Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Suleiman Kova, kamanda wa polisi aliyewahi kutamba kwa kuzuia uhalifu akiwa RPC kwenye mikoa mbalimbali ameongelea hoja ya Gwajima kuomba mabadiliko ya mic na kiti. Amesema kwa uzoefu wake ndani ya Jeshi la Polisi na kuhoji watuhumiwa huwa ni suala la saikolojia kwa mtu mwenye msongo wa mawazo na kutojiamini yeye mwenyewe na kutoamini wengine.
Pia, soma=> Bungeni: Askofu Gwajima agoma kukalia kiti na kutumia kipaza sauti alichoandaliwa na Kamati ya Maadili
Kamanda Mstaafu Kanda Maalum ya Dar es saalaam Kamishna Suleiman Kova leo kwenye Amplifaya ya Clouds FM ameelezea tukio la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kuomba kubadilisha kiti na microphone vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yake kuvitumia wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge Dodoma, Kova ameelezea tukio kama hili kwa kutumia uzoefu wake akiwa Polisi na kuhoji Watu mbalimbali wenye tuhuma.
"Wakati mwingine Mtu akishafanya jambo flani anakuwa na hisia flani ambazo sio za kawaida labda anafikiri nikikaa hapa naweza nikadhurika, ni tatizo la kisaikolojia kwa Mtu ambae ana msongo wa mawazo anakuwa hajiamini na haamini Mtu yeyote yule, kwahiyo anaweza kufanya jambo lolote lile”
"Mfano mimi zamani nilikuwa nahoji Wahalifu, akiletwa kwangu akisikia ni Kova anapoingizwa mule ndani anadondoka chini paap bila kumgusa, yani anaona amekutana na kitu cha hatari sana kutokana na yeye anavyoelewa, kama ni madhambi anayakumbuka yote"
Kamanda Mstaafu Kanda Maalum Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.
Pia, soma=> Bungeni: Askofu Gwajima agoma kukalia kiti na kutumia kipaza sauti alichoandaliwa na Kamati ya Maadili
========Kamanda Mstaafu Kanda Maalum ya Dar es saalaam Kamishna Suleiman Kova leo kwenye Amplifaya ya Clouds FM ameelezea tukio la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kuomba kubadilisha kiti na microphone vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yake kuvitumia wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge Dodoma, Kova ameelezea tukio kama hili kwa kutumia uzoefu wake akiwa Polisi na kuhoji Watu mbalimbali wenye tuhuma.