Sugu ashinda kesi dhidi ya Faiza kuhusu malezi ya mtoto, Faiza aomba nafasi ya kujirekebisha

Sugu ashinda kesi dhidi ya Faiza kuhusu malezi ya mtoto, Faiza aomba nafasi ya kujirekebisha

Status
Not open for further replies.
View attachment 262836

Mahakama ya Sinza Mori imetoa hukumu ya hatma ya mtoto wa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na mama wa mtoto wake Faiza kwa kuruhusu mtoto huyo kulelewa na baba yake kwa madai kuwa mama hana vigezo vya kumlea mtoto huyo kimaadili.

Uheard ilipata nafasi ya kuongea na Faiza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo huku akiwa na huzuni kubwa alisema hajatendewa haki na kudai Mheshimiwa Sugu amekua si baba bora kwa mwanae kwani aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuombwa kodi ya nyumba, mlevi sana pia amekua na safari nyingi hivyo hawezi kumuhudumia mtoto wao.

Ameongeza kuwa pamoja na lawama ambazo amepewa kuhusu mavazi yake amedai yuko tayari kujirekebisha lakini si kuchukuliwa kwa mtoto wake ambaye ana miaka miwili kwa kuwa amekua akimuhudumia na kumpa kila ambacho mtoto anastahili kupewa.

Vyanzo: MillardAyo, Mwananchi na Bongo5

Sioni kama hiyo ni kweli ,mtoto anaonekana wa miaka kama 6-9
 
Tena mijitu mingine ilivyo ya balaa mdogo mdogo unashanga kesho wamempakata na mtoto mwenyewe.
Ndugu wamshauri huyu Mwanamke atulie amwachie Sugu amlee mtoto ,yeye ajitahidi kumtembelea mtoto kiungwana na kusahau ugomvi wao ilikuonyesha mapenzi ya mama kwa Mtoto(Mapenzi ya Wazazi).

Wazazi wengi na tena kwa dunia ya siku hizi wanajisahau sana-hasa wanawake wanajisahau sana kulinda midomo yao na ukiongeza na hizi Mitandao ni shida tu. Hakuna ulazima kubwabwaja ya chumbani kwako hata kama ulikosana na aliyekuwa bwana au Mume wako.

Kwa faida ya afya ya Mtoto mbele ya safari ya maisha yake.Akina mama hata kama mume achana kwa ugomvi na wanaume zenu tabia hii ya kuhorojeka kwenye mitandao au kwa marafiki haina faida yoyote zaidi ya kuwapa uchungu watoto au mtoto uliyemzaa.

Ndio hvyo ingekua mtoto analelewa vizuri mahakama inge balance n kumpa faiza haki.....ila kuna mengi sisi hatujui yatakua yamemyima haki huyo chizi.
Sio kila mwanamke anafaa kua mama na huyo faiza hana akili kuweka mahusiano mtandaoni.
Cku zote uhusiano wa wawili mnajadiliana nyie sio kuhusisha wa2 n kujivua nguo,

Hiyo mahakama imetenda haki tena ingekua mimi ndio sugu hata mtoto asingemuona kwa miaka ila ajifunze
 
Wakuu;

Binafsi nampa hongera mbunge Sugu kwa kufanya uamuzi huu na pia Mahakama iliyotoa hukumu imetenda haki kwa mtoto.

Tuache ushabiki, kwa kweli hapa hakuna maadili. Lazima mtoto atalelewa katika maadili mabovu. tunajenga nini kwa kizazi cha watoto wetu??

Je, huyu mama wa mtoto ndiye huyu member wtu humu FaizaFoxy

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Last edited by a moderator:
Huyu mwanamke alitumiwa kumchafua sugu sasa kibao kimegeuka huwezi kukaa uchi wewe aibu umpe mzazi mwenzio hata kidogo, anadai ana ndoto nyingi na mwanae ndoto gani kwa mavazi haya mbele za mtoto? Anataka mtoto aje aige haya baadae amgeuze mtoto kitega uchumi, waje kuwa na tabia kama za Lulu kuhongwa na waume za watu ili mama aishi poa, hapana aisee kila mwenye mtoto lazima akemee hili, ndio inauma kwa alichofanyiwa kama mzazi ila yeye faiza ndio kapelekea maumivu haya akae augulie ajipange upya kimaadili. Sugu hongera ungechelewa mwanao angekuja kuwa binti bila kujua bikra yake ilitokaje.
 
Wakuu;

Binafsi nampa hongera mbunge Sugu kwa kufanya uamuzi huu na pia Mahakama iliyotoa hukumu imetenda haki kwa mtoto.

Tuache ushabiki, kwa kweli hapa hakuna maadili. Lazima mtoto atalelewa katika maadili mabovu. tunajenga nini kwa kizazi cha watoto wetu??

Je, huyu mama wa mtoto ndiye huyu member wtu humu FaizaFoxy

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Soma post namba 98
 
Sheria zingine zingo gender biased tu

Pole faiza
Hapo sheria imechanganywa na mambo ya kimaadili zaidi na sidhani kunyang'anywa mtoto na mahakama inamaanisha Sugu atakaa nae milele mtoto, endapo katika kipindi cha muda mfupi ujao kama ataonyesha kumhitaji mtoto wake na akajipanga kwenda kumdai bado watamrudishia, hapo fanya kama bro wako ndo alikuwa demu wake kama shangazi mtu unamwona wifi yako wa zamani amepiga pamba za namna hiyo utajisikiaje na bro wako amemwachia mtoto (hata kama maisha ya sasa tunasema kila mtu na maisha yake lakini bado ile hali ya undugu ndugu wa kiafrika tunayo lazima utakuwa una mashaka hata kama kweli anamlea kweli)

Katika situation kama hizi sheria ya mitandao ndio inafaa maana picha za ajabu ajabu kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya rangirangi zipungue na kulinda maadili ya taifa tubaki na za kwenye whatssup tu na kutumiana kwenye email
 
Wakuu;

Binafsi nampa hongera mbunge Sugu kwa kufanya uamuzi huu na pia Mahakama iliyotoa hukumu imetenda haki kwa mtoto.

Tuache ushabiki, kwa kweli hapa hakuna maadili. Lazima mtoto atalelewa katika maadili mabovu. tunajenga nini kwa kizazi cha watoto wetu??

Je, huyu mama wa mtoto ndiye huyu member wtu humu FaizaFoxy

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Theheheheehehe nimecheka sana kwa maandishi yako.
 
Last edited by a moderator:
ukisoma comments za wadada humu utagundua aina ya wamama tulionao kwa maisha ya sasa.

huwezi kuwa unategemea mtoto ndio awe mtaji wa kukufanya wewe uishi na kufanya ujinga mwingine.

mtoto wa kike hawezi hata siku moja kulelewa na mama wa hivi utegemee atakuwa na maadili yoyote kwa jamii.

ni aibu kumtetea mama wa hivi ati kisa ni mwanamke mwenzio
 
View attachment 262836

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu amemshtaki aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally na aliyezaa naye mtoto kwa madai kuwa mwanamke huyo hana maadili na anahofia atamharibu mtoto wao. Sugu anataka kumchukua mtoto huyo na aishi naye (child custody).

Faiza ameiambia Bongo5 kuwa baada ya siku chache zilizopita kupandishwa kizimbani na kujibu shtaka hilo, alisema yeye hawezi kukubali kumuachia Sugu mtoto huyo kwa kuwa yupo chini ya umri.

“Kweli Sugu amenipeleka mahakamani kumtaka mtoto,” amesema Faiza. “Mimi naona ni mtu anayekwepa majukumu kwa sababu chanzo cha yote nilikuwa namkata atulipie kodi ya nyumba, kwa sababu toka tuachane hajawahi kulipa kodi ya nyumba na siyo baba ambae anajali majukumu ya nyumbani kama inavyotakiwa.”

“Kwahiyo nilivyoanza kumshauri kuhusu hilo akaniambia yeye anaweza kumchukua mtoto wake na mali zake anaweza kumlea mtoto wake. Sasa nilivyobishana naye kuhusu hilo wiki moja baadaye ndo likaja ili suala la KTMA ndio akalichukulia kama sababu ya kuweza kupeleka suala mahakamani kwa kudai sina maadili, kwahiyo nitammharibu mtoto. Kwahiyo kesho Jumanne ndio hakimu anatoa hukumu juu ya hili.

Lakini mtoto bado ni mdogo ana miaka miwili na kama miezi tisa bado mdogo anahitaji malezi yangu, pia hili suala nitalipeka ustawi wa jamii ili waangalie haki ya malezi ya mama kwa mtoto.”

=======

Muendelezo:
Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi aliyoifungua Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ dhidi ya mkewe wa zamani

View attachment 262838

Ni habari ambayo imeandikwa na gazeti ya Mwananchi June 23 2015 ikitokea Mahakamani Manzese Dar es salaam kuhusu kesi iliyokua imefunguliwa na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kuhusu mke wake wa zamani.

Taarifa inasema Mahakama ya Manzese imeamuru Mbunge Joseph Mbilinyi akabidhiwe mtoto wao kutokana na kesi aliyoifungua dhidi ya mke wake huyu akidai anamuharibu mtoto.

Hii habari imekuja siku kadhaa tu baada ya TUZO ZA KILI 2015 ambapo mke huyu wa zamani aliingia kwenye headlines kutokana na vazi alilokuwa amevaa.

View attachment 262837

=======

Muendelezo: Alichosema mama wa mtoto wa mhe. Sugu baada ya maamuzi ya mahakama

View attachment 262841

Mahakama ya Sinza Mori imetoa hukumu ya hatma ya mtoto wa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na mama wa mtoto wake Faiza kwa kuruhusu mtoto huyo kulelewa na baba yake kwa madai kuwa mama hana vigezo vya kumlea mtoto huyo kimaadili.

Uheard ilipata nafasi ya kuongea na Faiza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo huku akiwa na huzuni kubwa alisema hajatendewa haki na kudai Mheshimiwa Sugu amekua si baba bora kwa mwanae kwani aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuombwa kodi ya nyumba, mlevi sana pia amekua na safari nyingi hivyo hawezi kumuhudumia mtoto wao.

Ameongeza kuwa pamoja na lawama ambazo amepewa kuhusu mavazi yake amedai yuko tayari kujirekebisha lakini si kuchukuliwa kwa mtoto wake ambaye ana miaka miwili kwa kuwa amekua akimuhudumia na kumpa kila ambacho mtoto anastahili kupewa.

Vijana wote mnapokuwa mnaangalia mwenzi wa maisha msitizame sura na muonekano wa nje.
Haya yamemkuta Sugu lakini naamini wengi wanajuta kwa kuoa watu wanao draw attention ya public.
Beaten once twice shy,pole SUGU!!!!
 
Best interest and welfare principle za makuzi na malezi ya mtoto ndizo zinazompiga chini Faiza. Ashauriwe.!! kwenda ustawi wa jamii anaongeza mzunguko. Ustawi wa jamii hawabadilishi maamuzi ya mahakama. Ajipange akate rufaa akiwa na sababu zilizoshiba. Maamuzi haya ya awali yaweze kupinduliwa na Mahakama ya juu. Otherwise atazunguka sana.

Huyu mama inamuuma maana Mara nyingi watu wa jinsi yake hutumia kisingizio cha mahitaji ya MTOTO lakini ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya anachopewa mama kwa ajili ya malezi ya mtoto huwa anakitumia mama! Hapo mtoto anatumika kama kitega uchumi. Namshauri huyu mama akabidhi maisha yake kwa Yesu ili aokoke! Lakini nadhani uvaaji huu hajauanza leo na baba mtoto anajua hivyo, pamoja na kujua hivyo aliridhia awe mama watoto wake. Sasa asijifanye kushtuka leo. Mimi Nadhani sababu aliyotoa ni kisingizio tu! Sababu halisi anaijua mwenyewe! Sikubaliani kabisa na mavazi hayo, lakini kwa baba mtoto hayo mavazi nadhani anayakubali vinginevyo atoe ushahidi kuwa hii ni tabia ngeni kwa mama huyu. Na kama mama mtoto akiweza kuthibitisha kuwa hayo ndiyo mavazi yake ya kutokea na ndiyo yaliyomvutia Sugu, basi anaweza kushinda rufaa!
 
sugu na yeye alifikilia nini, kuzaa na huyo mwanamke mwezi mchanga.
 
Hiv kweli hii pia inahitaji mtu hadi uwe na uelewa mkubwa?
Prints hizo picha nenda Nursery School waonyeshe watoto bila kusema chochocte haalafu waandalie debate juu ya kwamba Je huyu Mama ungependa akuleeee?ungeona balaa.
Dem kimeo,na kama kawaida ya still pictures hadi wajuu yaaniw atoto wa huyo Mwanae watazikuta picha za Bibi yao.

Hongera Sugu kwa Kushinda kesi,na Mungu akupe baraka na nguvu ya kumlea Mtoto katika Mapenzi mema na malezi yaliyo Bora sana.

Tuachae ushabiki wa kijuha,sio kila kitu Siasa
 
naweza kukubaliana na mahakama kwa upande wa kipato..kwamba faiza hana kipato cha kumlea mtoto vizuri..lakini kwa aadili,sioni kama sugu ana maadili mazuri kushinda ya mama yake.wanasema anapulizaga kwa sana..sasa unadhani kwa mazingia hayo mtoto yuko kwenye mikono salama?..shughuli za kibunge zilivyo sugu lazima awe ana safiri sana na muda mwingi hayuko nyumbani,je atakua anaandamana na mtoto?..akimwacha hao anaowaachia ana uhakika mtoto atakua salama zaidi kuliko mkononi mwa mama yake?..ningekua shangazi wa mtoto ningeomba tuyajadili kama familia...kw aajili uya mtoto na sio kupelekana mahakamani maana naamini ina athari kwa saikolojia ya mtoto....still naamini hakuna mtu anaweza mpenda mtoto kuliko mama yake mzazi!...miezi tisa tumboni si mchezo..labour sio mchezo
Hapo sheria imechanganywa na mambo ya kimaadili zaidi na sidhani kunyang'anywa mtoto na mahakama inamaanisha Sugu atakaa nae milele mtoto, endapo katika kipindi cha muda mfupi ujao kama ataonyesha kumhitaji mtoto wake na akajipanga kwenda kumdai bado watamrudishia, hapo fanya kama bro wako ndo alikuwa demu wake kama shangazi mtu unamwona wifi yako wa zamani amepiga pamba za namna hiyo utajisikiaje na bro wako amemwachia mtoto (hata kama maisha ya sasa tunasema kila mtu na maisha yake lakini bado ile hali ya undugu ndugu wa kiafrika tunayo lazima utakuwa una mashaka hata kama kweli anamlea kweli)

Katika situation kama hizi sheria ya mitandao ndio inafaa maana picha za ajabu ajabu kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya rangirangi zipungue na kulinda maadili ya taifa tubaki na za kwenye whatssup tu na kutumiana kwenye email
 
Safi sana Sugu janamke popo kama Hilo halifai kukulelea mwanao jiulize alimwacha mtoto na nani wakati anaenda kuonyesha masaburi yake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom