Mzee Kimamingo
JF-Expert Member
- Mar 31, 2024
- 1,861
- 4,462
Hii nzuriGenocide ni simpler solution đź’€
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii nzuriGenocide ni simpler solution đź’€
Shida yenu mnahisi kuonewa wakati nyinyi ndio wakorofi,sijui mtaacha lini kudeka.Na ndio hicho nimekisema tangia mwanzo na hatari kwa Watanzania na nchi nyingine ni kwa kuwaona wanyarwanda wote na warundi wote popote walipo kama virusi fulani ambavyo inapaswa vifukuzwe au kuondolewa.., Je swali kabla ya Kabila kulikuwa hakuna watusi hapo North Kivu ? Na sijasema hilo eneo waachiwe Watusi au Rwanda, bali Jamii zote ambazo zipo hapo sasa hivi ikiwemo na hao watusi; Hamtaki basi walindeni kama raia wengine wa Congo. Sababu chokochoko za huko zinaleta shida na matatizo kwa eneo zima la maziwa makuu na Afrika kwa Ujumla.
Myopic thinking kwa kusema watusi wa Kongo ni Wakongo na mimi nimeshakuwa Mtusi au mtu wa Rwanda ? Tatizo watu kama wewe kesho hamkiwii kusema kabila fulani liende kwenye mkoa fulani (ni mentality ambayo waliitumia sana wakoloni n kufanikiwa ) Divide and Rule...Shida yenu mnahisi kuonewa wakati nyinyi ndio wakorofi,sijui mtaacha lini kudeka.
Hata JK alivyo warudisha mlilalamika sana na kusema tuna Waonea sasabu wazee wenu walikuja Tz miaka mingi iliopita. Tungewachekea basi tungevuna mabua
Nadhani tukianza kusema sio Raia na kuwaonea na kutokuwapa Haki ambazo wanapewa Raia wengine huenda wangesema eneo la Upanga basi wabaki peke yao na mtu mweusi asipite kwa hofu kwamba anaweza kuwauwa (Mfano Mtikila alivyoanza issue za Gambachori that was dangerous) na kila Muhindi angeanza kutafuta bodyguard tusingewalaumu...; Kwahio tunapoangalia ubaya wa Kagame; Museveni na Serikali ya Congo huko Kinshasa tusiache kuangalia na hao waliopo hapo Congo ambapo pia ni kwao kuhakikisha wanaishi kama Binadamu / Wakongo wenzao; Ukitaka kujua shida au raha ya kitu jaribu kuvaa viatu vya muhusika.Ni watu wana haki kama binadamu wengine ila hawana haki ya kutawala sehemu ambayo ulikwenda kulima Chini ya mkoloni, na ikatokea tu upo hapo baada ya Uhuru. Tutsi sio indegnous.
Mfano Mzuri wa Tutsi ni wahindi hapa Tanzania, wakati wa Ukoloni waliletwa wengi kufanya kazi za ukarani na nyenginezo, wana haki ya kupewa kila kitu kama raia wa Tanzania, ila wana haki ya kudai eneo liwe lao? Wana haki kulazimisha asilimia fulani ya viongozi wa toke kwao? Wana haki kulazimisha Boda walinde wao? Hapana hawana haki hio.
Huwezi kugawa nchi Ili kufurahisha kundi fulani tu la kikabila.Kwanza kabisa mimi sio Mtaalamu na baada ya kuangalia kwa haraka matakwa ya pande tofauti nimeona ni vigumu sana kwa upande mmoja kukubaliana na matakwa ya upande mwingine kutokana na usalama wao na kutokuaminiana; Hivyo Suluhisho pekee ni hapo katikati kuwepo na nchi ya hao waliomo. Kwa kufahamu vizuri ugumu wa mgogoro huu ni vema ukauangalia katika mtizamo (perspective) ya watu Husika;
Watutsi ambao ni Wakongo (Ambao Watu wa Congo wanasema ni Wanyarwanda na warudi Kwao):
- Kumbuka hawa kabla ya wakoloni kuweka mipaka yao baadhi yao walikuwepo hapo, kwahio kuwepo kwao Congo sasa hivi sio kwamba wote walikuja bali walijikuta wamewekwa Congo; Kwahio hawa kwa mtizamo wao ni Wakongo
- Hawa watu wananyanyaswa kwamba sio Wakongo na warudi kwao, Sasa kwao wapi sababu ukiwafukuza je unawafukuza na ardhi ?
- Hawa watu wanachotaka wao ni kuwa na haki sawa kama wakongo na uwezo wa kupiga kura n.k, jambo ambalo wakongo hawataki kuwapa (na wana hoja sababu kwa macho yao hawa ni mamluki)
- Hao askari wa M23 nao wanataka wawe assimilited kwenye jeshi la Congo (jambo ambalo sidhani kama Congo watakubali)
Nchi ya Congo
- Wao wanaona hawa sio raia wala wakongo na kwao wanaweza kuwa hatari kwa usalama wa nchi kama mapandikizi, na pia wanaona wanatumika kama nyenzo ya kuwaibia na pia kikundi cha M23 ambacho kinasema kinawalinda watutsi hao kwa Congo kundi hili ni magaidi.
- Kwa Rais wa Congo kukubali hawa watu waingizwe nchini na kupewa kila haki hata yeye akikubali kuna watu wa Congo ambao watamuona kama msaliti, na vilevile kwa macho yake hii ni hatari ya kuleta mamluki (watu ambao wewe unaona sio Watu wako katika nchi yako).
- Congo wanaona M23 ni kama nyenzo ya Rwanda kuwaingilia na ukizingatia hata Kabila alivyochukua nchi alipata msaada wa hawa watu na wakitokea Uganda na kumuondoa Mobutu utaona kwamba Rais wa Congo ana hoja za msingi za kutokukubaliana na assimilation ya hawa watu Congo.
Nchi ya Rwanda:
Kumbuka nchi ya Rwanda Kagame alivyochukua nchi kuna wale watu ambao inasemekana ndio walihusika na mauaji ya Kimbari pamoja na Waliokuwa ndio wanaongoza nchi walikimbilia Congo na kupokelewa Congo, na Ufaransa pamoja na Mobutu kuwafundisha zaidi ili waweze kurudi Rwanda na kumpindua Kagame; Ingawa Kagame na yeye kuona hivyo akatumia Watutsi waliopo Congo kuwafundisha ili kuweza kuwakabili hao anaowaona ni waasi (hivyo matatizo ya Rwanda ni kama yakahamia Congo).
Kwahio ni ngumu kwa Kagame kuona kuna Watutsi wanaonyanyaswa Congo wakati yeye aliingia kwenye madaraka kwa kuonyesha kwamba anamaliza manyanyaso hayo; Na Tukisema hao Watutsi warudi Rwanda, je warudi wapi ukizingatia wengine wapo hapo tangia enzi na enzi ? Pia Kagame lazima jicho lake litakuwa Congo sababu anaona kuna uwezekano wa kuvamiwa kutokea Congo
Uganda:
Uganda pia na yeye yupo macho sababu kunaweza kutokea waasi wowote kutokea Congo kuleta machafuko Uganda ukizingatia community hizi kuna watu ambao walikimbia kutoka Congo kwenda Uganda na wanaweza kurudi wakati wowote na vice versa
Tanzania:
Shida yoyote ya jirani yako pia ni ya kwako mfarakano wowote utakaotokea huko lazima na wewe utakufikia; Pia kuna ndugu zetu Wanyarwanda na Warundi wengi zaidi ambao walikuja huko baada ya shida za huko kwao, shida zinazotokea huko huenda zikaanza kupelekea hawa ndugu zetu kutengwa na kunyanyaswa kama vile watusi wa Congo wanavyoonekana ni matatizo na waleta shida.
Hitimisho
Hitimisho pekee na la kudumu, ni hawa watu waliopo sasa hapo North Kivu (Jamii zote) waweze kupata nchi yao hapo hapo na nchi zote za maziwa makuu na kwa kushirikiana zinaweza zikawa na Base ya kuangalia Amani hapo, na kuhakikisha vinatokomeza vikundi vyote vya Kuasi (Magaidi hata kama wanajiita Freedom Fighters) na vya aina yoyote kwa kuwa assimiliate katika nchi yao hii mpya. Na kuhakikisha hakuna masalia ambayo yanaweza kuanzia hapo na kuleta shida yoyote au kutishia Amani katika nchi Jirani.
Suala hili inabidi sisi kama Waafrika tusaidiane kulimaliza na kabla ya Afrika sisi majirani kwanza (Maziwa Makuu)
ndicho kagame anachotafuta, na wakifanya hivyo hawatamaliza hata mwaka, wataungana na rwanda na kuwa nchi moja ili rwanda iongezeke kieneo na kiresources.Kwanza kabisa mimi sio Mtaalamu na baada ya kuangalia kwa haraka matakwa ya pande tofauti nimeona ni vigumu sana kwa upande mmoja kukubaliana na matakwa ya upande mwingine kutokana na usalama wao na kutokuaminiana; Hivyo Suluhisho pekee ni hapo katikati kuwepo na nchi ya hao waliomo. Kwa kufahamu vizuri ugumu wa mgogoro huu ni vema ukauangalia katika mtizamo (perspective) ya watu Husika;
Watutsi ambao ni Wakongo (Ambao Watu wa Congo wanasema ni Wanyarwanda na warudi Kwao):
- Kumbuka hawa kabla ya wakoloni kuweka mipaka yao baadhi yao walikuwepo hapo, kwahio kuwepo kwao Congo sasa hivi sio kwamba wote walikuja bali walijikuta wamewekwa Congo; Kwahio hawa kwa mtizamo wao ni Wakongo
- Hawa watu wananyanyaswa kwamba sio Wakongo na warudi kwao, Sasa kwao wapi sababu ukiwafukuza je unawafukuza na ardhi ?
- Hawa watu wanachotaka wao ni kuwa na haki sawa kama wakongo na uwezo wa kupiga kura n.k, jambo ambalo wakongo hawataki kuwapa (na wana hoja sababu kwa macho yao hawa ni mamluki)
- Hao askari wa M23 nao wanataka wawe assimilited kwenye jeshi la Congo (jambo ambalo sidhani kama Congo watakubali)
Nchi ya Congo
- Wao wanaona hawa sio raia wala wakongo na kwao wanaweza kuwa hatari kwa usalama wa nchi kama mapandikizi, na pia wanaona wanatumika kama nyenzo ya kuwaibia na pia kikundi cha M23 ambacho kinasema kinawalinda watutsi hao kwa Congo kundi hili ni magaidi.
- Kwa Rais wa Congo kukubali hawa watu waingizwe nchini na kupewa kila haki hata yeye akikubali kuna watu wa Congo ambao watamuona kama msaliti, na vilevile kwa macho yake hii ni hatari ya kuleta mamluki (watu ambao wewe unaona sio Watu wako katika nchi yako).
- Congo wanaona M23 ni kama nyenzo ya Rwanda kuwaingilia na ukizingatia hata Kabila alivyochukua nchi alipata msaada wa hawa watu na wakitokea Uganda na kumuondoa Mobutu utaona kwamba Rais wa Congo ana hoja za msingi za kutokukubaliana na assimilation ya hawa watu Congo.
Nchi ya Rwanda:
Kumbuka nchi ya Rwanda Kagame alivyochukua nchi kuna wale watu ambao inasemekana ndio walihusika na mauaji ya Kimbari pamoja na Waliokuwa ndio wanaongoza nchi walikimbilia Congo na kupokelewa Congo, na Ufaransa pamoja na Mobutu kuwafundisha zaidi ili waweze kurudi Rwanda na kumpindua Kagame; Ingawa Kagame na yeye kuona hivyo akatumia Watutsi waliopo Congo kuwafundisha ili kuweza kuwakabili hao anaowaona ni waasi (hivyo matatizo ya Rwanda ni kama yakahamia Congo).
Kwahio ni ngumu kwa Kagame kuona kuna Watutsi wanaonyanyaswa Congo wakati yeye aliingia kwenye madaraka kwa kuonyesha kwamba anamaliza manyanyaso hayo; Na Tukisema hao Watutsi warudi Rwanda, je warudi wapi ukizingatia wengine wapo hapo tangia enzi na enzi ? Pia Kagame lazima jicho lake litakuwa Congo sababu anaona kuna uwezekano wa kuvamiwa kutokea Congo
Uganda:
Uganda pia na yeye yupo macho sababu kunaweza kutokea waasi wowote kutokea Congo kuleta machafuko Uganda ukizingatia community hizi kuna watu ambao walikimbia kutoka Congo kwenda Uganda na wanaweza kurudi wakati wowote na vice versa
Tanzania:
Shida yoyote ya jirani yako pia ni ya kwako mfarakano wowote utakaotokea huko lazima na wewe utakufikia; Pia kuna ndugu zetu Wanyarwanda na Warundi wengi zaidi ambao walikuja huko baada ya shida za huko kwao, shida zinazotokea huko huenda zikaanza kupelekea hawa ndugu zetu kutengwa na kunyanyaswa kama vile watusi wa Congo wanavyoonekana ni matatizo na waleta shida.
Hitimisho
Hitimisho pekee na la kudumu, ni hawa watu waliopo sasa hapo North Kivu (Jamii zote) waweze kupata nchi yao hapo hapo na nchi zote za maziwa makuu na kwa kushirikiana zinaweza zikawa na Base ya kuangalia Amani hapo, na kuhakikisha vinatokomeza vikundi vyote vya Kuasi (Magaidi hata kama wanajiita Freedom Fighters) na vya aina yoyote kwa kuwa assimiliate katika nchi yao hii mpya. Na kuhakikisha hakuna masalia ambayo yanaweza kuanzia hapo na kuleta shida yoyote au kutishia Amani katika nchi Jirani.
Suala hili inabidi sisi kama Waafrika tusaidiane kulimaliza na kabla ya Afrika sisi majirani kwanza (Maziwa Makuu)
Hakuna wa kuigawa Drc..Una hoja ya msingi,
Congo igwanywe tu kwa sababu imeshindwa kutawalika kutokea Kinshasa, DRC Mashariki wapewe nchi yao.
Kuna tatizo gani ikiwa hivyo?ndicho kagame anachotafuta, na wakifanya hivyo hawatamaliza hata mwaka, wataungana na rwanda na kuwa nchi moja ili rwanda iongezeke kieneo na kiresources.
Kwa hiyo Kagame ni Putin wa Africa?Kuna tatizo gani ikiwa hivyo?
Mbona Russia wamechukua 20% ya Ukraine na hawajafanywa chochote?
Mkuu mimi sio mzoefu, naweza pia kuwa nakosea, ila ninavyofahamu vita vya M23 si sawa na vya nyuma,Okay nadhani wewe una ujuzi na hilo eneo zaidi; hapo Kivu kuna Jamii ngani na je zote haziwezi kukaa pamoja; sababu kwa sasa kusema hawa wakongo wa asili ya Kitusi kukubaliwa kuwa na haki zote za kiraia za Congo nzima ni ngumu sababu ya chuki iliyopo; je unadhani kipi rahisi kukubaliwa na hao kina Batwa, Nande na Bashi au kukubaliwa na Congo nzima ? Sababu kinachoendelea sasa hao wote ni kama watoto yatima
Kwa nini sio Trump anayeitaka Greenland au Panama??Kwa hiyo Kagame ni Putin wa Africa?
Trump hajaivamia Greenland na Panama kama Kagame na Putin walivyovamia jirani zaoKwa nini sio Trump anayeitaka Greenland au Panama??
Yani masharti ya kugawa hilo eneo ni kuwapa Watutsi kama Viongozi, so hata likigawanywa ina maana hutawasaidia wa kazi wa Kivu, pengine wakachezea kichapo kuliko cha sasa, watapata tabu kama wanazopata Wanyarwanda.Hayo madini tunayacontrol vipi ? Sababu hata sisi Tanzania raia tunasema tuna madini kwa maneno tu ila wanufaika mwisho wa siku sio sisi; Mbili sijasema watusi wapewe eneo; nimesema hilo eneo ambalo sasa hivi watu ni kama Yatima wakiwemo watusi litengwe na liwe nchi kamili na watu waliopo waweze kujipanga na kuendesha nchi yao na kama watafanya vitu kwa demokrasia basi majority watakuwa na nguvu (Na kama watakuwa na busara na sio wapuuzi basi watachaguana viongozi kulingana na merits na sio huyu wa Kabila langu)
Greenland wakianza kupigania mpakani mwa Marekani atavamia.Trump hajaivamia Greenland na Panama kama Kagame na Putin walivyovamia jirani zao
Huu ni mtazamo wako tu, sio lazima iwe hivyo na kwanini wapigane ?...Greenland wakianza kupigania mpakani mwa Marekani atavamia.
Unajifunza kuwa tatizo siyo nchi, tatizo ni maslahi binafsi ya viongozi wa pande zisizokubaliana.Mkuu, mwafrika akili zake anazijua mwenyewe. Sudan walipigana mpaka wakatenga Sudan mbili. Ajabu ile Sudan ya Kusini baada ya kuwa nchi, wakashindwana wao kwa wao na sasa wanapigana.
Mexico kuna wakati huwa inaruhusu Task Forces za DEA kuingia kufanya operations baadhi ya maeneo, pia DRC imekuwa na vita tangu enzi za Mobutu wakati Rwanda ikiwa na viongozi wajinga wajinga.Huu ni mtazamo wako tu, sio lazima iwe hivyo na kwanini wapigane ?...
Magenge ya wauza unga wa Mexico yanapigana yenyewe kwa yenyewe mpakani mwa Mexico na Marekani ila Marekani hajaivamia Mexico.
Kagame kavamia Drc Ili na kuivuruga hiyo nchi kwa manufaa yake binafsi na wanasiasa wenzake wachache.
Mexico inafanya hayo kwa ridhaa yake, huo sio uvamiziMexico kuna wakati huwa inaruhusu Task Forces za DEA kuingia kufanya operations baadhi ya maeneo, pia DRC imekuwa na vita tangu enzi za Mobutu wakati Rwanda ikiwa na viongozi wajinga wajinga.