Habari ndugu zangu Watanzania
Mara nyingi na kwa kipindi kirefu tumekuwa tukisikia na kuambiwa kuwa Tanzania taifa letu ni kisiwa cha amani, kwamba tofauti na mataifa mengine Tanzania ni nchi yenye utulivu na amani, lakini bila shaka jambo hilo siyo la kweli tena. Kwani
Ripoti ya tume ya uchunguzi ya jaji Chande inasema vurugu za uchaguzi zilisababisha mauaji ya watu zaidi ya 500. Hiyo ni idadi kubwa sana ya watu na bila shaka hayo ni machafuko makubwa sana ya kisiasa.
Ukiangalia mauaji yaliyotokea Afrika Kusini mwaka 1960 yalichukua uhai wa watu 69 lakini bado yakaitwa Sharpeville Massacre. Sasa fananisha hizo namba mbili 518 na 69 ili uweze kuona ukubwa wa tatizo.
Lakini mbali na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2025, mwaka huu pia 2026 tarehe saba mwezi wa saba kulikuwa na hamasa mitandaoni ya kufanyika kwa maandamano mengine.
Wakatokea watu wakawatambulisha vijana wanaitwa Mbwa Mwitu wenye mafunzo maalum ya kivita. Na kwamba vijana hao walikuwa tayari kukabiliana na waandamanaji.
Maana ake ni kwamba kama maandamano yangetokea tarehe saba mwezi wa saba mwaka 2026 hali ingekuwa mbaya zaidi. Lakini kwa hekima kuu sana waandamanaji waliahirisha maandamano.
Nichukue nafasi hii kuwapongeza waandamanaji kwa uamuzi huo mtukufu ulionusuru taifa hili kuingia kwenye machafuko mengine tena ambayo yangeendelea kulifedhehesha taifa letu. Mwenyezi Mungu yupo, naye anajua madai ya haki ya waandamanaji na kwa wema na hekima yake atawatimizia kwa wakati.
Sasa tumeshajiridhisha kwamba taifa hili halina amani. Swali ni hili tufanye nini ili turejeshe amani au labda niseme tujenge msingi wa amani. Yafuatayo bila shaka yanaweza yakasaidia...
1. Tuendeshe chaguzi zilizo huru na za haki
Bila shaka matatizo yaliyotokea yametokea kwa sababu watu hawana Imani na chaguzi zinazoendeshwa hapa nchini. Ndio maana kuna chama kimoja kilikataa hata kushiriki uchaguzi wenyewe. Kama uchaguzi ule ungekuwa unaaminika kila chama kingesimamisha wagombea wananchi wangepiga kura na watu wangesikiliza matokeo kwa amani.
Ukweli ni huu tutake tusitake vyama vikubwa vyote hapa nchini vina wafuasi wengi. Kwa hiyo mashindano hayo ya kisiasa hayana budi kumalizwa kwa njia ya uchaguzi, chama kitakachoshinda, kimeshinda, kilichoshindwa kijiandae kwa chaguzi zijazo.
Kwa mfano wale wanaompenda tuseme Deogratius wampigie kura Deogratius siyo walale nyumbani wasubiri Deogratius awekwe madarakani kwa nguvu. Na wale wanaompenda Emmanuel wakampigie kura Emmanuel, siyo Emmanuel akamatwe na aonewe, wafuasi wake waandamane na kisha waanze kupigwa risasi. Mwenye kura nyingi apewe uongozi. Kwa mfano kama akishinda Emmanuel apewe uongozi wasiompenda Emmanuel wakubali matokeo huo ndio utaratibu wa uchaguzi. Na Emmanuel ni mtu mwenye hekima yule ataongoza kwa hekima wala hatalipa visasi.
2. Turuhusu maandamano
Matatizo yaliyopo yanatokana na kukataza maandamano. Kwa maana zamani zile miaka ya 2016 lilitolewa katazo la maandamano ya kisiasa, waandamanaji wakasema ni haki yetu kikatiba, hawakujibiwa waliambiwa andamaneni mtakiona. Kama ilivyo kawaida ya waandamanaji wakasikiliza busara za viongozi wa dini wakaahirisha maandamano.
Lakini uonevu ule usingedumu milele, kwa maana ilipofika mwaka 2025 watu wakataka tena kuandamana. Wakakatazwa tena kuandamana. Mm nakumbuka nilisikia kuwa kutakuwa na maandamano ya kupigania demokrasia, mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi na utawala wa sheria. Nikasema ni mambo mazuri sana hayo wanayadai hao wazalendo watukufu. Nikawauliza maandamano hayo yataanzia wapi ili nami nijiunge nao tuweze kupigania taifa letu. Nikaambiwa hawawezi sema kwasababu watampa adui namna ya kuyaharibu. Nikashangaa Hee! alafu adui mwenyewe kumbe ni polisi.
Basi nikajifunza tatizo ni kukataza maandamano, hicho ndio kinasababisha maandamano yawe ya utaratibu huo.
Kwa hiyo ili turejeshe amani inabidi turuhusu maandamano, watu wakitaka kuandamana hata kila siku waruhusiwe. Watoe tu taarifa polisi kwa ajili ya usalama. Hii itakuza demokrasia na kuongeza uwajibikaji. Kumbuka maandamano siyo fujo (hata kanisani kuna maandamano ya ekaristi sijui nini) ni utaratibu wa kipekee wa kuwasilisha maoni au malalamiko. Acheni watu wachonge mabango, waimbe nyimbo, wakate matawi ya mti watoe dukuduku lao. Kama malalamiko yao hayana msingi waelimishwe na wapewe mda watajitambua tu. Lakini kwa kuwa hawafanyi fujo wanaandamana tu waachwe.
3. Tuendeleze jitihada za kukomesha ufisadi wa viongozi na tabaka flani la juu na kutokomeza umaskini kwa raia walio wengi.
Maandamano ya oktoba 29 2025 yalikuwa na doa moja waandamanaji walichoma mali za watu. Hii inatokana na hasira za ugumu wa maisha na ufisadi wa viongozi na washirika wao. Kwahiyo ili nchi iendelee kuwa ya amani ni lazima serikali ya chama chochote kitakachokuwa kimechaguliwa kihalali kifanye vita dhidi ya ufisadi kuwa agenda kuu. Kila awamu, kila chama, kila mwaka mpaka kiyama mapambano dhidi ya ufisadi na kushughulika na umaskini wa raia viwe kipaumbele kwa serikali.
Mataifa mengine yamefanya hivyo mfano China na tumeona matunda yake. Matunda yake ni amani na maendeleo. Tunaweza kuiga mema ya mataifa mengine na kuboresha mengine kulingana na mazingira yetu.
4. Kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya
Tume ya uchunguzi ya jaji Othman Chande katika mapendekezo yake imesema kuwa ili Tanzania irejeshe amani ni lazima katiba mpya iwe imepitakana kabla ya mwaka 2030. Na tena kwa bahati nzuri suala la katiba mpya ni ajenda ya vyama vyote kwa hiyo hakuna sababu ya kuendelea kulipotezea swala hili.
Mchakato wa katiba mpya lazima uhusishe pande zote wale wa upande chama tawala na wale wa upande wa wapinzani na wanaharakati, hata hivyo mara hii lazima tuhakikishe tunafikia mwafaka isiwe kama 2014. Ikiwezekana katiba iliyopendekezwa na ile ya Warioba zipigwe chini zote tuanze upya. Kwanza wanasema waandamanaji wengi mwaka jana walikuwa jen z na sidhani kama walishiriki ule mchakato wa awali.
Mjadala wa kutengeneza katiba itakuwa ndio nafasi adhimu ya pande zote zinazohasimiana kujadiliana na kufikia mwafaka kuhusu mustakabali wa taifa letu na hivyo kuridhiana.
#AMANI
#KATIBAMPYASASA