Laki Si Pesa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 5,085
- 9,022
Nyerere ndio alie itransform TAA kutoka chama kisichoeleweka mpaka kuwa chama "serious" cha kupigania uhuru na mpaka katiba ya TAA kaiandika Nyerere. TAA ya Abdul Sykes haikuwa na katiba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyerere ndio alie itransform TAA kutoka chama kisichoeleweka mpaka kuwa chama "serious" cha kupigania uhuru na mpaka katiba ya TAA kaiandika Nyerere. TAA ya Abdul Sykes haikuwa na katiba[/QUOTE]Laki...
Unakusudia katiba ya TAA au ya TANU?
Ungesema hivi ingekuwa vizuri zaidi ungesema, "TAA ya baba yake Abdul," kwa kuwa African Association aliasisi baba yake Kleist Sykes 1929.
Ingekuwa baba kamuachia mwana chama kisichoeleweka na kisichokuwa na katiba.
Hivi ungefikisha ujumbe vizuri zaidi.
Lakini Abdul Sykes wakati alipokuwa kiongozi wa TAA hakuona umuhimu wa kuandika katiba, mpaka alipochaguliwa Nyerere kuwa kiongoz wa TAA ndipo akaandika katiba, hapo ndipo utakapojua Nyerere ndio alikuwa "king maker" wa TAA, ndio alioamsha ari ya kudai uhuru. bila Nyerere TAA isingefika popoteLaki...
Unakusudia katiba ya TAA au ya TANU?
Ungesema hivi ingekuwa vizuri zaidi ungesema, "TAA ya baba yake Abdul," kwa kuwa African Association aliasisi baba yake Kleist Sykes 1929.
Ingekuwa baba kamuachia mwana chama kisichoeleweka na kisichokuwa na katiba.
Hivi ungefikisha ujumbe vizuri zaidi.
Laki...Lakini Abdul Sykes wakati alipokuwa kiongozi wa TAA hakuona umuhimu wa kuandika katiba, mpaka alipochaguliwa Nyerere kuwa kiongoz wa TAA ndipo akaandika katiba, hapo ndipo utakapojua Nyerere ndio alikuwa "king maker" wa TAA, ndio alioamsha ari ya kudai uhuru. bila Nyerere TAA isingefika popote
Kiranga,Hotuba hii ya Nyerere inajibu vipi tuhuma dhidi yake kwamba amepindisha na kuficha historia ya ukombozi Tanzania?
Sasa hujaona hapo amesema Kasela Bantu ndiye aliyempeleka kwa Sykes, na hapo ndipo akapata kujuana na wazee?Kiranga,
Nataabika sana nafsi yangu kupitia maneno hayo hapo chini:
"Mimi nimeanza siasa na Wazee wa Dar es Salaam. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.''
Swali litakuwa aliwajuaje hawa wazee?
Kafika Pugu kawatafuta katika mitaa ya Dar es Salaam?
Wazee wa Dar es Salaam waliokuwa katika siasa wanafahamika na nitawataja wachache.
Kulikuwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Said Chaurembo na John Rupia ambao walikuwa katika TAA Political Subcommittee toka mwaka wa 1950.
Nitawataja wengine ambao hawa walikuwa wanachama shupavu wa TAA na baadhi walihudhuria katika mkutano wa kwanza wa TANU August 1954 - Iddi Faiz Mafungo na ndugu yake Iddi Tosiri na kulikuwa na Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Iddi Tulio, Issa Nasir, Abdallah Shomari, Jumbe Tambaza, Rajab Simba, Boi Singizi, Said Chamwenyewe na wengineo wengi.
Hawa wazee aliwajua vipi hadi akawaamini na wao wakamuamini katika jambo kubwa kama lile la kuunda chama cha siasa na kudai uhuru?
Haiyumkiniki hata kidogo kuwa hakupelekwa na mtu kwenda kujulishwa na kuwa ati alikwenda mwenyewe kama mwanasiasa.
Mambo hayakuwa yanaendeshwa hivyo.
Dar es Salaam ya miaka ile bila wasta hufiki popote na wala huna atakaekupokea.
Sina haja ya kueleza nafasi ya Hamza Mwapachu kwa Mwalimu katika siasa hizi bandiko litakuwa refu sana.
Hao wazee hapo chini wote walikuwa wanachama wa TAA wengine toka enzi za African Association wakati ikiongozwa na Kleist Sykes na wakaja pia kuwa chini ya uongozi wa Abdul Sykes baada ya kifo cha baba yake 1950 na walikuwanae katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na katika mambo mengi ya mjini achilia mbali kuwa wengine walikuwa na biashara zao Kariakoo Market ambako Abdul ndiye alikuwa Market Master.
Baadhi ya wazee hawa Mwalimu Nyerere aliwajua pale Kariakoo Market alipokuwa akienda mara kwa mara kumuona Abdul Sykes na mmoja katika hawa ambao wakajakuwa karibu sana ni Mzee Mshume Kiyate na Shariff Abdallah Attas.
Historia hii inafahamika vyema sana na watu wa Dar es Salaam wa miaka ile.
Kiranga,Sasa hujaona hapo amesema Kasela Bantu ndiye aliyempeleka kwa Sykes, na hapo ndipo akapata kujuana na wazee?
Nashangaa unaandika kama Nyerere anaficha historia hii, wakati mwenyewe kasema haya kwenye hotuba hii?
Kataja mpaka machimbo aliyokuwa akifukizwa na wazee, kwa kisomo cha Quran na cha njia za jadi!
Unategemea Mjamaa mwenye faksafa za collectivism, baada ya kusema "wazee" in a collective fashion, akutajie majina ya mmoja baada ya mwingine?Kiranga,
Hajasema kitu hapo.
Kusema angesema kuwa kamsikia Abdul kutoka kwa Hamza Mwapachu.
Kusema angesema aligombea nafasi ya urais wa TAA dhidi ya Abdul Ukumbi wa Arnautoglo na akashinda Abdul akawa makamo wa Rais.
Kusema angesema kiongozi wa wazee wote wa Dar es Salaam alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na waliompeleka kwake ni Abdul Sykes na Dossa Aziz.
Kusema angesema kwa kuwatambua wazee kwa majina yao.
Hizi dua nadhani Mwalimu anadhani yeye wa kwanza kufanyiwa na wazee.
In Shaa Allah ikitokea fursa nitazieleza dua zote kuanzia ile ya Abdul alipovamiwa ofisini na Town Clerk Mzungu anauza kadi za TANU.
Sakata hili wazee wakuamua kutawaswil kwa Allah Abdul anusurike asifukuzwe kazi.
Kuna kisoma cha Rashid Ali Meli.
Kuna mambo mengi sana sikutaka kuyaandika katika kitabu cha Abdul Sykes.
sina rejea ya katiba ya TAA , nilikuwa naunganisha dots tu, ingawa nina uhakika niko sahihiLaki...
Hii ya kuwa TAA haikuwa na katiba na katiba kaja kuiandika Nyerere wewe hii umeipata wapi?
Ikiwa umesoma mahali tafadhali hebu tupe rejea yake.
Baada ya hayo ndiyo In Shaa Allah tuje kwenye, ''king maker.''
Tusitangulize kwama punda akaja nyuma.
Laki...Mi nadhani kitendo cha Abdul Sykes kuchukua madaraka ya TAA kwa kutumia ubabe na vurugu, hakikuwafurahisha wazee wengi wa TAA, ndio maana kwenye uchaguzi alishindwa kirahisi na Nyerere, Hata huo umakamo wa rais itakuwa alipewa kwa shingo upande ili asimletee vurugu Nyerere, Haiwezekan ushindwe uchaguz halaf upewe cheo kikubwa hivyo
Kiranga,Unategemea Mjamaa mwenye faksafa za collectivism, baada ya kusema "wazee" in a collective fashion, akutajie majina ya mmoja baada ya mwingine?
Hivyo itakuwa ni kinyume na kanuni za Ujamaa zinazoiangalia jamii collectively.
Kashakutajia wawiki watatu hao, jashasema wazee, kwa mujibu wa wajamaa kamaliza hapo.
Mengine mjazie nyie wanahistoria.
Sasa angeandika kitabu cha kuelezea yote uliyoelezea wewe, wewe ungekuwa na justificatiin gani ya kuandika kitabu?
Yani unataka Nyerere aanze kukumbuka majina ya watu wote aliokutana nao mwaka 1952?
Hoja ya kwamba Nyerere amepindisha historia kwa kutotaka watu wajue alikoanzia imezimwa kwa hotuba hii.
Angetaja majina ya wazee mia, ungeweza kuja na majina mengine ya wazee mia ambayo hakuyataja, alijuana na wazee wengi sana, hawezi kumaliza kuwataja wote.
Kitu cha msingi ni kwamba, kakubali kwamba alileleea na wazee wa Dar.
Sasa hapo utasemaje anataka kuficha historia hii?
Laki...sina rejea ya katiba ya TAA , nilikuwa naunganisha dots tu, ingawa nina uhakika niko sahihi
Kiranga,
"Disadvantage," niliyonayo mimi ni kuwa nimeishi ndani ya historia hii kama mtoto wa watu hawa kwa hiyo nayajua mengi ambayo kwa staha sikuweza kuyaandika.
Uhuru ulikuja na changamoto nyingi sana na hasad hazikukosekana.
Hivi hujiulizi mimi nani hadi niaminike kiasi cha kukabidhiwa nyaraka zote za TAA na TANU walizokuwanazo akina Sykes na kuruhusiwa kuandika maisha ya marehemu Abdul Sykes.
Hakuna mtafiti yeyote aliyepata kuziona hizi nyaraka isipokuwa mimi na kuna mengi.
Uhuru ulikuja na fitna na husda.
Hakuna anaetaka Mwalimu akumbuke majina 100.
Aĺitakiwa akumbuke jina moja tu la Mshume Kiyate lingetosha:
![]()
MIONGO MIWILI WAMEKATAA KUBADILISHA JINA LA MTAA WA TANDAMTI KUWA ''MSHUME KIYATE''
Mzee Mshume Kiyate na Baba wa Taifa , 1964 Jina la Mshume Kiyate kwa sasa si geni tena katika historia ya TANU na kupigania uhur...mohamedsaidsalum.blogspot.com
Hiyo picha hapo chini tumepiga mwaka wa 1968 mimi nilikuwa na umri wa miaka 16 na Kleist miaka 18.
Picha hii niko mimi, Kleist Sykes, Abdallah Tambaza, Abdul Mtemvu na Wendo Mwapachu sisi watano familia zetu zote zimeusika kwa karibu sana na historia ya TANU.
Naamini umenielewa.
Kiranga,Mtu akikwambia:-
1. Nyerere ni mjamaa.
2. Wajama ni collectivists, ndiyo maana ya Ujamaa.
3.Alitaka kujenga nchi isiyo na matabaka ya "Hawa wazee wa TANU walioleta Uhuru pamoja na familia zao", na "Hawa vifaranga wengine tumewapa hadhi tu ya uraia wa Tanzania". Alitaka kujenga jamii ya watu sawa.Ndiyo maana hata uchifu aliupiga marufuku. Licha ya yeye kutoka ukoo wa kichifu. Kama alifanikiwa au alishindwa ni suala jingine, hii ndiyo nia yake.
4 Alitaka kwa upande mmoja kuwapa wazee heshima zao, na kutunza historia, ndiyo maana katoa hiyo hotuba, na ndiyo maana shule niliyosoma mimi inaitwa Tambaza.
5. Lakini pia, hakutaka kuwafanya wazee hawa na familia zao wajione wana hadhi ya kipekee nchini Tanzania, kwani, Tanzania ni nchi ya watu sawa.
6. Kawataja wachache, wengine kawataja "wazee" in a collective way, typical of a Mjamaa.
Utapingaje hoja hiyo?
Sijakisoma kitabu, kinapatikana wapi? Kuna wadogo zangu wanakuja kunisalimia mapumziko yao ya Christmas naweza kuwaagizia waninunulie.Kiranga,
Ndugu yangu nataka nikuulize swali umekisoma kitabu cha Abdul Sykes?
Sijakisoma kitabu, kinapatikana wapi? Kuna wadogo zangu wanakuja kunisalimia mapumziko yao ya Christmas naweza kuwaagizia waninunulie.
Maadam sijakisoma, nimekusoma na kukupata wewe muandishi, tujadili mantiki ya hoja nilizoweka hapo juu.
Hujanijibu, japo kwa dondoo tu, wakati nasubiri wadogo zangu waniletee kitabu.
KUSAJILIWA KWA TANU ABDUL NA ALLY SYKES WALIMSUBIRI NYERERE MTAA WA KIPATANyerere ndio alie itransform TAA kutoka chama kisichoeleweka mpaka kuwa chama "serious" cha kupigania uhuru na mpaka katiba ya TAA kaiandika Nyerere. TAA ya Abdul Sykes haikuwa na katiba
Ahadi ni deni, kwa vile nilichoahidi hakina time frame, endelea kusubiria
P