Sultan Tamba na Mussa Banzi Chukueni maua yenu japo bado tunawadai muendelezo wa baadhi ya filamu. Kanumba alichangia kuua soko la filamu

Sultan Tamba na Mussa Banzi Chukueni maua yenu japo bado tunawadai muendelezo wa baadhi ya filamu. Kanumba alichangia kuua soko la filamu

Mleta mada imefafanua vizuri sana , hongera sana.
Naunga mkono hawa ndugu kama wapo wapewe pongezi zao kwa kazi zao, kazi zao zikuwa jana lakini leo na kesho hata kesho kutwa zitabaki kuwa bora kuliko kazi zinazofanywa leo.

Ikiwezekana pia wasitoe kwa upya kipindi hiki, maana ukienda kwenye maduka ya filamu kuipata shumileta ama insyuka itakuwa vigumu sana.

Pia wanaweza kuzitoa kwa mfumo wa sasa tofauti na Cd ama vhf na pia zikawa HD.

Yote kwa yote zilikua ni nyakati zenye filamu nzuri kuliko nyakati zote .
Naaam siku hizi kumejaa wauza sura tu.
 
Cindy na Candy hivi yule demu anaitwa nani,?
Jina la uigizaji anaitwa Mikala ,jina halisi nimelisahau.

Aliwahi kuigiza pia filamu inaitwa The lost twins .Humo ndani amecheza na mama Monalisa (Natasha) (Suzan Lewis) ,Kanumba nk.

BTW huyo dada amefariki kitambo kwa ajali ya gari huko Marekani ila ana mdogo wake wanafanana mno (99%) .

Account ya IG ni hii luckiya07
 
Nasikitika kuwaambia Chawa wa Mayweather leo kaongea ukweli mtupu.
😂😂😂😂😂😂😂😂Mbona umemtaja kiwepesi hivyo.

Anaitwa Floyd Sinclair Joy Money Mayweather Jr ukipenda muite TBE, Face of money, Face of boxing for all the times, number 1 Pound for Pound for all the times, The most accurate puncher , Defensive genius nk
 
Naona umechanganya mambo. Sijajua kama unafahamu kuwa Sultan Tamba ni tofauti na Tamba Arts Group, kundi ambalo lilikuwa chini ya Dk. Maneno Tamba (pale Magomeni). Maneno alikuwa kaka wa Sultani.

Hili kundi la Tamba ndiko alikoanzia Mussa Banzi kabla hajaanzisha kampuni yake. Hivyo mengi uliyoandika kwenye bandiko lako hayana ukweli, na hujui chochote kuhusu film industry...
 
Kihongwe ,hapa Kivuli cha Ibrahimu bwana(bad boy fighter) humu ametumia jina la Desmond kinazikwa rasmi ili huyu dada Nolinda aweze kumtawala kishirikina na aweze kuchuma mali zote na kumfanyia chochote anachotaka .

Attachments

  • 7967b2d4d46b42808732523ae62fd2c9.mp4
    2.2 MB
Nimetoka kuangalia "Mzee wa Busara", Zigi alipata shida kweli. Nairudia sehemu ya pili. Nikimaliza nitatoa mrejesho.

Nimetafuta sana igizo la "Tetemo" ila sijaliona, kama kuna yeyote anayefahamu namna ya kulipata naomba anisaidie.
Tutumie short clip. Sema huyo mzee alikuwa mwanga sana 😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Tamthiliya za zamani mfano kama hiyo tetemo, gharika,taswira nk sidhani kama ni rahisi kupatikana labda uwacheki wahusika akina Christian Mhenga,William Mtitu nk
 
Naona umechanganya mambo. Sijajua kama unafahamu kuwa Sultan Tamba ni tofauti na Tamba Arts Group, kundi ambalo lilikuwa chini ya Dk. Maneno Tamba (pale Magomeni). Maneno alikuwa kaka wa Sultani.

Hili kundi la Tamba ndiko alikoanzia Mussa Banzi kabla hajaanzisha kampuni yake. Hivyo mengi uliyoandika kwenye bandiko lako hayana ukweli, na hujui chochote kuhusu film industry...
Sultan na Maneno ni mtu na kaka yake na walikuwa wanafanya kazi kwa kusaidiana ila mtu ambaye alikuwa ana play part kubwa ni Sultan.

Maneno ameshiriki kuandaa filamu chache sana na hakuna filamu aliyoiyoitoa yeye peke yake bila msaada wa Sultan .
 
Kosa lake ni kukiuka makubaliano na shetani angekuwa hai Hadi leo
Hizo stori za vijiweni hazina uthibitisho wowote.

Walikuwa wanasema Ramsey naye ni freemason na kawaida freemason huwa hawazikani ndio maana Ramsey hakuja kwenye msiba wa Kanumba 😂😂😂😂😂😂😂😂

Achana na wabongo kabisa wajuaji sana.
 
Naona umechanganya mambo. Sijajua kama unafahamu kuwa Sultan Tamba ni tofauti na Tamba Arts Group, kundi ambalo lilikuwa chini ya Dk. Maneno Tamba (pale Magomeni). Maneno alikuwa kaka wa Sultani.

Hili kundi la Tamba ndiko alikoanzia Mussa Banzi kabla hajaanzisha kampuni yake. Hivyo mengi uliyoandika kwenye bandiko lako hayana ukweli, na hujui chochote kuhusu film industry...
sawa leta ya ukweli tukupe sadaka bishop
 
Tamba Arts group walikuwa wanajua kuigiza kweli. Nimependa jinsi ambavyo waigizaji wao ambavyo walikuwa hawaogopi kamera na walijua kuigiza uhusika kwa kiasi kikubwa.

Nipo kuangalia Fungu la kukosa, Riyama kauvaa uhusika sana, Dimoso naye akiigiza kulewa mambo yanakuwa mwake mwake😂😂😂. Kwasasa naendelea na ahadi ya yule mwanamke aliyemgonga Dimoso aliyeahidi kuwajengea nyumba (Mr. and Mrs. Dimoso)
Dah umenikumbusha mbali sana
.Hivi fungu la kukosa ndio ile Riyama anakuwa chizi?

Kwa haraka haraka nakumbuka kuna usaliti ulitokea kama sio Dimoso basi Riyama.

BTW Dimoso nilimuona mara ya mwisho kwenye Insyuka 3 yeye ndiye aliyemconnect Sanjo na mganga ambaye alifanikiwa kumzidi nguvu Nsyuka na kuyeyuka nyuma yake na kwenda kumfunga /kumgongelea msumari kwenye mbuyu.
 
sawa leta ya ukweli tukupe sadaka bishop
Huyo analeta ujuaji mwingi na hana anachokijua.

Nakutolea mfano girlfriend filamu iliyochezwa na T.I.D ,AY,Monalisa,Ndende,Jay Mo,Jafarai, Nina nk , waliunganisha nguvu watu wanne ,Maneno Tamba, Sultan Tamba, mume wa Monalisa ambaye ni mkenya anaitwa George Tyson ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kupata ajali, na kuna mwingine jina limenitoka.

Yote hayo yakifanyika chini ya Tamba Arts group.
 
Back
Top Bottom