Suluhisho la Kudumu la Mgogoro wa Maziwa Makuu (Rwanda, Congo et al) ni kutenga na kupata nchi ya hao waliopo hapo sasa (North Kivu)

Ttzo alilianzisha Rwanda miaka 1990s maana hao watutsi wapo hapo DRC miaka na miaka ila hawajawai baguliwa kwann waje waseme wanabaguliwa miaka ya 1990s
 
fuatilia kinachoendelea DRC , watutso waliopewa uraia ndan ya DRC wanatumika kufanikisha agenda mbovu za maadui wa DRC , sio kwel kwamb serikali ya DRC inawatenga ila tabia zao hata ww ungefanya kama afanyavyo DRC
 
Hivi tukisema leo wahindi wote na waarabu na hao wote uliowataja sio watanzania by virtue ya tamaduni zao na ongea yao na vinasaba zaidi vya watu wa huko arabuni au India tutakuwa tumewatendea Haki ? Sababu hicho ndicho kilichopo huko.
hz story zinatengenezwa na Rwanda. Je kuna mhutu ndani ya Jeshi au serikali ya Rwanda kweny vyeo vya juu ? ika wapo watutsi kwenye vyeo vya juu huko DRC , Lawama za Rwanda anapewa DRC , walifikia makubaliano ila Rwanda ba M23( watutsi) ndo waliyavunja makusudi wakilenga kuendeleza vita na sio amani
 
hv watutsi wananyimwa haki ipi iwapo hata vyeo vya juu walishapewa humo DRC , rejea mkuu wa majeshiUkraine aliyeongoza majeshi ya nchi mbili , DRC na Rwanda , Kagame amewin akili za wabantu maana wabantu( wahutu,) wavivu kufanya utafiti , et watutsi wanyimwa haki zao kama zpi?
 
..hatua ya kwanza ni pande zote kuweka silaha zao chini.
Hii ilishatokea walishaweka na baadae wakazichukua.., issue ni kwamba why should they pick them in the first place; ni kwamba kuna loopholes au sababu za wao kuweza kufanya hivyo na mazingira ni rafiki kwa watu kufanya hivyo, hivi unajua hata kwa anayevuma ni M23 ila kuna vikundi vya Kuasi vingi sana ?
..hatua ya pili ni Watutsi kutambuliwa kuwa wao ni raia wa DRC.
Is that as easy as you are saying ? Yaani watusi hawa watambulike mpaka Kinshasha huko ambako watu wanawaona (with or without reason) kwamba ni mapandikizi na wasaliti ? Ingawa sidhani kama tumefika huko ila hali ikiendelea hivyo ni kama hapo baadae tushauri baadhi ya wapalistina (ambao walikuwepo Israel ya sasa iliyojitwalia eneo) kwamba watambulike mpaka Israel (will be good theoretically) ila practically ni kama kuchanganya mafuta na maji.
..Watutsi nao wawe loyal kwa Congo na kuacha kujichukulia kama Wanyarwanda.
Nadhani wao wanasema ni Wacongo (ambao ni wacongo na sio wakimbizi waliojichanganya, lakini how can you distinguish kama hakuna systematic checks) kwahio hata kama watusi wakiwa royal vipi lazima kuna watakaowaona hawafai (case in point kipindi cha Mobutu kuna watu walianza kuwafukuza hawa watusi na hata Bungeni kusema Banyarwanda sio Wacongo..., sasa kwa issue hio hata wewe unaweza kuwa loyal 100 percent kwa nchi ambayo wanakuona wewe sio mwenzao na anytime wanaweza kusema ondoka ?!!!
..Rwanda ihakikishiwe ulinzi kwa vikosi neutral visivyotokana na majirani wa Rwanda na DRC kulinda mpaka wa nchi hizo.
Neutral from where and who is going to pay for them (sababu people don't stay neutral and sometimes they have their agendas) Congo hawakuwaamini /vikosi vya East Africa na baadae akaamia SADC kwahio kwa hawa watu ambao mwisho wa siku its all about resources usitegemee watu kubakia Neutral na ukizingatia haya ma taasisi kujumlisha hata OAU yalishabaki kama mapambo yasiyo na meno
..DRC iache kuwasaidia Fdlr, na Rwanda iache kuwasaidia M23.
Bila kuondoa mzizi wa fitina watakuwa hawaachi bali wana pause..., ndio maana nikasema hii sehemu mpakani ingekuwa buffer zote isiyofungamana na upande wowote huyu akija apate kipigo na yule akipita vilevile...
 
..Congo tayari iko decentralized.

..wana mfumo wa utawala wa majimbo.
Hayo majimbo yana meno au any military power ? Issue sio kwenye vitabu vinasema nini bali issue is if it works...
..hivi m23 haiwezi kuwa chama cha siasa?
Kwahio wawape Kibali chama ambacho ni cha wachache (yaani kinachosema kipo pale kusimamia haki / kulinda watu wa aina fulani)? Unaona hio ni sawa.., Binafsi naona hii M23 hata ingekuwa disintegrated na isiwepo kabisa Chama chochote au Kundi lolote ambalo lipo pale kutetea watu wa aina fulani pekee na sio watu wote, kwangu mimi hilo ni tatizo kuliko solution ambayo inaweza kugharimu zaidi huko mbeleni
..Wacongo wahimizwe kutafuta political solution, na sio military solution, au kuigawa DRC vipande.
Na ndicho kinachofanyika hapa sidhani kama kuna mtu anasema hivi vita viendelee (unless anafaidika binafsi na hawatakii mema raia) kitu ambacho kina ukweli na waasi wengi ndio motive yao.., Achana na Congo tu mimi ningependa hata Afrika nzima iwe moja ila ndio hivyo kama watu waliopo ni maji na mafuta na they can not see reason (naona maana ya msemo wa kwamba unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni lakini ni vigumu kumlazimisha kunywa maji)
..Na sio kwamba DRC ni kubwa mno, na haitawaliki.
What do you call this mkuu..., Na ukiondoa kipindi cha Mobutu ambapo alikuwa na military power na kujaribu kuwapa wacongo identity what has been happening you can not call it systematic government
..Maeneo yote ya DRC yana amani isipokuwa North Kivu ambako Rwanda inafadhili maasi.
Kwahio Rwanda kufadhili hayo maasi (M23) ingawa kuna vikundi vya waasi zaidi ya kimoja (ni kwamba Congo hii itarudi enzi za nani Mobutu au pre Patrice Lumumba ambapo ilikuwa imejigawa kila kona ? Na kwanini Rwanda inaweza kufadhili hao waasi (the main reason) na kwanini tusiondoe hio reason ?

Things are never Black or White there are a lot of Grey Areas
 
kwan huu mgogoro si ulianza miaka 1990s je kabla ya hapo walikuwa wanabaguliwa pia maana hawakuwa na agenda zozote , huez baguliwa kama ww ni mwenyej , kuna namna hao ni wageni
There were no transitional provisions adopted on nationality when Congo obtained independence from Belgium in 1960, but Article 6 of the ‘Luluabourg’ Constitution of 1964—the first constitution of the new state and the first legal determination of nationality—declared to be Congolese ‘all persons one of whose ancestors was or had been a member of a tribe or part of a tribe established in the Congo before 18 October 1908’, the date on which the Belgian Congo was created. This position was confirmed in the nationality law of 18 September 1965. Arguments that the presence of someRwandophones on Congolese territory before 1908 meant that all could claim citizenship were not accepted.

A decree-law adopted in 1971 specifically addressed their situation, providing that people originating from Rwanda or Burundi (only) and established in Congo on 30 June 1960 had Congolese nationality. In 1972, a general nationality law promulgated soon after the change of the country’s name to Zaire moved the date of arrival for this group back ten years, to 1 January 1950.
In 1981, after the fall from favour of the Banyarwanda adviser to President Joseph-Désiré Mobutu who had pushed these changes, a new code of nationality was adopted by the Zairian parliament which established dramatically more restrictive rules. It provided for attribution of nationality to ‘any person one of whose ancestors was a member of one of those tribes established in the territory of the Republic of Zaire as defined by its frontiers of 1 August 1885’, the date on which the borders of the Congo Free State were officially recognised.

Under the rule of Mobutu Sese Seko, the Banyarwanda were not considered citizens of Congo despite many of them having lived in Kivu since long before Congoan independence, and even colonization. In 1972, they were granted citizenship rights. However, this was rescinded in 1981, though it was never made into law. In practice, they have had no voting rights and no representation. Since the takeover of Congo by Laurent Kabila in May 1997, there has been no formal change of policy. As of 2003, the issue of citizenship for the Bayarwnada has been left to the Transitional Government, created in June of 2003.
 
Ttzo alilianzisha Rwanda miaka 1990s maana hao watutsi wapo hapo DRC miaka na miaka ila hawajawai baguliwa kwann waje waseme wanabaguliwa miaka ya 1990s
Hivi unajua kuna kipindi enzi za Mobutu Governor wa hapo alianza kuleta siasa za ubaguzi na watusi kuanza kuchomewa moto nyumba zao ? Ni hivi hizi tensions zilikuwepo zilikuwa zinahitaji spark tu ili moto uweze kuwaka na moto huo uliwaka baada ya wakimbizi kuongezeka na kuendelea kupata kasi baada ya France na Mobutu kuwapokea wale so called waliosababisha genocide Rwanda na kuwapa msaada na Kagame na yeye akafanya vice versa kuwafundisha wakimbizi waliopo Congo (in short kuyapeleka matatizo ya Rwanda Congo)
 
fuatilia kinachoendelea DRC , watutso waliopewa uraia ndan ya DRC wanatumika kufanikisha agenda mbovu za maadui wa DRC ,
Nani kabisha hili ? Na kama ni hivyo huoni kwamba ni vigumu kwa hawa Watusi ambao ni Wacongo ni vigumu kupewa haki zao kama Wacongo ? Kwahio what gives au unashauri nini ? (Wafukuzwe ? Je wafukuzwe na ardhi au wapelekwe wapi) Au unaona waangamizwe kabisa katika uso wa Dunia ?
sio kwel kwamb serikali ya DRC inawatenga ila tabia zao hata ww ungefanya kama afanyavyo DRC
Hapo unajicontradict mwenyewe kwamba hawatengwi ila wanatengwa sababu ya tabia zao hence wanatengwa ila Congo inafanya hata mimi ambacho ningefanya ?

Hivi sio Kabila aliowatumia (achana na hawa Watusi ambao ni Wacongo) bali Watusi ambao ni wa Rwanda ikiwemo James Kabarebe kuweza kufanikisha kuchukua nchi alafu akawabwaga ?; Mobutu pia aliwatumia baadhi kwa faida zake mwenyewe; Ila kwa kuwatumia hawa hakuondoi ukweli kwamba kuna Watusi ambao ni Wacongo...

Na hapo Kivu sio Watusi pekee kuna makabila mengine ambayo yanaendelea kupata shida kutokana na incompetent na tamaa ya madaraka ya watu wanaotumia hizi chaos kama ladder ya kupata madaraka...
 
hz story zinatengenezwa na Rwanda. Je kuna mhutu ndani ya Jeshi au serikali ya Rwanda kweny vyeo vya juu ? ika wapo watutsi kwenye vyeo vya juu huko DRC ,
Hivi mkuu hata unafuatilia Historia ? Hivi unajua Kagame (mkimbizi) alikuja kwa kupigana na jeshi lake ili kuondoa jeshi ambalo defacto objectives ilikuwa ni kuwaangamiza watusi katika uso wa dunia ? Hivi unajua katika hii transition na kilichofanyika mpaka hapa its like a miracle sababu kilichofanywa under those 100 days ilikuwa ni jambo la aibu kutokea ? Now that is another case and Rwandese problem and they need to sort it out themselves mimi sina mandate wala facts za kuweza kusema wafanye hiki au kile (ila hawa Wahutu kwa walichofanya na ukizingatia wapo wengi I think they can wait and take a rough with a smooth kujenga nchi yao)
Lawama za Rwanda anapewa DRC , walifikia makubaliano ila Rwanda ba M23( watutsi) ndo waliyavunja makusudi wakilenga kuendeleza vita na sio amani
Hivi hapa nani anatetea M23 au kikundi chochote kila cha Waasi ? Wote hawa ni wabaya and are after power ila kupigana huku kwa hawa wote kunawaletea shida raia.., na hata Kagame akifa leo au leo wakiweka silaha zao wote chini bado kuna mzizi wa fitina ambao anytime ikija spark ni kuwasha moto....
 
suluhisho ni kuchukua nchi yote na kuisuka upya. Congo haijapata kiongozi makini na mwenye kuiunganisha nchi
 
suluhisho ni kuchukua nchi yote na kuisuka upya. Congo haijapata kiongozi makini na mwenye kuiunganisha nchi
Congo they had a Honest President with a view ya kuwaunganisha (Patrice Lumumba) na walimuua kwa kusalitiwa na one of his own (Mobutu) kwahio kwa mchezo kama huu wa walafi tutaendelea na muendelezo wa rewind; play rewind; play...

Ukiona kuna waasi wengi wanaochipukia kila siku basi tambua hio Nation is not as United as it seems...
 
Hi ni sawa na kusema Rwanda akabidhiwe hicho kipande cha nchi. M23 - Controlled Police force ndio walinde mpaka kweli ?
 
Wakigawa nchi ya congo na kuwapa watutsi..

Itasababisha na watutsi Tanzania na wao wadai ngara igawanywe iwe nchi yao.

Mbona makabila mengine hayana hizo tabia za kudai nchi
 
Territorial integrity ya Cong DR unaichukulia aje?
 
unabishana na nan mkuu?? kwan lazima kila mtu akubaliane na ww??
 
Hi ni sawa na kusema Rwanda akabidhiwe hicho kipande cha nchi.
Je Kivu ina watusi peke yake ?
Banyarwanda are Hutus, Tutsis and Batwa who all speak Kinyarwanda and live along the Rwandan border in Kivu province, together with Hunde, Nyanga and Nande.
M23 - Controlled Police force ndio walinde mpaka kweli ?
Hao M23 pamoja na waasi wowote wengine wa aina yoyote hawapaswi kuwepo, kwangu mimi waasi if necessarly should be a short term thing kwa nchi yenye good governence neno waasi linatakiwa kuonekana kwenye vitabu / kamusi pekee na sio normal occurance
 
unabishana na nan mkuu?? kwan lazima kila mtu akubaliane na ww??
Nani kabisha hapa ? Mimi huwa siongei na mtu bali issues zilizowekwa mezani na hapa hakuna kukubaliana na mimi bali hoja iliyowekwa mezani sasa wewe ukileta Hoja ambazo zinakinzana na facts wala hakuna haja ya kukubishia bali hata mwenyewe unaweza ukijibishia ukilinganisha na uhalisia
 
Wakigawa nchi ya congo na kuwapa watutsi..
Kivu kuna watusi pekee ?!!
Itasababisha na watutsi Tanzania na wao wadai ngara igawanywe iwe nchi yao.
Kwanini ? Sisi tumebagua Kabila lolote ? na ni Nini advantage ya kuchukua nchi yenu ? Tatizo hilo wangefanya Wachagga la kudai nchi huenda leo hii nao wangekuwa hawana tofauti na Watusi na Wahutu huko Rwanda kwa ku overflow.., Na hapa issue ni kwamba Congo ijaribu kuangalia raia wake wote na kama imeshindwa (kushindwa ambako kunaleta shida katika maziwa makuu ) Huenda its about time waachie huko ambapo kumewashinda
Mbona makabila mengine hayana hizo tabia za kudai nchi
Mengi hayana reason, na ukiangalia hio Congo hata baada ya Kupata Independence ni sehemu nyingi zilikuwa zinataka kujitenga na zilikuwa zinagombana kufanya hivyo (Wachagga pia walitaka kuchukua independence wapate nchi yao) jambo ambalo huenda wangelifanya leo hii tungekuwa na watusi na wahutu hapa (Tanzania) wanagombana sababu ya eneo kuwa dogo...

 
Territorial integrity ya Cong DR unaichukulia aje?
Haki ya mwananchi katika nchi yake ni ipi ? Kuna social contract kama aliyepewa majukumu ya kukulinda na kuhakikisha hazi zako zote unapata akishindwa kufanya hivyo hata any moral mandate ya kusema wewe ni part ya sehemu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…