Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Kwanza kabisa mimi sio Mtaalamu na baada ya kuangalia kwa haraka matakwa ya pande tofauti nimeona ni vigumu sana kwa upande mmoja kukubaliana na matakwa ya upande mwingine kutokana na usalama wao na kutokuaminiana; Hivyo Suluhisho pekee ni hapo katikati kuwepo na nchi ya hao waliomo. Kwa kufahamu vizuri ugumu wa mgogoro huu ni vema ukauangalia katika mtizamo (perspective) ya watu Husika;
Watutsi ambao ni Wakongo (Ambao Watu wa Congo wanasema ni Wanyarwanda na warudi Kwao):
Nchi ya Congo
Nchi ya Rwanda:
Kumbuka nchi ya Rwanda Kagame alivyochukua nchi kuna wale watu ambao inasemekana ndio walihusika na mauaji ya Kimbari pamoja na Waliokuwa ndio wanaongoza nchi walikimbilia Congo na kupokelewa Congo, na Ufaransa pamoja na Mobutu kuwafundisha zaidi ili waweze kurudi Rwanda na kumpindua Kagame; Ingawa Kagame na yeye kuona hivyo akatumia Watutsi waliopo Congo kuwafundisha ili kuweza kuwakabili hao anaowaona ni waasi (hivyo matatizo ya Rwanda ni kama yakahamia Congo).
Kwahio ni ngumu kwa Kagame kuona kuna Watutsi wanaonyanyaswa Congo wakati yeye aliingia kwenye madaraka kwa kuonyesha kwamba anamaliza manyanyaso hayo; Na Tukisema hao Watutsi warudi Rwanda, je warudi wapi ukizingatia wengine wapo hapo tangia enzi na enzi ? Pia Kagame lazima jicho lake litakuwa Congo sababu anaona kuna uwezekano wa kuvamiwa kutokea Congo
Uganda:
Uganda pia na yeye yupo macho sababu kunaweza kutokea waasi wowote kutokea Congo kuleta machafuko Uganda ukizingatia community hizi kuna watu ambao walikimbia kutoka Congo kwenda Uganda na wanaweza kurudi wakati wowote na vice versa
Tanzania:
Shida yoyote ya jirani yako pia ni ya kwako mfarakano wowote utakaotokea huko lazima na wewe utakufikia; Pia kuna ndugu zetu Wanyarwanda na Warundi wengi zaidi ambao walikuja huko baada ya shida za huko kwao, shida zinazotokea huko huenda zikaanza kupelekea hawa ndugu zetu kutengwa na kunyanyaswa kama vile watusi wa Congo wanavyoonekana ni matatizo na waleta shida.
Hitimisho
Hitimisho pekee na la kudumu, ni hawa watu waliopo sasa hapo North Kivu (Jamii zote) waweze kupata nchi yao hapo hapo na nchi zote za maziwa makuu na kwa kushirikiana zinaweza zikawa na Base ya kuangalia Amani hapo, na kuhakikisha vinatokomeza vikundi vyote vya Kuasi (Magaidi hata kama wanajiita Freedom Fighters) na vya aina yoyote kwa kuwa assimiliate katika nchi yao hii mpya. Na kuhakikisha hakuna masalia ambayo yanaweza kuanzia hapo na kuleta shida yoyote au kutishia Amani katika nchi Jirani.
Suala hili inabidi sisi kama Waafrika tusaidiane kulimaliza na kabla ya Afrika sisi majirani kwanza (Maziwa Makuu)

- Kumbuka hawa kabla ya wakoloni kuweka mipaka yao baadhi yao walikuwepo hapo, kwahio kuwepo kwao Congo sasa hivi sio kwamba wote walikuja bali walijikuta wamewekwa Congo; Kwahio hawa kwa mtizamo wao ni Wakongo
- Hawa watu wananyanyaswa kwamba sio Wakongo na warudi kwao, Sasa kwao wapi sababu ukiwafukuza je unawafukuza na ardhi ?
- Hawa watu wanachotaka wao ni kuwa na haki sawa kama wakongo na uwezo wa kupiga kura n.k, jambo ambalo wakongo hawataki kuwapa (na wana hoja sababu kwa macho yao hawa ni mamluki)
- Hao askari wa M23 nao wanataka wawe assimilited kwenye jeshi la Congo (jambo ambalo sidhani kama Congo watakubali)
Nchi ya Congo
- Wao wanaona hawa sio raia wala wakongo na kwao wanaweza kuwa hatari kwa usalama wa nchi kama mapandikizi, na pia wanaona wanatumika kama nyenzo ya kuwaibia na pia kikundi cha M23 ambacho kinasema kinawalinda watutsi hao kwa Congo kundi hili ni magaidi.
- Kwa Rais wa Congo kukubali hawa watu waingizwe nchini na kupewa kila haki hata yeye akikubali kuna watu wa Congo ambao watamuona kama msaliti, na vilevile kwa macho yake hii ni hatari ya kuleta mamluki (watu ambao wewe unaona sio Watu wako katika nchi yako).
- Congo wanaona M23 ni kama nyenzo ya Rwanda kuwaingilia na ukizingatia hata Kabila alivyochukua nchi alipata msaada wa hawa watu na wakitokea Uganda na kumuondoa Mobutu utaona kwamba Rais wa Congo ana hoja za msingi za kutokukubaliana na assimilation ya hawa watu Congo.