Binafs yangu siyo Muccm! Ila kwenye hili tuacheni masikhala bhana!
Sifa moja wapo ya kuwa Rais wa mabunge Duniani IPU, ni lazima uwe mbunge pia katika nchi utokayo
Swali langu ni dogo tu hapa, Dr.Tulia asipoutetea ubunge wake pale Mbeya mjini, anakuwa amekosa sifa za kuendelea kuwa Rais wa mabunge Duniani
Inafahamika kabisa kwamba, Wanambeya wanaweza wasimpe kura za kutosha Dr.Akson Tulia, Je, hata sisi Watanzania tukubali kukosa hii heshima mojawapo katika nchi yetu ya Dr. Tulia kuwa kiongozi mkubwa anayetambulika Duniani kwa kushindwa kumwambia Sugu asigombee au kumwibia kura zake mara tu itakapoonekana kashinda
Embu fikiri..! Nafasi hiyo hiyo ingelikuwa iko kwa Sugu, ni kweli wanachadema na Watanzania wangependa Sugu atoke kwenye nafasi hiyo na kupoteza sifa ya kuwa Rais wa IPU kwa sababu tu kuna Dr Tulia kamzidi kura? Isingewezekana bhana!
Mh Sugu, tafadhari tafuta jimbo lingine mapemaa!