Suma Lee atoa elimu nzito katika post yake ya msiba wa msanii Jebby

Suma Lee atoa elimu nzito katika post yake ya msiba wa msanii Jebby

Kufufuliwa na Mungu ni jambo rahisi sana kwake je ikiwa hujafika kaburibi ugarudishiwa roho labda uko porini tu itakuwaje ukipiga kelele maana utaamka, tumesoma hiv
HAIJAALISHI UMEKUFA PORINI AU BAHARINI AU UMEZIKWA, au UMECHOMWA, ANACHOKIITAJI MUNGU NI ROHO, KIWILIWILI SIYO SHIDA, MWILI UTATOOZA NA KUTOKA MAFUNZA NA ITABAKI MIFUPA, anachokiitaji ni roho, unaenda kufufuliwa tena akhera na kuanza kuhukumiwa kama umefanya makosa, Pia kama umeonewa utapata malipo huko, kama umeonea utahukumiwa huko, NDIO MAAANA TUNAPOFANYA MAKOSA TUNATAKIWA TUMREJEE MUUMBA NA TUSIRUDIE TENA COZ KUNA MAISHA BAADA YA KUFA
 
Yesu alitumbia kifo ni kama usingizi mzito, ina maana mtu hajitambui akiwa amekufa na hakuna ushahidi wowote yakinifu unaoelzea wafu hujisikiaje wakiwa kaburini hizo stori zingine huwa ni za kubuni tu na ni uongo , shetani huwafanya watu waamini kuwa watakpokufa basi kuna chance wanaweza kuishi huko ahera hivo huwafanya watu wajisahau katika kutenda mema na kufuata sheria za Mungu wakijua kuwa wataishi tena maisha mengine huku wakiamini maombi ya ndugu zao duniani yanaweza kuwafanya wasamehewe dhambi zao kitu ambacho si kweli, Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa coz shetani hayupo tayari kuhukumiwa jehanamu peke yake hivo huwasaka wafuasi wake huku akijua kuwa ana muda mchache tu. Ni afadhali watu wakachunguza maandiko sasa kwani unabii unaonesha kuwa tupo kwenye utawala wa mwisho kabisa wa dunia, tena tulishatoka mguuni tupo kwenye unyayo ambako baada ya hapo utawala wa Yesu utafuata, ni jinsi kama ilivoelezea katika kitabu cha daniel
Watu waanze kutafuta maarifa sasa
 
  • Thanks
Reactions: PNC
INNA LILLAH WA INNA ILAIHI RAAJIUUN
[HASHTAG]#JEBBY[/HASHTAG]

UNAVYO JIHISI KIFO.
Mtu huwa hatambui kuwa amekufa pale anapokufa. Yeye hujihisi anaota anakufa, anajihisi analia, anaoshwa, anafungwa na anateremshwa kaburini. .

Bado anajihisi kuwa anaota anapofunikwa na mchanga. Kisha hulia kwa makelele na hakuna anae msikia.
Baadae kila mtu anapotawanyika na ameachwa pekee chini ya ardhi, Mungu huirudisha roho yake. Anafungua macho na kuamka kutoka "ndoto yake mbaya" .
Mwanzoni, hufurahi na kushukuru kuwa alikuwa anaota tu, na sasa ameamka kutoka usingizini. Kisha hujigusa mwili wake ambao utakuwa umefunikwa na kitambaa cheupe,na kwa mshangao hujiuliza "shati/gauni langu liko wapi?"
Kisha ana anza kujihisi "niko wapi?" "hii ni sehemu gani?" Mbona kuna harufu ya udongo kila mahali? Ni nini haswa ninacho kifanya hapa?
Hapo ndipo atakapo anza kugundua kuwa yuko chini ya ardhi na alicho kihisi haki kuwa ndoto!
Ndiyo, anagundua kuwa ni kweli yeye amekufa, na amezikwa. .

Anapiga kelele kadri anavyoweza kuwaita watu waliokuwa karibu nae ambao wangeweza kumuokoa:
"baba"
"mama"
"kaka"
"dada"
"rafiki"

Hakuna anaemjibu. Kisha anagundua kuwa Allah ndio tegemeo lake pekee. Akilia na kumuita huku akimuomba msamaha :
"Yaa Allaaaaah...
Yaa Allaaaaaah...
Nisamehe mimi
Yaa Allaaaaaah!!! .

Anaita akiwa na hofu kubwa,ambayo hakupata kuwa nayo alipokuwa hai . .

Kama alikuwa mtu mwema na mcha Mungu, malaika wawili wakiwa na uso ulio na furaha watamkalisha na kumliwazana kumhudumia vizuri. .

Kama alikuwa mtu mbaya na hakuwa mcha Mungu, malaika wawili watamwongozea hofu yake na kumpa mateso kufuatana na amali zake mbaya. .

Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu, dhambi za baba yangu, mama yangu, mke/mume wangu na wanangu na jamaa zangu na marafiki. .

Ewe Allah, usiuchukue uhai wangu ila pale nitakapo kuwa tayari kukutana nawe.

Kaka na dada katika uislam,una chaguo mbili hapa:

#1.Uache ilimu hii hapa isomwe na hakuna kitakacho tokea.

#2.[HASHTAG]#TAg[/HASHTAG] Isambaze ilimu hii kwa marafiki zako,.na wote wengine.
In Sha Allah itakuwa na manufaa kwao, na wewe utafaidika.
Ameen.
NB😛ichani ni Suma lee akiwa na msanii mwenzake marehemu Jebby.View attachment 754546
Huenda na yeye anadhani anaota kumbe ndo anatoa ujumbe kweli.

Kufa ni moyo kupoteza uwezo wa kusukuma damu. Hivyo hupelekea mwili wote kushindwa kufanya kazi ikiwa ni pamoja na ubongo ambao hutunza kumbukumbu

Hakuna aliyewahi kufa akawa hai tena
 
Uwepo wa dini tofauti tofauti unaleta mitazamo tofauti tofauti kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Kwa mfano, linapokuja suala la KIFO ( MAUTI ), Kila dini ina mtazamo tofauti kutokana na kitabu wanachotumia. Dini ya Kiislamu, Kikristo, Kihindu, Kibudha, Kishinto na pia dini za asili za Kiafrika na Kiasia bado zinatofautiana kuhusu kifo, jinsi mtu anavyokufa, kile kinachotokea akiwa kaburini na baada ya kifo ( ufufuko ) itakuwaje. Ukichukulia dini hizi kubwa mbili ambazo ni Ukristo na Uislam unakuta mitazamo inakinzana katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu. Na kila mtu anaamini kuwa mtazamo ulioandikwa katika kitabu cha dini yake iwe Biblia takatifu ama Quran tukufu. Ninachoona ni kwamba; kabla hatujaanza kukosoa maandishi ya mtu kuhusu suala la imani, tunapaswa tuwe na uelewa dhahiri wa imani / dini ya mtu huyo ili tuweze kujua kuwa anatofautiana na sisi wa imani nyingine. Hii itatusaidia kutokumkosoa pale anapotoa mtazamo wa dini yake bali tunajaribu kumuelewa. Lazima tujengeane tabia ya kukubali kutokukubaliana, ambayo itatufikisha katika hitimisho la pamoja ya kwamba kila mtu aamini anachokiamini kuhusu kifo / mauti. Muislam akitoa mtazamo wa dini yake, Wasio waislam wanapaswa kumuelewa na hakuna haja ya kuanza kuonesha mtazamo ya kwamba mafundisho fulani ni uongo. Pia Mkristo anapotoa mtazamo wa dini yake, anapaswa pia kuheshimiwa na wasio wakristo. Suma Lee ametoa mtazamo sahihi wa kifo kwa mujibu wa mafundisho yake ya Uislam. Suala la kuhoji kuwa hajawahi kufa na kufufuka, hilo halina mantiki hata kidogo. Kwa sasa aliyewafunulia kitabu chao ( Allah ) ndiye anayewaeleza kuhusu kifo na jinsi mfu anavyokuwa huko kaburini. Hivyo, hatupaswi kumpinga aliyetoa mtazamo wa kitabuni kwake, kama una hoja zenye mantiki, basi mpinge mtoaji wa mwanzo ( Allah ) wa hicho kitabu unachodhani hakijaeleza suala la kifo kama unavyotaka.
 
unajua siku zote ukweli hujitenga peke yake, nadhani kati ya imani hizi mbili juu ya kifo basi moja ya imani ni ya kweli kabisa,hakuna majibu mawili hapa nadhani kuna jibu moja tu sahihi. Watu hujikuta wapo kwenye dini kutokana na malezi ya wazazi wao pasipo kujiuliza maswali mengi na kuyapima maneno ya vitabu vitakatifu wanavyoviamini, mi naamini pia hakuna madhehebu mengi duniani but kuna still dhehebu moja tu la kweli sema bado tu watu bado hatulijui, mi nadhani mtu akijitoa kikamilifu na kufunga na kuomba juu ya kupata imani ambayo ni ya kweli na dhehebu la kweli basi atalijua,
 
HAIJAALISHI UMEKUFA PORINI AU BAHARINI AU UMEZIKWA, au UMECHOMWA, ANACHOKIITAJI MUNGU NI ROHO, KIWILIWILI SIYO SHIDA, MWILI UTATOOZA NA KUTOKA MAFUNZA NA ITABAKI MIFUPA, anachokiitaji ni roho, unaenda kufufuliwa tena akhera na kuanza kuhukumiwa kama umefanya makosa, Pia kama umeonewa utapata malipo huko, kama umeonea utahukumiwa huko, NDIO MAAANA TUNAPOFANYA MAKOSA TUNATAKIWA TUMREJEE MUUMBA NA TUSIRUDIE TENA COZ KUNA MAISHA BAADA YA KUFA

your wrong mkuu , hakuna maisha baada ya kufa
 
Izo Hadithi za abunuwasi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]itabid mtu tukisha mzika tusubiri mda kdgo afu tuka mtoemo maana atakua amesha rudishiwa uhai
 
Back
Top Bottom