Sugu ashinda kesi dhidi ya Faiza kuhusu malezi ya mtoto, Faiza aomba nafasi ya kujirekebisha

Sugu ashinda kesi dhidi ya Faiza kuhusu malezi ya mtoto, Faiza aomba nafasi ya kujirekebisha

Status
Not open for further replies.
Kwanza kile ni kitoto kidogo sana kwangu, nnahisi hata mwanangu wa kwanza ni mkubwa kwa yule.

Pili, hana vigezo.

Kweli usilolijuwa ni usiku wa kiza. Sikulaumu.

Alaa, basi mie nilidhani bucha zote maini radha sawa ati!
 
Alaa, basi mie nilidhani bucha zote maini radha sawa ati!

= ladha

Dhana yako si sahihi. Unaweza mfananisha yule kinyangarakata na mama'ko? mama'ko anaweza kwenda kuvaa nepi na kujianika robo tatu utupu mbele ya halaiki ya watu namna hii:


Aliyekuwa Mke wa Mbunge Mh. Sugu Faiza Ally Atoa Mpya..Avaa Pampers​
 
Nao wananchi wa Mbeya Mjini nao hamnazo, utamchaguaje mwendawazimu kama Sugu anayetembea na kuzaa na hamnazo kama Faiza? Mwanaume mwenye akili sawa sawa hawezi kufuata malaya kama yule. Huu ni wakati wa wana Mbeya kujipima ili Oktoba ikifika muamue mambo ya maana. Tupa mbali sugu na Faiza.

Huu sasa urojo...!! Watu wanaotumia masaburi kuwaza utawajua tu....
 
km mtoto ni mdogo uyo ---- alikua anapata wapi muda wa kwenda kwenye hvo vipati vya kina zari na ktma tena usiku? acha sugu amchukue dogo tuu atalelewa ht na bibi yake
 
Vazi tuu linatosha kutoa utambulisho wa tabia yako kwa watu, mama mzazi unaenda out makalio nje pwaaaaa..... unarudi alfajiri afu nikuachie mtoto wangu...

Never never and never!!!!

Sugu Chukua mtoto wako, mwache Faiza aendelee kumeki headlines
 
naweza kukubaliana na mahakama kwa upande wa kipato..kwamba faiza hana kipato cha kumlea mtoto vizuri..lakini kwa aadili,sioni kama sugu ana maadili mazuri kushinda ya mama yake.wanasema anapulizaga kwa sana..sasa unadhani kwa mazingia hayo mtoto yuko kwenye mikono salama?..shughuli za kibunge zilivyo sugu lazima awe ana safiri sana na muda mwingi hayuko nyumbani,je atakua anaandamana na mtoto?..akimwacha hao anaowaachia ana uhakika mtoto atakua salama zaidi kuliko mkononi mwa mama yake?..ningekua shangazi wa mtoto ningeomba tuyajadili kama familia...kw aajili uya mtoto na sio kupelekana mahakamani maana naamini ina athari kwa saikolojia ya mtoto....still naamini hakuna mtu anaweza mpenda mtoto kuliko mama yake mzazi!...miezi tisa tumboni si mchezo..labour sio mchezo

Kama ingekuwa sio issue ya hayo mavazi hata kama hana uwezo, kwa umri wa huyo mtoto isingeruhusiwa apewe Sugu kwa kuwa baba wa mtoto ana jukumu la kutoa ela ya matunzo mpaka mtoto atakapofikia umri ambao upo recommended kwa baba wa mtoto kumchukua.

Maamuzi yaliyofanyika ni kama temporary solution kwa kuwa hata mitaani tumeshuhudia wamama wachache waliopinda wanawafungia watoto wadogo wanakwenda kuserebuka huku nyuma majanga yanawatokea jamii inaanza kuwazonga. Ni kweli hakuna kama mama mbele ya mtoto hata kama ni jangudoa ila kuna wengine wamepinda aisee japo ni kundi dogo na ndio maana hata hao wakaona huyu kama ameshona nguo ya namna hii alafu anapigwa picha kwa hiyari yake na kugeuka kwa mapozi tofauti tofauti kwanini wasiamini kwamba ipo siku anaweza akafanya tukio la ajabu, though kulikuwa na uwezekano wa kumpa lakini kama ingetokea madhara flani kwa mtoto lazima watu watapiga kelele.

Hapo amezidiwa ujanja na Sugu akajenga hoja zimeonekana zina mashiko, issue ya bangi kwa kuwa hakuna mtu aliejitokeza kueleza ukweli inabaki ni story tu unless kama aliwahi kupelekwa rehabs hapo ingekuwa shida nyingine
 
Kama kuna sehemu taasisi za serikali zinajitahidi kutoa haki basi ni kwenye masuala ya custody ya mtoto na matunzo ya mtoto. Naamini, mahakama imetenda haki kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na hadhi ya mahakama yenyewe. Tuelewe kuwa ktk mahakama za mwanzo, lengo kuu linakuwa kwa kiasi kikubwa ni 'kupatanisha', ndo maana hata mawakili hawaruhisiwi. Tena tukumbuke Faiza hajakana tuhuma dhidi yake-amesema yupo tayari kujirekebisha.

Pia ningependa kupitia nafasi hii niipongeze ofisi ya Ustawi wa Jamii iliyo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Ni Ofisi iliyojaa wadada wanaofanya kazi zao kwa ueledi na uadilifu mkubwa bila kujali jinsia wala kipato cha mtu. Nawapa hongera za dhati.

Katika suala la Sugu kuna mambo 4 ambayo inabidi tuyaelewe:
  1. Kuna uwezekano mtoto anatumika kama kitega uchumi au chambo. Ikumbukwe, jukumu la kulea mtoto ni la wazazi wote wawili. Hivyo wazazi wote lazima wajishughulishe kutafuta kipato kwa ajili ya malezi ya mtoto. Faiza hana kazi inayoeleweka na Sugu ni Mbunge ambaye anakipato kikubwa na hadhi. Kuna kitu dada zetu hawajui-kwa mujibu wa Ustawi wa Jamii, ukiachana na mwanaume haina maana mwanaume huyo anajukumu la kumlea mwanamke na mtoto. Mwanaume anawajibika kutoa sehemu ya matunzo. Wasiwasi wangu ni kuwa Faiza alikuwa anatumia mahitaji ya mtoto kama njia ya kuvuta pesa kutoka kwenye 'ATM', ndo maana unaona anaomba pesa ya kodi. Kwanini Sugu aingie gharama ya kumtunza mwanamke ambaye hayupo nae tena kimahusiano?
  2. Kisasi. Wapenzi wengi wanapoachana kuna kuwa na hali ya kutaka kukomoana na kama kuna watoto/mtoto basi wao pia hutumiwa ili kukomoana. Wengi hatukumjua Faiza kabla hajaachana na Sugu. Lakini alipoachana nae ndipo tukamjua kupitia vimbwanga vyake vya pampasi, shati bila suruali/sketi/bukta na gauni la kamba. Naamin lengo lake lilikuwa kumkomoa Sugu kwa kumharibia hadhi yake mbele ya jamii na wapiga kura wake, maana ingekuwa tabia yake angekuwa ameshayafanya haya kabla hajaolewa au wakati yupo na Sugu.
  3. Mtoto alikuwa hatarini zaidi angeendelea kuishi na mama yake. Jamani, tunaishi ulimwengu wa kidigitali. Kila kitu kinachowekwa mtandaoni kinaendelea kuwapo kwa muda mrefu zaidi kuliko namna nyingine ya kutunza kumbukumbu. Mtoto wa Sugu, kama mtoto wa mwanasiasa, tena wa upinzani angekuwa rahisi kuonewa na wenzake shuleni na hata kwenye mtandao kutokana na kile mama yake akifanyacho(easy target for bullies and cyberbullying). Hakuna mtoto anayestahili hili. Tuwaweke watoto wetu mbali na mtandao.
  4. Faiza ni mzembe. Ingawa wanasema uchungu wa mwana aujua mzazi, sijaona uchungu wa huyu dada kwa mtoto. Machozi yake nayafananisha na machozi ya Mamba. Alipoachana na Sugu na kupewa custody ya mtoto (mpaka mtoto afikishe miaka 5 (is it 7?), ndipo anaweza kuishi na baba) alitakiwa ajue it is just a matter of time kabla hajachukuliwa na baba yake. Alitakiwa achunge matendo yake, alitakiwa awe mama mzuri na aonekane ni mama mzuri. Lakin kwa uzembe akaamua ajielekeze katika kumuumiza mzazi mwenzie bila kujua kuwa anampa hasira za kudai mtoto.

Mwisho, hii tabia ya BAADHI ya wanawake kuwafanya wazazi wenzao ni 'cash cows' ife.Tabia hii inarudisha nyuma harakati za kupambana na mfumo dume.Lazima waone fahari ktk kutafuta chao kwa ajili ya watoto wanaowazaa. Faiza ananafasi ya kupata custody ya mtoto akienda mahakama za juu. Akienda huko atafute wakili na pia asiiambie mahakama kwamba atajirekebisha, maana kufanya hivyo ni kukiri kuwa ana matatizo. Ikumbukwe sheria zinaangalia maslahi ya mtoto, ndo maana ktk hali ya kawaida mtoto wa miaka 2 kama Sasha alitakiwa kuishi na mama yake, lakin mazingira yako tofauti
 
Faiza amehojiwa na wanaharakati na hizi ni hoja zake:
1.kwamba sugu nae hafai kuwa baba kwasababu ni mvuta bangi (hili wana hip hop wenzake mtasaidia)
2. Sugu si mkaaji nyumbani so mtoto ataishi kwa bibi au mama sugu. Hapa kuna madogo ambao wamekuwa wakimlala Dada Wa kazi kwa mpigo kiasi kwamba baba hajulikani kati yao. Hivyo pia si salama kwa ustawi Wa mototo.
3.Kwamba home kwa sugu daily kunaingia Dada poa. Hili pia si salama kwa makuzi ya mtoto.
4. Toka waachane sugu hajawahi toa matumizi ya mtoto na hata shule hajui mtoto alikuwa anasoma shule gani. Faiza anahoji Inakuwaje baba Wa namna hii asiyejali mtoto akabidhiwe mtoto ambae hamjali?
5. Kama kigezo ni mavazi tu basi amekubali atajirekebisha.
6. Kwamba swala hili limeibuka wakati mh. Sugu alipoombwa child support.
7. Kwamba hata ujauzito Wa Sasha sugu alitaka utolewe ila faiza alikataa baada ya sugu kuwa amempa mimba tatu mwanzo ambazo zote alilazimisha zitolewe.
8. Kwamba sugu ni mdhalilishaji (m...la...w...i...tiiiiii) Wa wanawake (mifano IPO. MF. Shy rose, binti Wa Sweden, faiza n.k). Sasa baba mdhalilishaji anawezaje kuwa mlezi bora.

Duhh kama usemayo faiza ni kweli basi huyu mtoto mpelekeni pale SOS mawasiliano akalelewe pale. Manake kila mahali ni moto.
 
Faiza amehojiwa na wanaharakati na hizi ni hoja zake:
1.kwamba sugu nae hafai kuwa baba kwasababu ni mvuta bangi (hili wana hip hop wenzake mtasaidia)
2. Sugu si mkaaji nyumbani so mtoto ataishi kwa bibi au mama sugu. Hapa kuna madogo ambao wamekuwa wakimlala Dada Wa kazi kwa mpigo kiasi kwamba baba hajulikani kati yao. Hivyo pia si salama kwa ustawi Wa mototo.
3.Kwamba home kwa sugu daily kunaingia Dada poa. Hili pia si salama kwa makuzi ya mtoto.
4. Toka waachane sugu hajawahi toa matumizi ya mtoto na hata shule hajui mtoto alikuwa anasoma shule gani. Faiza anahoji Inakuwaje baba Wa namna hii asiyejali mtoto akabidhiwe mtoto ambae hamjali?
5. Kama kigezo ni mavazi tu basi amekubali atajirekebisha.
6. Kwamba swala hili limeibuka wakati mh. Sugu alipoombwa child support.
7. Kwamba hata ujauzito Wa Sasha sugu alitaka utolewe ila faiza alikataa baada ya sugu kuwa amempa mimba tatu mwanzo ambazo zote alilazimisha zitolewe.
8. Kwamba sugu ni mdhalilishaji (m...la...w...i...tiiiiii) Wa wanawake (mifano IPO. MF. Shy rose, binti Wa Sweden, faiza n.k). Sasa baba mdhalilishaji anawezaje kuwa mlezi bora.

Duhh kama usemayo faiza ni kweli basi huyu mtoto mpelekeni pale SOS mawasiliano akalelewe pale. Manake kila mahali ni moto.

Kwa hiyo mh shy rose alifumuliwa marinda na sugu?
hii sio sababu ya kufanya mtu asipewe custody ya mtoto kutoka kwa mama hovyo kama yule.
huyu dada mambo anayozidi kuyaongea ndio jamii inazidi kumuona ni punguani na hana maana yoyote.

Bob marley alikuwa mvuta bangi mzuri na mkewe lakini waliwalea watoto wao kwa maadili ya kule na kuwawezesha kufanikiwa.
 
Daaaaaahh!!

Asante nimeiona hiyo post #98 .

Umejua kupangua mpira wa penalt!!!!!!!!!!

Binafsi nilitaka kushangaa kwani sitegemei mtu kama wewe unaweza kufanya mambo kama hayo ya huyo mwenye jina linalofanana na lako.

wewe ni mtu makini hata hapa katika post zako unaonekana.

Honngera sana, endelea hivyo hivyo.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

mkuu mbna umemwagia sifa hivi!!! au ndio unatengeneza mapito kwa huyo dada?
nakupa wiki moja lzm utapishana nae mfatilie ktk post zake
 
Huyu mwanamke aikua akifanya makusudi kumdhalilisha Mbunge, mbona zamani hata kabla yakuzaa hakuwahi kufanya hivyo...Imekula kwake

Umewahi kuona nguo alizokuwa akivaa toka hapo awali?
Je huyo Mh.alimkuta kwenye mavazi gani mpaka wakapeana mimba..ktk hali ya Kijamii kwakweli hatuna haki ya kuhukumu kesi hii lakini kwa kuwa maamuzi ya mahakama yanabebwa na facts basi yatupasa kuheshimu..
Lakini mimi ninayemfahamu Faiza kuvaa vile ni kawaida yake hata kabla ya kuwa mama.
Anyway kuna picha alipiga amevaa kichupi na akiwa mja mzito ni warning gani alipewa na Mheshimiwa akiaa kama mhusika aliyekuwa akilea mimba.
Hapa kuna mambo mengi tuu..ila kwa mtazamo wangu mahakama ilipashwa kuangalia saana umri wa mtoto na ingempa kipindi ajirekebishe juu ya mavazi yake.
 
Kwanza kile ni kitoto kidogo sana kwangu, nnahisi hata mwanangu wa kwanza ni mkubwa kwa yule.

Pili, hana vigezo.

Kweli usilolijuwa ni usiku wa kiza. Sikulaumu.

kwa mwandiko wako humu huna miaka 40..prove me wrong
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom