View attachment 262836
Mahakama ya Sinza Mori imetoa hukumu ya hatma ya mtoto wa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na mama wa mtoto wake Faiza kwa kuruhusu mtoto huyo kulelewa na baba yake kwa madai kuwa mama hana vigezo vya kumlea mtoto huyo kimaadili.
Uheard ilipata nafasi ya kuongea na Faiza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo huku akiwa na huzuni kubwa alisema hajatendewa haki na kudai Mheshimiwa Sugu amekua si baba bora kwa mwanae kwani aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuombwa kodi ya nyumba, mlevi sana pia amekua na safari nyingi hivyo hawezi kumuhudumia mtoto wao.
Ameongeza kuwa pamoja na lawama ambazo amepewa kuhusu mavazi yake amedai yuko tayari kujirekebisha lakini si kuchukuliwa kwa mtoto wake ambaye ana miaka miwili kwa kuwa amekua akimuhudumia na kumpa kila ambacho mtoto anastahili kupewa.
Vyanzo: MillardAyo, Mwananchi na Bongo5
Sioni kama hiyo ni kweli ,mtoto anaonekana wa miaka kama 6-9