Sugu ashinda kesi dhidi ya Faiza kuhusu malezi ya mtoto, Faiza aomba nafasi ya kujirekebisha

Sugu ashinda kesi dhidi ya Faiza kuhusu malezi ya mtoto, Faiza aomba nafasi ya kujirekebisha

Status
Not open for further replies.
Big up kwako Sugu!Bora umemuepusha mwanao na janga asijekuwa kama mtt wa P Funk na kajala!
 
Hapo kwenye kipato si angemuwezesha mama wa mtoto ili awe na uwezo wa kumlea binti....

Ila inauma aiseee kunyanganya mtoto... Hata kama fyuzi zilikata lazima zijiunge fasta.. Namuonea huruma tu

kuna watu hawawezesheki.
unampa mtaji anaenda kutanua na kununulia nguo na kusukia nywele.
kuna jamaa yangu alipanga kumpa demu wake mtaji ili afanye biashara.
akampa 500000 ili ahifadhi.
akaja baada ya wiki mbili na 500000 nyingine anamwambia nipe ile ya mwanzo nichanganye nikafunge mzigo hola.
jamaa mpaka leo hataki hata kumsikia huyo demu
 
Faiza alikuwa anataka kumtumia mtoto kama kitega uchumi.Hope Sugu ana ndugu zake ambao wana uwezo wa kukaa na mtoto

familia za kiafrika zinavyokuwaga kubwa hawezi kukosa wa kumpiga tafu...sema dah! huyo mtoto akija kukua akaenda shuleni wenzake watamtania sana maana picha za maza wake sio kabisa..
 
Ha ni nke huyo au.? Jitu lenda vitakovye nje kama sando za mtoo.?! Sugu bangi moto ela na kwa faiza sebu.! Lile linkaa ka jenda heka.!
 
Baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ kushinda kesi mahakamani ya kutaka apewe amlee mtoto wake aitwaye Sasha,aliyekuwa mzazi mwanzake,Faiza Ally amefunguka kuwa ni bora kufa kuliko kumuona mtoto wake akilelewa na mama mwingine wakati yeye yupo hai.

Sugu alimfikisha mahamakani mzazi mwenziye kwa madai kuwa ameshindwa kumlea mtoto wao kwa kuwa mama huyo si mwadilifu.

Faiza ameandika hivi kupitia Akaunti ya Instagram:

Sielewi joseph ameshindaje kesi- ushahidi wa picha peke yake sioni kama unatosha mimi kupokonya mtoto wangu- mtoto wangu ni mdogo sana ananihitaji sana – na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa ajili ya kusimamia hili- sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana !

Sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili- mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu- nina ndoto na mwanangu nyingi sana – nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea- naona uchungu sana kupelekea mahakani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .

Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe- ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake …mungu naomba nielekeze.nisimamia na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba Sasha.
 
Kwenda zako, kavae kile kitenge chako chenye kama bkn hivi lione malezi gani wampa kutwa nusu nanihii....nenda kakate rufaa ulipe na gharama za kesi.
 
Nafikiri Sugu anajaribu kumprotect Mtoto wake in future asije kuwa bullied na lifestyle ya mama yake... Maana itamuumiza kisaikolojia akishakuwa Mkubwa.
 
lazima ubadilike kwanza, badili tabia uchukue mwanao, Sugu yuko sawa, hiyo tabia yako itamtesa mtoto maishani, ni sawa na kumwambia mtu "we mtoto wa SHETANI"
 
Sheria zingine zingo gender biased tu

Pole faiza
 
Huyu nyota yake ilifaa iendane na huyu. Ni vile walikosa mtabiri.
 

Attachments

  • 1435116633549.jpg
    1435116633549.jpg
    42.3 KB · Views: 578
  • 1435116667465.jpg
    1435116667465.jpg
    45.6 KB · Views: 507
Hee! Huyo dada nae ana mtoto?mbona hafananii?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom