Mkuu
Tized ninashukuru sana kwa kunialika katika kuchangia uzi huu muhimu sana ambapo suala la kungonoka kati ya wawili wapendanao limekuwa ni tatizo sana. Tena mbaya zaidi hata vijana ambao hata 40s hawajatimiza lakini wana tatizo kubwa sana. Matokeo yake wamekuwa wakiishia kununua madawa ya kichina au hata kupost humu kuwa wanahitaji msaada. Uliyoyasema hapo kwenye post yako ni haswa habari yenyewe na hakika hata kama umri umeenda lakini kama utazingatia life style na mengine basi hata siku moja hutashindwa kumridhisha mke au mpenzi wako. Mimi kama
Zogwale ambaye kiumri niko mbali lakini maisha ya ndani si tatizo kabisa japo siwezi kuwa sawa na wakati ule nikiwa katika 20s na 30s. Cha msingi:
(a) Epuka kuwa na wapenzi wengi kwa kuwa at times unaiikuta nguvu zako kimapenzi zinapungua due to overdose/use.
(b) Epuka magomvi kati yenu na kama ikitokea kuhitilafiana basi kabla hamjaingia kulala yamalizeni tena kama hali inaruhusu malizia na penzi la aina yake. Hapa hamtakaa mchokane,
(c) Mazoezi wewe na mwenzio, kama hajitumi andaeni programme ya mazoezi pamoja. Wote hapa mtakuwa active sana.
(d) Chakula ni dawa na ni sumu!!!!!! kwa nguvu za mapenzi!!!! Epuka vyakula vya kuunga sana!!! Prefer mchemsho. Kula whole grain - kwangu tunakula dona limechanganywa soya, karanga, ulezi, mtama i.e ni lishe tunapikia ughali.
(f) Matunda, mboga za majani na maji mengi.
(g) Pombe natumia occasionally na wine on and off. Kwa hapa wenzangu wa umri wangu walevu wanaonekana wazee mno.
(h) Epuka red meat, kula protein za nafaka na white meat.
(I) Karanga na jamii yake, water melon na mbegu zake, boga na mbegu zake!!!!
Kwa hayo na mengine huna sababu ya Viagra au madawa ya kichina.
Nawasilisha mkuu. Nilikuwa off JF kwa muda kidogo.Sorry for late response.