Sukari inauzwa hadi 5000 na Serikali iko kimya hadi sasa, bei elekezi ni ipi?

Sukari inauzwa hadi 5000 na Serikali iko kimya hadi sasa, bei elekezi ni ipi?

Hamna chochote mnachoweza kuifanya hiyo serikali ya CCM. Mkileta chokochoko mtapigwa virungu

Hamieni Burundi.
 
Hivi hii Serikali inafuatilia kweli maisha ya Wananchi wake huko mitaani? Watu wanauziwa Sukari Tsh. 5000 kwa kilo na Wafanyabishara hata hawana hofu yoyote.

Ni kwamba hakuna anayejali hali za Wananchi tayari linatengenezwa tatizo la kisiasa ili waje walitumie kwenye kampeni zao?
Dah!... hatari hii
 
Matatizo ya bei ya sukari hayawezi kumalizwa na serikali kutoa bei elekezi.

Ingekuwa hivyo, serikali ingetoa bei elekezi ya shilingi moja kila mtu awe na sukari bwerere.

Matatizo ya sukari yatamalizwa kwa serikali kuweka mazingira rafiki zaidi ya uzalishaji, sukari ikizalishwa kwa wingi, kwa ufanisi zaidi, na wazalishaji mbalimbali nchini, bei itashuka automatically kutokana na nguvu za soko za supply and demand.

Sasa, kama kweli unataka kutatua tatizo la bei ya sukari, na bidhaa nyingine yoyote, angalia mifumo ya kiserikali kwenye kuchochea uzalishaji, angalia sheria za viwanda, angalia mikopo kwa wafanyabiashara wanaouza sukari, angalia sheria za ardhi, angalia matatizo ya wazalishaji wa sukari , angalia ukiritimba wa kiserikali unaowakabili wazalishaji, angalia predictability ya soko la sukari nchini na matatizo ya wazalishaji wa nje kuingiza sukari yenye bei rahisi kwa mara moja na kuingilia soko la ndani na ku discourage uzalishaji zaidi ndani.

Angalia matatizo yanayojikita kwenye mchakato mzima wa uzalishaji.

Usiangalie bei elekezi tu.

Katika dunia ya leo, bei haipangwi na serikali, bei inapangwa na incentives zinazoendana na nguvu za soko, demand and supply.

Mimi kama ni mfanyabiashara wa sukari, mzalishaji, halafu gharama zangu za uzalishaji ni sh 5,000 kwa kilo, halafu serikali ikaja kunipa bei ya kuuza sh 4,000 kwa kilo, nitauza batch hiyo kwa hasara na kufunga kiwanda.

Kwa sababu kuendelea kuzalisha na kuuza kwa bei elekezi ni kuendelea kupata hasara. Hakuna mfanyabiashara mwenye akili timamu ambaye anafanya biashara ili apate hasara.

Sasa hapo mimi kufunga kiwanda kutamsaidiaje mlaji wa mwisho in the long term?

Hii miradi ya kuzalisha sukari iliishia wapi?

Mnashindwa nini kuachana nayo

Na nyie wasusieni tu wakae n sukari

Yao wale wao na familia zao uone

Kama hawatoiuza

Acheni kuwa watumwa

Ova
Kwanza wataalamu wa afya wanashauri watu wapunguze matumizi ya sukari.
 
Them Say...... 'Stop Crying Like Babies' Use Alternatives......PIPI GOLOLI (AKA) LAWALAWA GOLOLI 👇👇👇👇👇👇
1.jpg

2.jpg
 
Nchi Ya Ajabu Sana Nilikuwa Mkoa Mmoja Nikapanda Daladala Umbali Usiozidi Kilometers 10 Wanatoza Nauli Tshs 700 Na Ikifika Usiku Tshs 1500/= Bila Kujari Umbali
Nikampigia Kiongozi Wa LATRA Simu Nikamuuliza Ninyi Ndiyo Mamlaka Ulipewa Kusimamia
Usafirishaji Wa Abiria Na Kupanga Bei

Kwanini Mnaacha Wenye Daladala WaAmue Kutoza Pesa Watakavyo Hawana Tickets
Kama Tupo Banana Republic. Akasema Sasa Naomba Unitumie Number Za Daladala
Nikamjibu Kinachotakiwa Toka Ofisini Ingia Field Kuhakikisha Nauli Ni Zile Mlizosema

Baadaye Napanda Daladala Hali Imekuwa Sawa Wanatoza Nauli Iliyotangazwa
Huu Unaoitwa Uholera Unatengenezwa Na Serikali Yenyewe Sukari Inapanda
Serikali Haisemi Lolote Sijui Bodi Ya Sukari Kimya
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Ila Samia ana aibisha sana hili taifa aisee!

Yani ni kama nchi inajiendea tu
 
Hivi hii Serikali inafuatilia kweli maisha ya Wananchi wake huko mitaani? Watu wanauziwa Sukari Tsh. 5000 kwa kilo na Wafanyabishara hata hawana hofu yoyote.

Ni kwamba hakuna anayejali hali za Wananchi tayari linatengenezwa tatizo la kisiasa ili waje walitumie kwenye kampeni zao?
nyie ndio mko kimya, Ingekuwa ni Kenya raia wangeisha lianzisha, Nyie hata ikiuzwa Tsh 10,000/ hakuna kitu mnaweza fanya tofaut na kulalamika
 
bei elekezi ilikuwa awamu ya Mkapa tuu baada ya hapo kila mtu anauza bidhaa bei anayotaka awamu hii imevunja record
 
Bei ya soko Gani hiyo ndugu?

Hopping ni mwisho wa Nchi.
 
Poleni kwa mnaotumia sukari

Nyie ni watumwa na mna addiction

Ona mnavyohaha,kwani lazima mtumie sukari

Ova
wewe utakuwa mgonjwa uliyezuiwa kutumia sukari pole, sukari haikwepeki sukari ipo mpaka kwenye pombe.
 
Hivi hii Serikali inafuatilia kweli maisha ya Wananchi wake huko mitaani? Watu wanauziwa Sukari Tsh. 5000 kwa kilo na Wafanyabishara hata hawana hofu yoyote.

Ni kwamba hakuna anayejali hali za Wananchi tayari linatengenezwa tatizo la kisiasa ili waje walitumie kwenye kampeni zao?
Unaambiwa Mama hana habari yeyote, yeye yuko bize kumung'unya kungu na kwenda Uarabuni kuweka mazingira yake sawa baada ya kustaafishwa kwa manufaa ya umma.
 
Hivi hii Serikali inafuatilia kweli maisha ya Wananchi wake huko mitaani? Watu wanauziwa Sukari Tsh. 5000 kwa kilo na Wafanyabishara hata hawana hofu yoyote.

Ni kwamba hakuna anayejali hali za Wananchi tayari linatengenezwa tatizo la kisiasa ili waje walitumie kwenye kampeni zao?
Inatakiwa kuuzwa 9000
 
Back
Top Bottom