Sudan yakabiliwa na mgogoro mkubwa wa mafuta wakati bei ikipanda

Sudan yakabiliwa na mgogoro mkubwa wa mafuta wakati bei ikipanda

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG31N2262166292.jpg

Mji mkuu wa Sudan, Khartoum, unakabiliwa na mgogoro mkubwa wa mafuta. Mamia ya magari yamepanga foleni katika vituo vichache vya mafuta vinavyofanya kazi, huku madereva wakisubiri chini ya jua kali, na wakati mwingine wakisubiri kutwa nzima kununua dizeli au petrol.



Ridhwan Ahmed Al-Nayer, dereva wa taksi, amesubiri kutwa nzima, na hana uhakika kama atapata mafuta. Jambo ambalo linachosha si kimwili pekee, bali pia kiakili, na karibu kazi yake ya udereva wa taksi itasimama.



Mgogoro huo wa mafuta umeenea katika miji mingine nchini Sudan, na kufanya bei ya mafuta kupanda ghafla. Galoni ya petrol katika masoko ya kando kwa sasa inagharimu karibu pauni 30,000 za Sudan, sawa na dola za Kimarekani 8.69, ikiwa ni ongezeko la pauni 18,000 kuliko wiki moja iliyopita.



Mgogoro huo unatokana na uharibifu uliotokana na vita kwa miundombinu ya mafuta nchini Sudan. Kiwanda cha kusafisha mafuta kilichoko Khartoum, ambacho zamani kiliweza kutimiza asilimia 70 ya mahitaji ya mafuta nchini humo, kwa sasa kimefungwa. Visima vingi vya mafuta navyo kwa sasa haviwezi kufanya kazi (au: haviwezi kutoa mafuta), na kuilazimisha Sudan kutegemea zaidi mafuta yanayoagizwa kutoka nje. Viwanda sita vya mafuta nchini humo kwa pamoja vina uwezo wa kutoa mapipa 144,000 kwa siku, lakini kwa sasa vinaweza kutoa asilimia 15 hadi 20 kutokana na uharibifu unaotokana na vita.



Abdul-Khaliq Mahjoub, mchumi wa nchini Sudan, anasema utegemezi wa uagizaji kutoka nje unafanya soko la ndani kuwa hatarini, na wakati vita ikiendelea na uzalishaji wa ndani ukipungua, nchi hiyo inakabiliwa na ukomo wa hifadhi na kupanda kwa bei ya uagizaji, mambo yanayoongeza mateso kwa raia.



Wizara ya Nishati na Mafuta ya Sudan inasema nchi hiyo ina karibu mapipa milioni 1.36 ya petrol, ambayo ni sawa na usambazaji wa siku 88 kwa matumizi ya sasa, na mapipa milioni 1.24 ya dizeli, yanayoweza kusambazwa kwa siku 54.



Usambazaji wa mafuta nchini Sudan pia unaathiriwa na vurugu za baharini. Mvutano wa kikanda unaohusisha Iran umeongeza hatari ya usafiri katika Bahari Nyekundu kupitia Mlango wa Bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani.



Mohamed Al-Tayeb, mchumi wa nchini Sudan, anasema mvutano wowote wa kijeshi katika Ghuba unaathiri papo kwa hapo bei ya mafuta duniani, na kwa Sudan, athari hizo zinaongezeka mara mbili. Anasema sera bora, ikiwemo kujenga hifadhi na kujiingiza kwa moja kwa moja kwa serikali katika uagizaji, kungeweza kupunguza bei kwa karibu asilimia 25.



Sudan imepoteza karibu asilimia 75 ya hifadhi yake ya mafuta wakati Sudan Kusini ilipojitenga nayo mwaka 2011. Mapigano yaliyoanza Aprili 2023 yamevuruga usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini, na hivyo kudhoofisha zaidi sekta hiyo.
 
Back
Top Bottom