Tanzania, Somalia, Eritrea, and Djibouti – to the Central African time zone (GMT +2).

Some of the countries in this time zone include Sudan, eastern Democratic Republic of Congo, Rwanda, Burundi, South Africa and Egypt.

“The current time will be set back by one hour, meaning 1:00 am will be reset to 00:00 am effective from 1st February 2021,” said Ms Pitia.

The change was approved by South Sudan’s Cabinet two weeks ago but came under heavy criticism by citizens on social media.

The government spokesperson, Michael Makuei Lueth, said the country has not been using its real time.
Kwan na ss hatuwez kubadili maan si suala la kuamua tuu
 
Kwan na ss hatuwez kubadili maan si suala la kuamua tuu
Massawe sisi hatuwezi kujipangia hizo Meridian Greenwich Time zilipangwa huko London wakajipa nyuzi 0 na ndizo zinagawa dunia katika masaa 24 kwa kugawa mzunguko wa Dunia kuwa ni duara hivyo nyuzi360 hivyo ukigawa hapo utapata 15 ndio lisaa moja (360 / 24 = 15) sasa huwezi hamisha box lako la nyuzi hapa Tanzania ukajipachike la Bangladesh hizo zitakuwa ni saa za kichawi na hutaoana na wote hata Internrt au simu.
Hao sudan Kusini ni eneo dogo sana lililo ktk masaa ya Afrika ya Kati kwani Juba Makao makuu yapo ndani ya mstari wa Afrika Mashariki
ngoja kina @Mwifwa watajafafanua zaidi kwanini ni makosa kujihamisha nyuzi na kujipachika unavyotaka labda zikaribiane
 
Kumbe hii time zone ni kujiamulia tu.sio kulingana na mahali nchi imekaa kwenye latitude
Mkuu kikiboxer kinachoamua time zone ya mahali ni Longitude na SIO Latitude ya mahali husika. Mfano Sehemu kubwa ya Tanzania IPO Longitude 45° East ingawa sehemu kama Kigoma ingaliweza kutambulika kuwa Longitude 30° East (SAA moja nyuma) kama ilivyo Burundi, Rwanda na South Sudan.

Ahsante
 
Inasaidia nini sasa?
ndyo inayotengeneza Dakika, Saa, siku, mwezi, mwaka
na usingeweza kupost Jamii forum kujua ni lini ulijiunga, ulituma hilo swali
inaweza kudetermine una umri wa miaka mingapi tangu tarehe ya kuzaliwa na lini ulikufa tukaweka kumbukumbu kwa watoto na vizazi
 
Haa kwetu Kigoma na Tanga kuwaweka saa moja +3 ni kuwaonea
 
ndyo inayotengeneza Dakika, Saa, siku, mwezi, mwaka
na usingeweza kupost Jamii forum kujua ni lini ulijiunga, ulituma hilo swali
inaweza kudetermine una umri wa miaka mingapi tangu tarehe ya kuzaliwa na lini ulikufa tukaweka kumbukumbu kwa watoto na vizazi
KWahiyo wale waliozaliwa muda mchache kabla ya haya mabadiriko wana rekodi vipi umri wao? Anyway, tukubaliane kwamba haina impact yeyote kiuchumi either wa taifa, mtu mmoja mmoja etc. Ni wana siasa tu wamekosa cha kujadiri au cha kukifanyia mabadiriko then wameona waingine kwenye hilo la saa
 
hii kitu si ya leo kabisa na hakuna aliye hai
bila mabadiliko haya ya kuigawa Dunia ( Google greenwich meridian - Пошук Google)
kusingekuwa na mawasiliano haya wala tarehe, kwa hiyo sio wanasiasa
Km ni Sudan Kusini basi kuna siasa hapo maana mstari wa Longtude umemega eneo dogo tuwaache walidai
1612276827693.png
 
Back
Top Bottom