Sugu amnunulia mpenzi wake gari la kifahari!!

Huko ni kujinyima au ku act??
By the way hapo kuna somo kutoka kwa mbunge kwenda kwako wew mwananchi.

Thamini mwanamke wako, jali na kumpenda. Usiwe na uchoyo wa kizamani wa wazee wetu kuwa dingi anavaa fresh then mkewe kachooka.

Au sugu atembeleee gari kali then kipenzi chake awe mtu wa boda boda au kid wake ashindwe kwenda shule.

Kuna maisha ya kiongozi na kuna personal life. Usi changanye vitu hivi viwili.

Big up Sugu as long as unafanya majukumu vizuri[emoji106]
 
Wakati unampa big up ukumbuke jimboni kwake wanafunzi wanakaa chini. Na hao ndio wamempeleka Dom.
 
Sijawahi mheshimu wala mtambua Sugu kama mwanasiasa.
 
Private matter not for public consumption - hii tabia ya kuanika mambo binafsi kwenye mtandao ni ulimbukeni mkubwa wa baadhi yetu hasa celebs na celebs wanna be.
 
Mzee wa deiwaka college na deiwaka university, kweli kelele zinalipa
mkuu acha tu, SUGU alikuwa anakuja kutuimbia enzi hizo, watoto wa secondary za Moro, Kigurunyembe, JB, Morosec, n.k tunajazana ndani ya ukumbi wa Forest Hill, tunashabikia kelele zake! leo zimemfikisha hapa, kweli 'mgaa gaa na upwa hali wali mkavu'
 
mkuu acha tu, SUGU alikuwa anakuja kutuimbia enzi hizo, watoto wa secondary za Moro, Kigurunyembe, JB, Morosec, n.k tunajazana ndani ya ukumbi wa Forest Hill, tunashabikia kelele zake! leo zimemfikisha hapa, kweli 'mgaa gaa na upwa hali wali mkavu'
Siasa za bongo zinalipa
 
Once a public figure you are a public property.
Usijitoe akili. simplemind
 
Yule dada atakufa! angekuwa ndugu yangu yule ningempeleka kwa daktari wa akili
 
Sikuwahi kutaraji au kufikiri kama tuna viongozi wanaojali miiko ya uongozi au wanaoishi wanachokihubiri ila hoja yangu hapa ni kuonyesha respect kwa jamii yako.....hayo mengine yupo Mwenyezi Mungu atakayehukumu kila mmoja kwa stahili zake.

Kama ulikuja kwangu Mwanainchi na kunifanya niamini kuwa una uwezo wa kunipunguzia changamoto zinazonikabili...nami ninakupa kura yangu, kamwe sitarajii kuwa kesho utakuja sebuleni kwangu umeshika mguu wa mbuzi unakula ili hali mimi na Watoto tunahitaji tu Pembejeo tukalime tupate ugali.

Kama ni kugawa hovyo zawadi basi Girlfriend wake angekuwa wa mwisho baada ya waliomchagua.

Na ndio maana nimetumia neno show off.......najua wengi wa viongozi tulionao ni hao hao jamii ya Sugu..lakini walau respect basi wanajamii wako wenye matatizo tele...sio kila siku uonekane mitandaoni unakula raha na kugawa zawadi.
 
Wewe unataka pretenderz.
Vip utendeja wake wa kazi unasua sua?
Ahada zake kwa wananchi unazijua au kuzikumbuka? Wema usizidi uwezo anapiga mishe kwa ajili ya life lakini anaongoza na kutekeleza majukumu ya uongozi kwa ajili ya wananchi wake.

Je unataka awe selfish na asifanye majukumu yake kwa cirlc yake na anaowapenda? Kisa eti wew utamwonaje? Ukiachilia mbali uongozi pia ana maisha binafsi na majukum yake pia . Kama ulisaidia kutafuta hizo pesa mpangie na majukum na limitations otherwise hizo akili nyingi ulizo nazo kumpangia mipaka zitumie wewe ku make pesa na fanya yale aliyoshndwa kuyafanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…