Suluhisho la Kudumu la Kero Zote za Muungano, na Dawa ya Kutibu Sumu ya Ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari ni Kuwa na Serikali Moja ya JMT?

Inatakiwa iitishwe kura ya maoni ili wananchi waamue kama wanautaka muungano ama hawautaki. Kama wanautaka muungano,wanataka muungano wa aina gani?
 
Najua hukosoma hesabu hivyo hujui hesabu na mabandiko yako marefu bila point

Kwa summary bila kuchosa wasomaji

Serikari 3 automatically ndo serikali Moja yennye manimbo makubwa mawili, we utaita ni nchi whatever you name it

Chademe wameenda mbali zaidi wamita Kanda

Kwa hiyo chini ya cdm tutakuwa na serikali Moja ya shitikisho yenye Kanda 6 Zanzibar inclusive

Kwa nyie msioojua hesabu ni sawa na kusema serilikali 6 za Kanda + serikali Moja ya shirikisho jumla ni serekali 7
 
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu kwa hoja za kibaguzi za Utanganyika na Uzanzibari, ambapo wiki iliyopita nilisema zimesababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu Muungano wetu Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Kwa wasomaji wapya, wiki iliyopita nilizungumzia kuhusu kauli za kibaguzi za kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, nikazungumzia kuwa zinasababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia, na kuaahidi leo nitaumalizia mjadala huu kwa kuangazia chanzo cha ubaguguzi huu na suluhisho la kudumu la kuutibu ugonjwa huu na kuondoa kabisa kwa kumaliza sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari.

Mada ya leo ni historia fupi ya chanzo cha ubaguzi huu wa Utanganyika na Uzanzibari na suluhisho la kudumu la kumaliza kabsa kero zote za Muungano, na suluhisho la kudumu na dawa ya uhakika ya kutibu kabisa hii sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari, ambayo kiukweli kabisa ni kidonge kichungu kumeza kwa wahafdhina, ila kidoge kichungu ndicho kinachotibu maradhi. Swali hapa ni jee dawa ni kuwa na serikali moja ya JMT?.

Baada ya Muungano, kwa miongo kadhaa, tumekuwa na muungano wenye maelewana mazuri licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa kwenye kero za muungano, ila moto wa Utanganyika na Uzanzibari, uliwashwa na kitendo cha Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu, OIC, wakati Tanzania imejinasibu ni nchi isiyo na dini, secular state.

Wabunge 55 wa Bunge la JMT, wakaunda kundi la G-55 na kuidai serikali ya Tanganyika, ili iendelee kuwa haina dini na kuiruhusu serikali ya Zanzibar kuendelea kuwa mwanachama wa OIC.

Bunge lilipitisha Azimio la kuanzisha serikali ya Tanganyika, jambo ambalo lilimuibua Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuwakemea wabunge, kwa Bunge kukaa kama kamati ya Chama na kuwaeleza mfumo wa serikali tatu sio sera ya CCM, hivyo hoja hiyo ya kuundwa serikali ya Tanganyika, ikafa kifo cha mende, na kuzikwa jumla.

Zanzibar ikalazimishwa kujitoa OIC, na kuahidiwa, serikali ya JMT itajiunga na OIC, kitu ambacho hakikufanyika mpaka leo. Tuko wakati huo, wahafidhina wa Zanzibar wakawa na dukuduku la chini chini kuwa Zanzibar, haikutendewa haki, hivyo wakaanza vuguvugu za kudai Zanzibar yenye mamlaka zaidi.

Aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe, akapewa ushauri wa kisheria na mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado, wakaandaa hati za kisheria kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili, taarifa zikafika kunakohusika, Aboud Jumbe akaitwa Dodoma, akaenda kama rais wa Zanzibar, akarejea kama rais mstaafu na kusindikizwa nyumbani kwake Mji Mwema mpaka Mungu alipomuita, Dourado aliwekwa mahala salama, taarifa iliyotolewa ilisema kumetokea kuchafuka kwa hewa ya kisiasa Zanzibar kulikopelekea Jumbe kujiuzulu urais wa Zanzibar.

Baada ya Rais Nyerere kutoka Bara, alifuatiwa na Rais Mwinyi kutoka Zanzibar, akaja Mkapa kutoka Bara, akitarajiwa anafuatiwa na rais kutoka Zanzibar, hali haikuwa hivyo, akaingia Rais Kikwete, Wazanzibari wakajiona wako marginalized wakakoleza hoja ya Uzanzibari, baada ya Rais Kikwete kufuatiwa na Rais Magufuli kutoka Bara tena, Uzanzibari ukazidi kukolezwa. Akina sisi tuliuliza Je, kunahitajika ‘affirmative action’ ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Mungu akaingilia kati, kukatokea kilichotokea Machi 17, 2021 kwa Rais wa JMT kuwa ni Rais Samia kutoka Zanzibar, hoja za Utanganyika zikaanza kuibuliwa tena na wanasiasa muflis kuanza tena ubaguzi wa kunyoosheana vidole, vya Utanganyika na Uzanzibari.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Rejea za mwandishi kuhusu serikali moja
Huna jipya. Mmebaki kujivunia uccm ila Muungano umewashinda mmebaki kutuandikia makala ndefu za kinafiki. Kinachowashinda kuleta hiyo serikali moja ni Nini?. Shut up Kama hamwezi kufanya Jambo na sio kutuandikia makala ndefu zisizokuwa na maana.
 
Kuna mwamba alisema: waliozoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi. Muungano wa JMT ulisukwa kwa janjajanja nyingi.

Huo muungano hauna kero zozote; ni mbovu, period!

Mtafuteni huyo mwamba, naamini atawapa ushauri wenye suluhisho la uhakika.
 
Haitasaidia.
Ni kweli. Lakini tujiulize. Hivi ni akina nani wanaotaka jambo hili libaki hivi hivi pamoja na kelele zote hizi?. Je, nani ni mnufaika na hili? Tumeambiwa kuwa Jumbe alipotamani kubadi mfumo kwamba walimwita Dodoma akiwa raisi na alirudi akiwa amenyang'anywa uraisi. Je, ccm wananufaikaje na muundo lalamikiwa wa muungano?. Natamani serikali moja, ikishindikana basi serikali tatu.
 
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu kwa hoja za kibaguzi za Utanganyika na Uzanzibari, ambapo wiki iliyopita nilisema zimesababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu Muungano wetu Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Kwa wasomaji wapya, wiki iliyopita nilizungumzia kuhusu kauli za kibaguzi za kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, nikazungumzia kuwa zinasababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia, na kuaahidi leo nitaumalizia mjadala huu kwa kuangazia chanzo cha ubaguguzi huu na suluhisho la kudumu la kuutibu ugonjwa huu na kuondoa kabisa kwa kumaliza sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari.

Mada ya leo ni historia fupi ya chanzo cha ubaguzi huu wa Utanganyika na Uzanzibari na suluhisho la kudumu la kumaliza kabsa kero zote za Muungano, na suluhisho la kudumu na dawa ya uhakika ya kutibu kabisa hii sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari, ambayo kiukweli kabisa ni kidonge kichungu kumeza kwa wahafdhina, ila kidoge kichungu ndicho kinachotibu maradhi. Swali hapa ni jee dawa ni kuwa na serikali moja ya JMT?.

Baada ya Muungano, kwa miongo kadhaa, tumekuwa na muungano wenye maelewana mazuri licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa kwenye kero za muungano, ila moto wa Utanganyika na Uzanzibari, uliwashwa na kitendo cha Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu, OIC, wakati Tanzania imejinasibu ni nchi isiyo na dini, secular state.

Wabunge 55 wa Bunge la JMT, wakaunda kundi la G-55 na kuidai serikali ya Tanganyika, ili iendelee kuwa haina dini na kuiruhusu serikali ya Zanzibar kuendelea kuwa mwanachama wa OIC.

Bunge lilipitisha Azimio la kuanzisha serikali ya Tanganyika, jambo ambalo lilimuibua Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuwakemea wabunge, kwa Bunge kukaa kama kamati ya Chama na kuwaeleza mfumo wa serikali tatu sio sera ya CCM, hivyo hoja hiyo ya kuundwa serikali ya Tanganyika, ikafa kifo cha mende, na kuzikwa jumla.

Zanzibar ikalazimishwa kujitoa OIC, na kuahidiwa, serikali ya JMT itajiunga na OIC, kitu ambacho hakikufanyika mpaka leo. Tuko wakati huo, wahafidhina wa Zanzibar wakawa na dukuduku la chini chini kuwa Zanzibar, haikutendewa haki, hivyo wakaanza vuguvugu za kudai Zanzibar yenye mamlaka zaidi.

Aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe, akapewa ushauri wa kisheria na mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado, wakaandaa hati za kisheria kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili, taarifa zikafika kunakohusika, Aboud Jumbe akaitwa Dodoma, akaenda kama rais wa Zanzibar, akarejea kama rais mstaafu na kusindikizwa nyumbani kwake Mji Mwema mpaka Mungu alipomuita, Dourado aliwekwa mahala salama, taarifa iliyotolewa ilisema kumetokea kuchafuka kwa hewa ya kisiasa Zanzibar kulikopelekea Jumbe kujiuzulu urais wa Zanzibar.

Baada ya Rais Nyerere kutoka Bara, alifuatiwa na Rais Mwinyi kutoka Zanzibar, akaja Mkapa kutoka Bara, akitarajiwa anafuatiwa na rais kutoka Zanzibar, hali haikuwa hivyo, akaingia Rais Kikwete, Wazanzibari wakajiona wako marginalized wakakoleza hoja ya Uzanzibari, baada ya Rais Kikwete kufuatiwa na Rais Magufuli kutoka Bara tena, Uzanzibari ukazidi kukolezwa. Akina sisi tuliuliza Je, kunahitajika ‘affirmative action’ ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Mungu akaingilia kati, kukatokea kilichotokea Machi 17, 2021 kwa Rais wa JMT kuwa ni Rais Samia kutoka Zanzibar, hoja za Utanganyika zikaanza kuibuliwa tena na wanasiasa muflis kuanza tena ubaguzi wa kunyoosheana vidole, vya Utanganyika na Uzanzibari.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Rejea za mwandishi kuhusu serikali moja
Hatuwezi kuulinda muungano kwa 'gharama yoyote '. Muungano unapaswa kuwa kwa ridhaa ya raia wa pande mbili. Hatuwezi kulazimisha muungano eti kwa gharama yoyote hata kama haukubaliki na raia. Njia pekee ya kuthibitisha muungano huu unakubaliwa au haukubaliwi na raia wa pande mbili ni kuitisha kura huru ya maoni kila upande. Tunakumbuka muunga huu ulianzishwa na JK Nyerere na Abeid Karume, na hakukuwa na mchakato wowote wa kupata ridhaa/maoni ya raia wa pande mbili wakati ule.
 
Hiawezekani kuwa na serikali moja ,hapo kwa nature ya binaadamu tumeumbwa na tamaa hakuna atakayependa kuucha urais.

Kuwe na serikali tatu.

Serikali ya Muungano ioperate kote kote iwe na ofisi zanzibar na ofisi bara.

Bara na zanzibar kusiwe na rais bali kuwe na Kiongozi mkuu wa Tanganyika na Kiongozi mkuu wa Zanzibar ,wote wanareport kwa rais wa JMT.

Kiongozi mkuu wa Zanzibar anasimamia mambo ya znz na yanayohusu muungano znz na kiongozi mkuu wa tanganyika anasimamia tanganyika na mambo ya muungano Tanganyika.
 
Bado hilo linaweza lisiwe suluhisho la kudumu. Kwanini?
Wazanzibar wengi hatuko tayari na mfumo wa serikali moja, kwa kuwa serikali moja itaimeza Zanzibar na visiwa vya Unguja na Pemba vitageuzwa na kuwa wilaya mbili (sio hata mikoa) ndani ya muungano wa Tanzania. Hilo jambo hatulitaki kulisikia kwa kuwa mbali na kuua utambulisho wetu wa kizanzibar, linapingana na katiba ya Zanzibar na mwisho litaididimiza Zanzibar kiuchumi kwa kuwa Zanzibar itakosa upekee wake na kuwa sawa na wilaya za huko Tanganyika mfano wa Namtumbo, Kasulu, Tandahimba nk.

Nadhani suluhisho ni kuwa na serikali tatu (Zanzibar, Tanganyika, Tanzania) kwa sababu ndio muundo unaokubalika na pande zote mbili za muungano huku ukiwa na uwezo wa kuainisha vyema maslahi ya kila upande kwa wazi na usawa.
Yaan huyu mtumwa uzanzibari ulianza baada ya sultan kabla ya hapo ulikua muafrica tu
 
Back
Top Bottom