Suleiman Kumchaya haijui historia ya TANU karudia maneno ya mzee Pius Msekwa kuhusu TAA

Mkuu unafahamu historia ya wachagga?
Walimtangulia sana Nyerere.
Mfumo wao wa Uongozi hadi mwaka 1954 ulikuwa mbali sana.

Ulishasikia kitu kuhusu Mangi Thomas Marialle?
Uran,
Siku moja nikiwa na Abbas Sykes tulikwenda nyumbani kwa David Marealle.

David Marealle alikuwa jirani yangu.

David Marealle akaniambia,"Nimekuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza nimefikia nyumbani kwao hawa."

David Marealle anamnyooshea Bwana Abbas mkono.

Chief Thomas Marealle alikuwa rafiki yake Abdul Sykes na Abdul akimtania Chief Marealle akimwita, "King."

Alikuwa akimwambia, "Tom Waingereza hawataki kukuita King ili usifanane na mfalme wao King George."

Mimi nimekutana na Chief Marealle katika Nyaraka za Sykes.

Nimesoma hadi barua zake binafsi alizokuwa akiandikiana na akina Sykes, Chief Marealle akieleza fikra zake kuhusu harakati za uhuru na hali ya baadae ya Tanganyika.

Kupitia barua hizi nimejua mengi yaliyokuwa ndani ya Chagga Council.
 
Uran,
Siku moja nikiwa na Abbas Sykes tulikwenda nyumbani kwa David Marealle.

David Marealle alikuwa jirani yangu.

David Marealle akaniambia,"Nimekuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza nimefikia nyumbani kwao hawa."

David Marealle anamnyooshea Bwana Abbas mkono.

Chief Thomas Marealle alikuwa rafiki yake Abdul Sykes na Abdul akimtania Chief Marealle akimwita, "King."

Alikuwa akimwambia, "Tom Waingereza hawataki kukuita King ili usifanane na mfalme wao King George."

Mimi nimekutana na Chief Marealle katika Nyaraka za Sykes.

Nimesoma hadi barua zake binafsi alizokuwa akiandikiana na akina Sykes Chief Marealle akieleza fikra zake kuhusu harakati za uhuru na hali ya baadae ya Tanganyika.

Kupitia barua hizi nimejua mengi yaliyokuwa ndani ya Chagga Council.
Kuna mambo mengi sana kwenye hii Historia yanafichwa sana.
Hii Chagga Council ilikuwa na nguvu sana
 
hiyo Chaga Council ndio iliyotoa rasimu la kutaka kujitenga na Tanganyika na kuunda nchi yao ya Chagaland. Mareale ndio alienda UN kudai uhuru wa Chagaland
 
Laki...
Una ushahidi?

Bila ya ushahidi hatuwezi kutumia taarifa hii.
 
ina maana habari za Chief Mareale kwenda UNO kudai uhuru wa Chagaland na kutaka kujitenga na Tanganyika huna? basi hujui vizuri historia ya nchi hii
Laki...
Hayo nayajua nisiyojua ni kama Chief Marealle alitaka kujitenga.

Ndiyo nikakuomba ushahidi.
 
Mzee wetu Mohamed Said najua wengi wetu tuna kasumba ya kumpinga mjumbe badala ya ujumbe,wengi tunafikiri kwamba kwa sababu hatukubaliani na mjumbe basi tunaweza kutumia kigezo hicho hicho kukataa ujumbe,jambo ambalo si kweli.

Ujumbe wako naamini uko wazi kwamba kuna mengi tunapaswa kuyafahamu kuhusu historia ya nchi yetu sio kwa sababu ya ubaya ila ni kwa faida ya nchi yetu na vizazi vijavyo.

Najua kwamba historia yetu rasmi inaweza kuwa inakosa baadhi ya madini ambayo wewe unatuambia kwamba umeyafanyia utafiti na yenye vielelezo thatbiti.

Najua pia kwamba sio jambo rahisi kubadili historia rasmi hasa ukilinganisha kwamba mengi ya mambo uliyonayo kimsingi yanaonekana kuwa (errors of omission)mfano kutowataja kwa majina wahusika katika hao wazee wa Dar es Salaam) au kutokuelezea kwa kina mchango wao katika historia ya nchi yetu.

BInafsi nafikiri sasa ni wakati wa wanazuoni kama wewe na wengine wengi kuandika kuhusu historia katika mtazamo tofauti.Cha msingi ni kuhakikisha kwamba katika kufanya utafiti wako usiatafute kuichalenge official historia ispokuwa tu pale ambapo kuna reliable facts ambazo zinaweza kusaidia zaidi watu kuelewa historia yetu bila kuwa upotoshaji,uongo au chuki.

Biinafsi naamini hio ndio njia muafaka katika kuhakikisha kwamba historia ya nchi yetu inakuwa tajiri.Haijalishi hata tukiwa na aina sita za historia ya nchi yetu cha muhimu ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na utajiri wa taarifa utakaowezesha vizazi vijavyovyo kufurahi urithi huu wa historia.
Changamoto tunayokumbana nayo kwenye taarifa za Mzee Said hata sisi tusio na unguli kwenye mambo ya historia ni baadhi ya mambo yanayotushinda kuunganisha dots.

Yaani kama ni filamu basi Muandishi anamtambulisha Muhusika Mkuu katikati (kwenye act two), yaani pale Mwanzo (act one) anatuonyesha Wahusika wengine kabisa wakipambana kisha kwenye act two ndio anatokea Muhusika Mkuu na kukabidhiwa kila kitu, na kama miujiza mwishoni mwa filamu (act three) tunamuona Muhusika Mkuu akihitimisha kazi/jukumu alilopewa.

Ni nani atakubaliana na filamu ya aina hiyo?. Muhusika Mkuu ni lazima tumuone kuanzia kwenye act one na tumuone ana nini maalumu kushinda wengine kilichopelekea Wanakijiji/jamii yake kumpa jukumu la wanachohitaji.

Sasa Muandishi huyu ni kama anatuonyesha Wanakijiji wamempeleka Mwanakijiji Mwenzao kwa Mfalme na kumwambia "tumempata Mtu atakayetusaidia lile jambo letu" na Mfalme akiwauliza mmempata vipi? wao wanasema "tumekutana naye tu njiani anapita"

Kwa mfano kwenye filamu za Kichina basi kwenye act one utamuona Muhusika Mkuu akionyesha umaalumu wake sambamba na mazoezi makali ya Kung fu, labda anavyotatua changamoto fulani n.k...kwa kifupi lazima kuwe na kitakachowavuta Wanakijiji kumpata Muhusika Mkuu (Main Character) miongoni mwa Wanakijiji wengine kabla ya kupewa jukumu na jamii husika.
 
May Day,

Mimi ni mpenzi wa movies mfano ulionitolea mimi na nitakushangaza.

Nyumbani katika 1960s tulikuwa na projector 16mm tukiangalia silent films za Charlie Chaplin.

Pili nimemsoma Shakespeare kwa urefu tu sasa uliponitolea mfano wa Act na Scene umenirejesha udogoni.

Umenifurahisha sana.

Mwalimu Nyerere ni Mark Anthony wangu katika, "Julius Caesar. "

Msikilize Mwalimu hapo chini hii kanitumia msòmaji mmoja bila shaka anataka kunisaidia kujibu maswali yenu;

"Mimi nimeanza siasa na Wazee wa Dar es Salaam. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni hadi Chuo Kikuu nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ni siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda ili kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda kijijini Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA?Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana cha matatizo matatizo .

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua kuwa Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kubadilisha katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa shabaha ya kuleta na kupigania uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilishapendekezwa na akina Abdulwahd Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Ally na Abass Sykes (mdogo zake), Dosa Aziz ila waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.
Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu.
Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?
Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.
Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.
Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.
Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.
Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!
Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.
Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.
Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.

Melezo haya yalitolewa na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1985 baada ya kung'atuka madarakani .
 
May Day,

Mimi ni mpenzi wa movies mfano ulionitolea mimi na nitakushangaza.

Nyumbani katika 1960s tulikuwa na projector 16mm tukiangalia silent films za Charlie Chaplin.

Pili nimemsoma Shakespeare kwa urefu tu sasa uliponitolea mfano wa Act na Scene umenirejesha udogoni.

Umenifurahisha sana.

Mwalimu Nyerere ni Mark Anthony wangu katika, "Julius Caesar. "

Msikilize Mwalimu hapo chini hii kanitumia msòm00aji mmoja bila shaka anataka kunisaidia kujibu maswali yenu;

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu. Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Sasa Mzee said hii ndio mimi nimekuwa naitafuta kwenye rekodi zangu, ndio maana nimewahi kusema hapa kwamba kuna mambo nayatafuta lakini nimeyapoteza(kutokana na ku format computer) na ndio maana nimeshawahi kukutajia baadhi ya mambo akiwemo huyo Mzee Mwangosi n.k.

Majibu mengi yapo humu ya yanapishana na baadhi ya taarifa zako unazosema umezitoa kwenye nyaraka za Mzee Abdul Sykes.

Mimi nilisema Mwalimu alitaka kuanzisha Chama, ila kumbe walishaanzisha ila kwa ushauri kutoka waliopo Dar akashauriwa aachane nacho afungue matawi.

Hizi sote nilikuwa nazo ila kwa bahati mbaya kukatokea mkanganyiko nikazipoteza baadhi, na kusitafuta nitahitaji muda wa kutosha.
 
Hotuba hii ya Nyerere inajibu vipi tuhuma dhidi yake kwamba amepindisha na kuficha historia ya ukombozi Tanzania?
 
Laki...
Hayo nayajua nisiyojua ni kama Chief Marealle alitaka kujitenga.

Ndiyo nikakuomba ushahidi.
kitendo cha Chief Mareale kudal uhuru wa ka eneo kadogo ndani ya Tanganyika ndio kutaka kujitenga huko , au wewe unaelewaje kuhusu hili? Chief Mareale angekubaliwa kupewa uhuru na UN wakati Tanganyika bado haijapata uhuru hapo moja kwa moja angekuwa amejitenga na Tanganyika
 
Laki...
Hayo nayajua nisiyojua ni kama Chief Marealle alitaka kujitenga.

Ndiyo nikakuomba ushahidi.
kitendo cha Chief Mareale kudal uhuru wa ka eneo kadogo ndani ya Tanganyika ndio kutaka kujitenga huko , au wewe unaelewaje kuhusu hili? Chief Mareale angekubaliwa kupewa uhuru na UN wakati Tanganyika bado haijapata uhuru hapo moja kwa moja angekuwa amejitenga na Tanganyika
 
Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Nimewahi kuandika humu kuhusu "role" ya Wazee wetu wale, kwa sehemu kubwa ilikuwa hizo "Dua ya asili" na Mwalimu ndio aliwaonyesha kuwa inahitajika zaidi ya Dua.

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kumbe Mwalimu alikuwa na mawasiliano na Watu/Wanaharakati wa Dar, ila sio kina Sykes.

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!
Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Nadhani unaiona role ya "Wazee wetu".

habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Kumbe tangu akiwa Makerere Mwalimu alifuatilia kinachoendelea Dar Es Salaam?

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.
Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nadhani hapa unaiona nafasi na mchango wa "Wazee" wetu, ni zaidi ya kuwafikiria tu kina Sykes na ndiguze.
 
Laki . ..
Mimi sijasoma popote kuwa Chief Marealle alidai uhuru wa Wachagga ndiyo nakuomba kama una ushahidi unipatie.
 
Mimi siwezi kufanya ubishi na wewe kuhusu Dar es Salaam na watu wake.

La unapenda kuamini kuwa Nyerere akijuana na watu wengine hapa mjini ila si Abdul Sykes hapana tabu amini.

Hii ni nchi huru unaweza hata kuamini kigongo kuwa mungu wako na hakuna wa kukubughudhi itakuwa hili la Nyerere na Abdul Sykes?

Ila jiulize hao watu watakuwa nani katika TAA maana wote mimi nawajua ingawa nilikuwa mdogo.

Mbona alipofika Dar es Salaam Nyerere hakuwatafuta watu hao akamtafuta Abdul tena kwa kupelekwa kwake na Kasella Bantu?

Amini upendavyo mimi sina tatizo nimeiandika historia ya TANU kadri ya uwezo wangu.

Furaha yangu ni kama hivi ninavyoona ilivyokusisimueni na tuko hapa tunaijadili historia hii.

Haya ndiyo mafanikio yangu.
Alhamdulillah.
 
Sasa Mzee said hii ndio mimi nimekuwa naitafuta kwenye rekodi zangu, ndio maana nimewahi kusema hapa kwamba kuna mambo nayatafuta lakini nimeyapoteza(kutokana na ku format computer) na ndio maana nimeshawahi kukutajia baadhi ya mambo akiwemo huyo Mzee Mwangosi n.k.

Majibu mengi yapo humu ya yanapishana na baadhi ya taarifa zako unazosema umezitoa kwenye nyaraka za Mzee Abdul Sykes.

Mimi nilisema Mwalimu alitaka kuanzisha Chama, ila kumbe walishaanzisha ila kwa ushauri kutoka waliopo Dar akashauriwa aachane nacho afungue matawi.

Hizi sote nilikuwa nazo ila kwa bahati mbaya kukatokea mkanganyiko nikazipoteza baadhi, na kusitafuta nitahitaji muda wa kutosha.
May Day,
Abdul 1950 alikuwa na miaka 26 sasa ukimwita "mzee," unapoteza taswira ya historia yote ya wakati ule na ni katika umri huu ndipo alipokutana na Jomo Kenyatta katika mkutano wa siri Nairobi wa kuunganisha harakati za TAA na KAU .

Haya mliyajua?

Unategemea Nyerere aeleze haya ilhali hajaingia katika uongozi wa TAA Dar es Salaam?

Nyerere hakuna ajuaye kama Abdul alipata kumweleza historia yake na ya baba yake katika TAA.

Yapo mengi sana.
 
Sidhani kama nimewahi kumtaja Abdul kama Mzee kwani naelewa vema kuwa Mwalimu hakumkuta Abdul akiwa Mzee...kuna mahali umeninukuu vibaya Mzee Said.

Nilipoweka red, labda ndio maana Abdul aliiga jina la KANU akataka na huku iwepo TANU, ingawa kama sikosei hata Mwalimu alihoji/tahadharisha wasije kufananishwa sana na KANU, kabla ya hatimaye kukubaliana tu TAA iwe TANU...hili ndio nimesikia leo lakini angalau naweza kuunganisha dots.

Ila bado hapo sijaona hoja inayobadilisha "cocern" ya wengi kuhusu historia kupinda pinda kwa taarifa zako kuhusu harakati nzima za uhuru.
 
Mbona alipofika Dar es Salaam Nyerere hakuwatafuta watu hao akamtafuta Abdul tena kwa kupelekwa kwake na Kasella Bantu?

Awali mwenyewe umeweka bandiko hapa namna Mwalimu alivyopata taarifa za TAA tangu akiwa Makerere, (ingawa hiyo yote mimi nilikuwa ninayo kwenye hifadhi zangu), pia kumbuka Mwalimu alitaka kujua ni nani viongozi wa TAA, sasa vipi ishangaze kama alitaka apelekwe kwa huyo Katibu wa TAA baada ya yeye kuwepo Dar yalipo makao makuu ya hiyo TAA?

Sikuelewi hapo unapohoji ni kwa nini Mwalimu hakuwatafuta wengine, wengine kina nani? na ni nani wa kukwambia kama Mwalimu alifahamiana na wengine wengi baada ya kufika Dar ili hali wewe una rejea zaidi kwenye nyaraka za Abdul?

Hivi kwa kaliba ya Mwalimu kweli alikuwa Mtu wa kukaa ndani na kusubiri kushikwa mkono kutambulishwa kwa Watu? umuhimu wa Abdul ni kwa ajili ya TAA.

Ila jiulize hao watu watakuwa nani katika TAA maana wote mimi nawajua ingawa nilikuwa mdogo.

Sidhani kama ni sahihi kudhani kama TAA ndio ilikuwa ndio Dar Es Salaam na wakazi wake wote, TAA ilikuwa ni chama/kikundi tu na Dar Es Salaam ilikuwepo bado Mzee Said.
 
Hao wengi wanaijua historia ya baba yake Abdul vipi na lini aliasisi African Association?

Nyie wote mliopo hapa hakuna aliyeijua hiu historia hadi nilipoiandika na naamini wengi hamjasoma kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kitabu hiki kina ibra kubwa kila aliyekisoma kimemvuruga akili.

Mwaka 1988 Africa Events ilichapa makala yangu inayoeleza historia hii basi gazeti lote lilikusanywa.

Unalijua hili?

Abdul kakusudia kuunda TANU akiwa Kalieni Camp kitingoji kidogo nje ya Bombay wakati WW II imemalizika na askari wa KAR wanasubiri kurejeshwa makwao mwaka wa 1945.

KANU imeundwa 1960 na TANU 1954.
Sasa nani kamgeza nani?

Siku zote nikimsikitikia Kleist kwa kutonipa idhini ya kufungua shajara za baba yake nikazisoma huenda kungekuwa na kitu katika ule mkutano wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta na kundi lake la Kapenguria Six- Bildad Kaggia, Peter Mbiu Koinange, Kung'u Karumba, Achieng Aneko na Paul Ngei.

Nyinyi tatizo lenu ni lile la "denial," hii ni "syndrome," inayomkuta mtu katika mshtuko.

Mliaminishwa historia siyo.

Ndiyo maana wajuzi wa historia ya Africa walipokisoma kitabu changu waliniita kwao na wakanitia katika miradi miwili na kazi zangu niliziandika zikachapwa na Oxford University Press Nairobi na Oxford University Press New York.

Hapa nyumbani tunabilingishana huu mwaka wa 9 tunatishwa na ukweli tunamtwisha Mwalimu Nyerere mzigo usio wake.
 
Mbona alipofika Dar es Salaam Nyerere hakuwatafuta watu hao akamtafuta Abdul tena kwa kupelekwa kwake na Kasella Bantu?

Awali mwenyewe umeweka bandiko hapa namna Mwalimu alivyopata taarifa za TAA tangu akiwa Makerere, (ingawa hiyo yote mimi nilikuwa ninayo kwenye hifadhi zangu), pia kumbuka Mwalimu alitaka kujua ni nani viongozi wa TAA, sasa vipi ishangaze kama alitaka apelekwe kwa huyo Katibu wa TAA baada ya yeye kuwepo Dar yalipo makao makuu ya hiyo TAA?

Sikuelewi hapo unapohoji ni kwa nini Mwalimu hakuwatafuta wengine, wengine kina nani? na ni nani wa kukwambia kama Mwalimu alifahamiana na wengine wengi baada ya kufika Dar ili hali wewe una rejea zaidi kwenye nyaraka za Abdul?

Hivi kwa kaliba ya Mwalimu kweli alikuwa Mtu wa kukaa ndani na kusubiri kushikwa mkono kutambulishwa kwa Watu? umuhimu wa Abdul ni kwa ajili ya TAA.

Ila jiulize hao watu watakuwa nani katika TAA maana wote mimi nawajua ingawa nilikuwa mdogo.

Sidhani kama ni sahihi kudhani kama TAA ndio ilikuwa ndio Dar Es Salaam na wakazi wake wote, TAA ilikuwa ni chama/kikundi tu na Dar Es Salaam ilikuwepo bado Mzee Said.
May Day,
Soma hapo chini habari za Mzee Abdulwahid:

Back
Top Bottom