SoC04 Suluhu ya Ushoga nchini; Historia yangu binafsi na mbinu mbadala

Tanzania Tuitakayo competition threads

USHINDI MKUU

Member
Joined
Jun 4, 2024
Posts
44
Reaction score
70
Awali ya yote, naomba nieleze historia yangu kwa ufupi. Nia na madhumuni niweze kujenga picha ya jumla katika lengo zima la uzi huu.

Nilizaliwa katika mkoa wa Mwanza nchini Tanzania, Baba yangu alikuwa Polisi na mama yangu alikuwa Mama wa nyumbani. Wazazi wangu kwa pamoja walinipenda sana, walinijali, walinihudumia na nilikuwa mtoto mwenye furaha na malezi bora kwa ujumla wake.

Nilipokuwa na umri mdogo angalau miaka mitano, nilijikuta nimezama katika vitendo ambavyo kwa wakati huo sikuvijua jina lake, lakini baadaye nilipoanza kukua na kujitambua, nikaelezwa kuwa vitendo vile vinaitwa "ushoga" na wengine wakaanza kuniita "shoga". Sikuwa naelewa vizuri maana yake lakini kutokana na ukali wa maneno yao nilianza kutambua kuwa lile jambo kwa vyovyote halikuwa zuri.

Tulikuwa tukiishi katika nyumba za wafanyakazi wa serikali (kotaz) ambamo tulikuwemo takribani familia saba. Palikuwa na mtoto wa kiume nyumba ya jirani mwenye umri wa miaka nane ambaye alikuwa rafiki yangu sana tuliyekuwa tukicheza nae. Mimi nilikuwa nina umri wa miaka mitano kama nilivyotangulia kusema hapo awali.

Rafiki huyu alikuwa anapenda kunipeleka nyumbani kwao wakati wazazi wake hawapo. Alinifuata nyumbani na tukaongozana naye kwenda kwao. Tulikuwa tunaendesha magari ya plastiki katika michezo yetu. Katika hali ambayo sikuwa naielewa, katikati ya mchezo alikuwa akinivua kaptula na kuniambia tucheze kama ng'ombe halafu ananipanda kwa juu na kuanza kunibambia bambia huku akilia kama ng'ombe 'mooo mooo'. Sikuwa naelewa ni nini lakini kwa kiasi nilikuwa nakifurahia kile kitendo kwa sababu hata hivyo amenihakikishia kuwa "tunawaigiliza ng'ombe".

Baada ya kunifanyia kitendo kile kwa muda wa siku nyingi, nikawa namfuata mwenyewe namwambia anipande kama ng'ombe tucheze "king'ombe ng'ombe". Nilikuwa nafurahia sana na nikawa mzoefu kwenye mchezo huo, alinivua na kushika "chululu" yake na kuiweka juu ya "kitundu" changu. Kwa wakati huo tulikuwa watoto wadogo sana na sikujua maana ya kitendo tunachokifanya wala jina la kitendo hicho. Kilichokuwa akilini mwangu ni kufurahia ule mchezo tu basi. Tuliendelea na mchezo wetu kwa muda mrefu bila mtu yeyote kujua.

Baadaye tulihama tukahamia mkoa mwingine, nikawa sina wa kufanya nae ule mchezo huku nikizidi kumkumbuka rafiki yangu bila kujua niende kwa nani nikafanye nae. Nilikuwa ninaishi na kaka zangu na dada zangu lakini sikuwahi kujaribu kwao, ni kama nilikuwa na ufahamu wa ndani kuwa kitendo kile si chema. Kwa wakati huo sikujua nimfuate nani tukacheze nae mchezo wa "king'ombe ng'ombe".

Kutokana na kufurahia ule mchezo, kila wageni wa kiume walipokuja kulala nyumbani nililia kulala nao na kuanza kuwashika shika nyakati za usiku. Wengine waliniruhusu na wengine walinikemea lakini niliendelea na tabia hiyo kila siku. Wazazi nao waliniruhusu kulala na wageni kwa sababu hata hivyo waliwaamini sana, baadhi yao walikuwa ni watoto wa baba mdogo au shangazi na ndugu wengine. By the way, nyumba ilikuwa na vyumba viwili tu hivyo hapakuwa na namna nyingine.

Sikuwa nimetimiza umri wa balehe lakini kitendo kile kilikuwa kimenikaa sana katika UTU WANGU, ni kama gundi au muhuri uliopigwa chapa katika nafsi yangu. Niliendelea kwa muda mrefu sana, kila nikipata nafasi nilikuwa nachezeana na wavulana wenzangu kwenye kimbolela, mapagarani na shuleni. Nikawa bingwa wa mchezo huu.

Baada ya muda fulani, nikaanza kuwa na tabia za kike kike, nikawa nacheza na wasichana michezo ya rede au mdako na michezo mingine ya kike lakini sikuwahi kuwatamani au kulala nao. Hata sauti yangu nayo kwa namna ya "kimiujiza" nayo ikawa ya kike kabisa. Sikuwahi kucheza na wavulana wenzangu, nilikuwa nawaogopa sana kutokana pia na wengine kunitania kuwa nina sura ya kike na tabia za kike.

Nilipoanza kubalehe, sauti ikaanza kuwa ya kiume lakini vitendo vya kike. Baba yangu alinipeleka shule ya boarding katika mojawapo ya shule za Kanisa. Nilipokuwa shuleni nikawa nawatamani sana wavulana wenzangu wanifanye. Baadhi nilifanikiwa kuwashawishi nifanye nao wakakubali na wengine walikataa. Wengine walinifuata wenyewe baada ya kusikia habari zangu. Huo ndio ukawa mchezo wetu nilioupenda sana.

Siri ilipoanza kuvuja shuleni kwamba nafanywa na wenzangu, wakawa wananitania na kunidhihaki na kuniita shoga na majina mengine ya aina hiyo. Wengine wakawa wananivizia na kunishambulia kwa vipigo.

Kwa ujumla wake maisha ya shule yalianza kuwa magumu sana nikaanza kujenga tabia ya unyonge na kujitenga kila pahala. Kila nilipopita wenzangu walikuwa wananizomea na kunicheka kwa kejeli kubwa sana. Nilidhurika mno kiakili kiasi cha kutaka kukimbia shule.

Hisia za ushoga zilinitawala sana akili yangu lakini kwa kiasi kikubwa nilifanikiwa kujizuia na kujidhibiti hatimaye nilimaliza kidato cha nne. Bahati nzuri nilikuwa nina akili nyingi za darasani niliweza kufaulu kwa alama kubwa nikaenda kidato cha tano na sita mpaka chuo kikuu. Alhamdulillah.

Kwa ujumla wake sitambui nilikosea wapi, lakini siku zote ninajiasa kujidhibiti, kujiongoza, kujipenda na kuwasamehe watu wote. Siwezi kumlaumu mtu yeyote isipokuwa macho yangu yapo kwa Mungu ambaye ni mjuzi zaidi kuliko Mimi. Ninaamini ameniponya na atanipa fungu lililo bora zaidi.

Nimefanikiwa kuoa na nina watoto wawili mpaka sasa. Nampenda mke wangu na ananipenda pia. Tuna miaka mitano ya ndoa yetu.

USHAURI WANGU kwa wazazi wote wa nchi hii, wawe makini na watoto wao kwa kila hatua. Ni muhimu kutenga muda wa kutazama nyendo za mtoto na tabia zake kwa ujumla. Jambo dogo linaweza kuharibu mfumo mzima wa maisha ya mtoto na tabia yake yote na asiweze kujinasua milele. Tuwalinde watoto na tuwaongoze katika njia sahihi.

Wakati mwingine si kosa la wazazi kwa sababu mzazi hawezi kuwa Mungu muonaji wa vyote. Kuna kuteleza na kushindwa kutazama nyendo zote za Mtoto. Tumuombe Mungu awalinde watoto wetu pale ambapo macho yetu hayawezi kufika.

Ninaiomba serikali iunde vituo maalumu vyenye tiba ya kisaikolojia na ya kitabibu kwa wote waliodhurika na ushoga na ambao wako tayari kuachana nao. Tiba hii ihusishe mabingwa wa maradhi ya kitabia, maradhi ya kiakili na maradhi ya kibayolojia katika kuwakwamua waathirika wa jambo hili na inawezekana. Hata msaada wa kiroho pia unaweza kujumuishwa na iwe ni mkakati wenye malengo thabiti kabisa. Sio wote wenye nguvu za kiakili za kuweza kujiponya kama nilivyofanya mimi. Wengine wanahitaji msaada kutoka nje. Kujiponya inahitaji nidhamu ya hali ya juu na akili thabiti pamoja na usaidizi wa Mungu.

Serikali ione haja ya kuunda mkakati endelevu wa kuwasaidia wote waliozama katika shimo hili la giza kupitia wataalamu wake na taasisi zake. Madhara ya kutowasaidia ni pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya ngono, Ukimwi, kisonono na mengineyo. Tiba hii itajumuisha tiba ya kiakili, tiba ya madhara ya msongo wa mawazo au Post Traumatic Disorder pamoja na tiba ya kitabia. TUWASAIDIE.

Tanzania bila ushoga inawezekana tukiwekeza katika mbinu zenye nia ya kweli na ya dhati ya kuwasaidia waathirika wote kupitia vituo maalumu vya kitabibu na kisaikolojia ambavyo vinaweza kuwa na muundo wa "rehab" au muundo mwingine utakaofaa.

Katika yote Mungu ndio mjuzi zaidi. Macho yetu yazidi kumuelekea yeye daima.

Alhamdullilaah!
 
Upvote 56
Pole sana, naamini utakuwa umeacha kabisa...wanaoukumbwa na hii kadhia nawaonea huruma sana, kipindi nasoma advance Kuna jamaa mmoja mtu wa iringa huko tena ni kiongozi shuleni naye alifukuzwa Shule kisa kuwa ni shoga, daah inasikitisha kweli mwanaume kuwa shoga lakini nadhani wanaweza kujinasua japo Sina hakika.
 
I just hate it some guys decided to bully you simply because you are homosexual. I can only imagine jinsi umepitia vingi mpaka kuamua kubadilika ili kuendana na jamii inavyotarajia uwe.

That being said. Am not a homosexual na siamini kama jamii yetu Africa, haswa Tanzania, kama inatakiwa kusupport homosexuality kwa 100% kama donors wanavyotaka
 
asante chief, yote ni mapito ya maisha.
 
Pole sana, naamini utakuwa umeacha kabisa...wanaoukumbwa na hii kadhia nawaonea huruma sana, kipindi nasoma advance Kuna jamaa mmoja mtu wa iringa huko tena ni kiongozi shuleni naye alifukuzwa Shule kisa kuwa ni shoga, daah inasikitisha kweli mwanaume kuwa shoga lakini nadhani wanaweza kujinasua japo Sina hakika.
Kiukweli kujinasua sio rahisi, ni ngumu sana ila inawezekana.
 
Naam nikupe hongera sana kwa kufunguka na kulichukulia hili jambo kama janga na tatizo kubwa kwataifa na dunia nzima tofauti na mbuzi wengine ambao wao huona ni kama tabia sahihi na jambo la kujivunia
wapo kwenye mwezi wao huu wanauita priDEMONth, waathirika wakiwa na mtazamo halisi kuwa hili jambo halifai hakika tutakuwa na jamii thabiti
 
Umeelezea jinsi ulivyoingia na ulivyoishi na hisia hizo shuleni.
Lakini hujagusia hata kidogo ni kwa namna gani umejinasua kwa kutumia akili yako(kama unavyojinasibu) zaidi ya kuitupia mpira serikali na jamii tena.

Ingelikua vizuri kama ungeweka ABC ulizofata hadi ukajinasua, huenda kuna mwingine akatumia mbinu zako au zinazoshabihiana na zako akajinasua pasi na kuisubiri serikali kama wewe ulivyofanya.
 
Awali ya yote, naomba nieleze historia yangu kwa ufupi. Nia na madhumuni niweze kujenga picha ya jumla katika lengo zima la uzi huu.

Nilizaliwa katika mkoa wa Mwanza nchini Tanzania, Baba yangu alikuwa Polisi na mama yangu alikuwa Mama wa nyumbani. Wazazi wangu kwa pamoja walinipenda sana, walinijali, walinihudumia na nilikuwa mtoto mwenye furaha na malezi bora kwa ujumla wake.

Nilipokuwa na umri mdogo angalau miaka mitano, nilijikuta nimezama katika vitendo ambavyo kwa wakati huo sikuvijua jina lake, lakini baadaye nilipoanza kukua na kujitambua, nikaelezwa kuwa vitendo vile vinaitwa "ushoga" na wengine wakaanza kuniita "shoga". Sikuwa naelewa vizuri maana yake lakini kutokana na ukali wa maneno yao nilianza kutambua kuwa lile jambo kwa vyovyote halikuwa zuri.

Tulikuwa tukiishi katika nyumba za wafanyakazi wa serikali (kotaz) ambamo tulikuwemo takribani familia saba. Palikuwa na mtoto wa kiume nyumba ya jirani mwenye umri wa miaka nane ambaye alikuwa rafiki yangu sana tuliyekuwa tukicheza nae. Mimi nilikuwa nina umri wa miaka mitano kama nilivyotangulia kusema hapo awali.

Rafiki huyu alikuwa anapenda kunipeleka nyumbani kwao wakati wazazi wake hawapo. Alinifuata nyumbani na tukaongozana naye kwenda kwao. Tulikuwa tunaendesha magari ya plastiki katika michezo yetu. Katika hali ambayo sikuwa naielewa, katikati ya mchezo alikuwa akinivua kaptula na kuniambia tucheze kama ng'ombe halafu ananipanda kwa juu na kuanza kunibambia bambia huku akilia kama ng'ombe 'mooo mooo'. Sikuwa naelewa ni nini lakini kwa kiasi nilikuwa nakifurahia kile kitendo kwa sababu hata hivyo amenihakikishia kuwa "tunawaigiliza ng'ombe".

Baada ya kunifanyia kitendo kile kwa muda wa siku nyingi, nikawa namfuata mwenyewe namwambia anipande kama ng'ombe tucheze "king'ombe ng'ombe". Nilikuwa nafurahia sana na nikawa mzoefu kwenye mchezo huo, alinivua na kushika "chululu" yake na kuiweka juu ya "kitundu" changu. Kwa wakati huo tulikuwa watoto wadogo sana na sikujua maana ya kitendo tunachokifanya wala jina la kitendo hicho. Kilichokuwa akilini mwangu ni kufurahia ule mchezo tu basi. Tuliendelea na mchezo wetu kwa muda mrefu bila mtu yeyote kujua.

Baadaye tulihama tukahamia mkoa mwingine, nikawa sina wa kufanya nae ule mchezo huku nikizidi kumkumbuka rafiki yangu bila kujua niende kwa nani nikafanye nae. Nilikuwa ninaishi na kaka zangu na dada zangu lakini sikuwahi kujaribu kwao, ni kama nilikuwa na ufahamu wa ndani kuwa kitendo kile si chema. Kwa wakati huo sikujua nimfuate nani tukacheze nae mchezo wa "king'ombe ng'ombe".

Kutokana na kufurahia ule mchezo, kila wageni wa kiume walipokuja kulala nyumbani nililia kulala nao na kuanza kuwashika shika nyakati za usiku. Wengine waliniruhusu na wengine walinikemea lakini niliendelea na tabia hiyo kila siku. Wazazi nao waliniruhusu kulala na wageni kwa sababu hata hivyo waliwaamini sana, baadhi yao walikuwa ni watoto wa baba mdogo au shangazi na ndugu wengine. By the way, nyumba ilikuwa na vyumba viwili tu hivyo hapakuwa na namna nyingine.

Sikuwa nimetimiza umri wa balehe lakini kitendo kile kilikuwa kimenikaa sana katika UTU WANGU, ni kama gundi au muhuri uliopigwa chapa katika nafsi yangu. Niliendelea kwa muda mrefu sana, kila nikipata nafasi nilikuwa nachezeana na wavulana wenzangu kwenye kimbolela, mapagarani na shuleni. Nikawa bingwa wa mchezo huu.

Baada ya muda fulani, nikaanza kuwa na tabia za kike kike, nikawa nacheza na wasichana michezo ya rede au mdako na michezo mingine ya kike lakini sikuwahi kuwatamani au kulala nao. Hata sauti yangu nayo kwa namna ya "kimiujiza" nayo ikawa ya kike kabisa. Sikuwahi kucheza na wavulana wenzangu, nilikuwa nawaogopa sana kutokana pia na wengine kunitania kuwa nina sura ya kike na tabia za kike.

Nilipoanza kubalehe, sauti ikaanza kuwa ya kiume lakini vitendo vya kike. Baba yangu alinipeleka shule ya boarding katika mojawapo ya shule za Kanisa. Nilipokuwa shuleni nikawa nawatamani sana wavulana wenzangu wanifanye. Baadhi nilifanikiwa kuwashawishi nifanye nao wakakubali na wengine walikataa. Wengine walinifuata wenyewe baada ya kusikia habari zangu. Huo ndio ukawa mchezo wetu nilioupenda sana.

Siri ilipoanza kuvuja shuleni kwamba nafanywa na wenzangu, wakawa wananitania na kunidhihaki na kuniita shoga na majina mengine ya aina hiyo. Wengine wakawa wananivizia na kunishambulia kwa vipigo.

Kwa ujumla wake maisha ya shule yalianza kuwa magumu sana nikaanza kujenga tabia ya unyonge na kujitenga kila pahala. Kila nilipopita wenzangu walikuwa wananizomea na kunicheka kwa kejeli kubwa sana. Nilidhurika mno kiakili kiasi cha kutaka kukimbia shule.

Hisia za ushoga zilinitawala sana akili yangu lakini kwa kiasi kikubwa nilifanikiwa kujizuia na kujidhibiti hatimaye nilimaliza kidato cha nne. Bahati nzuri nilikuwa nina akili nyingi za darasani niliweza kufaulu kwa alama kubwa nikaenda kidato cha tano na sita mpaka chuo kikuu. Alhamdulillah.

Kwa ujumla wake sitambui nilikosea wapi, lakini siku zote ninajiasa kujidhibiti, kujiongoza, kujipenda na kuwasamehe watu wote. Siwezi kumlaumu mtu yeyote isipokuwa macho yangu yapo kwa Mungu ambaye ni mjuzi zaidi kuliko Mimi. Ninaamini ameniponya na atanipa fungu lililo bora zaidi.

Nimefanikiwa kuoa na nina watoto wawili mpaka sasa. Nampenda mke wangu na ananipenda pia. Tuna miaka mitano ya ndoa yetu.

USHAURI WANGU kwa wazazi wote wa nchi hii, wawe makini na watoto wao kwa kila hatua. Ni muhimu kutenga muda wa kutazama nyendo za mtoto na tabia zake kwa ujumla. Jambo dogo linaweza kuharibu mfumo mzima wa maisha ya mtoto na tabia yake yote na asiweze kujinasua milele. Tuwalinde watoto na tuwaongoze katika njia sahihi.

Wakati mwingine si kosa la wazazi kwa sababu mzazi hawezi kuwa Mungu muonaji wa vyote. Kuna kuteleza na kushindwa kutazama nyendo zote za Mtoto. Tumuombe Mungu awalinde watoto wetu pale ambapo macho yetu hayawezi kufika.

Ninaiomba serikali iunde vituo maalumu vyenye tiba ya kisaikolojia na ya kitabibu kwa wote waliodhurika na ushoga na ambao wako tayari kuachana nao. Tiba hii ihusishe mabingwa wa maradhi ya kitabia, maradhi ya kiakili na maradhi ya kibayolojia katika kuwakwamua waathirika wa jambo hili na inawezekana. Hata msaada wa kiroho pia unaweza kujumuishwa na iwe ni mkakati wenye malengo thabiti kabisa. Sio wote wenye nguvu za kiakili za kuweza kujiponya kama nilivyofanya mimi. Wengine wanahitaji msaada kutoka nje. Kujiponya inahitaji nidhamu ya hali ya juu na akili thabiti pamoja na usaidizi wa Mungu.

Serikali ione haja ya kuunda mkakati endelevu wa kuwasaidia wote waliozama katika shimo hili la giza kupitia wataalamu wake na taasisi zake. Madhara ya kutowasaidia ni pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya ngono, Ukimwi, kisonono na mengineyo. Tiba hii itajumuisha tiba ya kiakili, tiba ya madhara ya msongo wa mawazo au Post Traumatic Disorder pamoja na tiba ya kitabia. TUWASAIDIE.

Tanzania bila ushoga inawezekana tukiwekeza katika mbinu zenye nia ya kweli na ya dhati ya kuwasaidia waathirika wote kupitia vituo maalumu vya kitabibu na kisaikolojia ambavyo vinaweza kuwa na muundo wa "rehab" au muundo mwingine utakaofaa.

Katika yote Mungu ndio mjuzi zaidi. Macho yetu yazidi kumuelekea yeye daima.

Alhamdullilaah!
Vipi kwasasa ukikutana na Mabwana Zako waliokuwa wanakuchanua (mfano Kule shule ).Hongera sana kwakweli kwakushinda hilo ibilisi. Sasa walinde watoto wako mkuu.
 
Umeelezea jinsi ulivyoingia na ulivyoishi na hisia hizo shuleni.
Lakini hujagusia hata kidogo ni kwa namna gani umejinasua kwa kutumia akili yako(kama unavyojinasibu) zaidi ya kuitupia mpira serikali na jamii tena.

Ingelikua vizuri kama ungeweka ABC ulizofata hadi ukajinasua, huenda kuna mwingine akatumia mbinu zako au zinazoshabihiana na zako akajinasua pasi na kuisubiri serikali kama wewe ulivyofanya.
Asipofanya kama ulivyosema andiko lake linakosa uzito fulani hivi
 
Naam nikupe hongera sana kwa kufunguka na kulichukulia hili jambo kama janga na tatizo kubwa kwataifa na dunia nzima tofauti na mbuzi wengine ambao wao huona ni kama tabia sahihi na jambo la kujivunia
wapo kwenye mwezi wao huu wanauita priDEMONth, waathirika wakiwa na mtazamo halisi kuwa hili jambo halifai hakika tutakuwa na jamii thabiti
Asante sana.
 
Umeelezea jinsi ulivyoingia na ulivyoishi na hisia hizo shuleni.
Lakini hujagusia hata kidogo ni kwa namna gani umejinasua kwa kutumia akili yako(kama unavyojinasibu) zaidi ya kuitupia mpira serikali na jamii tena.

Ingelikua vizuri kama ungeweka ABC ulizofata hadi ukajinasua, huenda kuna mwingine akatumia mbinu zako au zinazoshabihiana na zako akajinasua pasi na kuisubiri serikali kama wewe ulivyofanya.
Asante sana kwa hoja yako.
 
Ushoga ni upumbavu
Ni mambo ya kujiendekeza.
Mtoto hata awe mdogo anatambua jinsia yake na anajua maana ya jinsia yake.

Tuache kusingizia malezi.
Shoga linaamua lenyewe liwe senge tu.
Yaani mwanaume utatamani vip ukaingiliwe matakoni eti unapata raha.

Serikali itunge sheria mashoga wanyonge uone kama haya yatatokea.

Mbona Russia, North Korea, saud Arabia n.k nchi zenye sheria kali hakuna mashoga
 
Back
Top Bottom