Hivi hii Serikali inafuatilia kweli maisha ya Wananchi wake huko mitaani? Watu wanauziwa Sukari Tsh. 5000 kwa kilo na Wafanyabishara hata hawana hofu yoyote.
Ni kwamba hakuna anayejali hali za Wananchi tayari linatengenezwa tatizo la kisiasa ili waje walitumie kwenye kampeni zao?
Matatizo ya bei ya sukari hayawezi kumalizwa na serikali kutoa bei elekezi.
Ingekuwa hivyo, serikali ingetoa bei elekezi ya shilingi moja kila mtu awe na sukari bwerere.
Matatizo ya sukari yatamalizwa kwa serikali kuweka mazingira rafiki zaidi ya uzalishaji, sukari ikizalishwa kwa wingi, kwa ufanisi zaidi, na wazalishaji mbalimbali nchini, bei itashuka automatically kutokana na nguvu za soko za supply and demand.
Sasa, kama kweli unataka kutatua tatizo la bei ya sukari, na bidhaa nyingine yoyote, angalia mifumo ya kiserikali kwenye kuchochea uzalishaji, angalia sheria za viwanda, angalia mikopo kwa wafanyabiashara wanaouza sukari, angalia sheria za ardhi, angalia matatizo ya wazalishaji wa sukari , angalia ukiritimba wa kiserikali unaowakabili wazalishaji, angalia predictability ya soko la sukari nchini na matatizo ya wazalishaji wa nje kuingiza sukari yenye bei rahisi kwa mara moja na kuingilia soko la ndani na ku discourage uzalishaji zaidi ndani.
Angalia matatizo yanayojikita kwenye mchakato mzima wa uzalishaji.
Usiangalie bei elekezi tu.
Katika dunia ya leo, bei haipangwi na serikali, bei inapangwa na incentives zinazoendana na nguvu za soko, demand and supply.
Mimi kama ni mfanyabiashara wa sukari, mzalishaji, halafu gharama zangu za uzalishaji ni sh 5,000 kwa kilo, halafu serikali ikaja kunipa bei ya kuuza sh 4,000 kwa kilo, nitauza batch hiyo kwa hasara na kufunga kiwanda.
Kwa sababu kuendelea kuzalisha na kuuza kwa bei elekezi ni kuendelea kupata hasara. Hakuna mfanyabiashara mwenye akili timamu ambaye anafanya biashara ili apate hasara.
Sasa hapo mimi kufunga kiwanda kutamsaidiaje mlaji wa mwisho in the long term?
Hii miradi ya kuzalisha sukari iliishia wapi?
Five agro-investors in the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (Sagcot) have received about Sh1.6 billion from the body’s Catalytic Trust Fund (CTF) established to stimulate their...