Suleiman Kumchaya haijui historia ya TANU karudia maneno ya mzee Pius Msekwa kuhusu TAA

Kuna kitu cha kutusaidia hapa kiongozi
britanicca instanbul Laki Si Pesa
Chillah,
Kwanza nakushukuru kwa kutuwekea Medali ya Mwenge wa Uhuru ya Mzee Suedi Kagasheki.

Nimefahamiana na mwanae Balozi Abdallah Kagasheki kuanzia miaka ya 1980 alipokuwa Balozi Saudi Arabia na nikimtembelea nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam kila alipokuwa likizo na niliwahi mwaka wa 2000 kufika nyumbani kwake Bukoba lakini bahati mbaya alikuwa amesafiri kwa hiyo hatukuonana.

Nimejuana vilevile na wajukuu wa Mzee Suedi Kagasheki yaani watoto wa Balozi Abdallah Suedi.
Nimemtaja Mzee Suedi Kagasheki katika kitabu cha Abdul Sykes na naweka hapo chini sehemu hizo:
1951
''Dr Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kufuzu udaktari.​
Baada ya kuelezwa kuhusu ule mkutano wa Arusha, Dr Mutahangarwa alimwonya Dossa kuhusu hatari ya mwenendo aliokuwa akichukua Abdulwahid kama Katibu na Rais wa TAA.​
Dr Mutahangarwa alimweleza Dossa hatari ambazo TAA na uongozi wake ungezikabili pindi serikali ikigundua kwamba TAA ilikuwa ikijaribu kuunganisha mapambano ya TAA na yale ya KAU.​
Hofu hii aliyoonyesha Dr Mutahangarwa ilikuwa bila wasiwasi wowote hofu ya kweli kabisa kwa sababu KAU ilikuwa inaunga mkono harakati za Mau Mau na Waingereza waliamini kuwa uongozi wa mapambano yale ulikuwa ukitoka KAU na Kenyatta wakiwa na Kaggia walishukiwa kuwa kati ya viongozi hao.​
Kutoka Mwanza Dossa alipanda meli hadi Bukoba ambako alipokewa na Chifu Rutinwa pamoja na mwanasiasa mkongwe, Ally Migeyo na Suedi Kagasheki na wanachama wengine wa TAA katika tawi la Bukoba.​
Aliporudi Dar es Salaam, Dossa alikamatwa katika stesheni ya gari moshi na kupelekwa Central Police.''​

1967
''Mwezi Novemba 1967 Tewa Said Tewa alikuwa amefanya ziara ya Mwanza na Bukoba iliyokuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa alifanya majadiliano na viongozi wa Waislam wa huko kama Sheikh Amin Abdallah wa Mwanza, Sheikh Ali Migeyo na Sheikh Suedi Kagasheki wa Bukoba.''​
 
Nashukuru kwa historia hii... Naomba kuja ma swali mengine ambayo yatanisaidia kupata kujua zaidi historia ya nchi yetu
 

Huyu mjukuu wa Dr Mutahangarwa kajaribu kueleza kidogo historia yao...
 
Chilla,
Vitabu hivi utavipata Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema na pia Msikiti wa Mtambani kuna vya Kiingereza na Kiswahili bei elfu kumi tu.
Kwanini vitabu vyako unauza misikitini ?
Uza kwenye maduka ya kawaida pia, au walengwa no waislamu wenzio?
 
Kwanini vitabu vyako unauza misikitini ?
Uza kwenye maduka ya kawaida pia, au walengwa no waislamu wenzio?
Remote,
Ibn Hazm ndiyo waliochapa kitabu hiki na wao wana maduka yao hayo ambayo hayako msikitini kama unavyodhani ni kama mfano wa Cathedral Bookshop pale St. Josephs' kwani duka hili lipo kanisani?

Cathedral Bookshop lipo pembeni ya kanisa na haya maduka yetu pia ni hivyo hivyo unaweza tu kufika Mtaa wa Mafia Msikiti wa Manyema utauona kwa pembeni na hivyo hivyo Mtoro na Mtambani.

Wanapenda kuuza vitabu vyao kwenye maduka mengine ya vitabu lakini hawataki kuchukua vitabu vyetu basi ndiyo tunauza kwenye maduka yetu.

Tanzania Publishing House huwa wanachukua vitabu vyetu, Soma Bookshop na Elite Bookshop lakini biashara ya vitabu ni ngumu sana.
 
Asante nitapita hapo.
 
Mohamed usilazimishe kuwa wewe ndiye mwenye hati miliki ya historia ya TAA,TANU nk..
 
Mohamed usilazimishe kuwa wewe ndiye mwenye hati miliki ya historia ya TAA,TANU nk..
Wakuku...
Hapana siwezi kulazimisha ila ukweli na hiki ndicho ninachoringia ni kuwa mimi ndiye wa mwanzo kusema kuwa hii historia inayosomeshwa na watu wakaiamini si historia ya kweli ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nikaandika kitabu kueleza historia yenyewe kama ilivyotakiwa kuandikwa.

Lakini kubwa ndiye mtafiti pekee ukimtoa John Iliffe ambae nimeziona na kusoma Nyaraka za Sykes.

Umuhimu wa hili ni kuwa wao ndiyo waasisi wa African Association na waasisi wa TANU na ndiyo waliompokea Mwalimu Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…