Pre GE2025 Sumaye: Hakuna anayeweza kuongoza hii nchi zaidi ya Rais Samia

Pre GE2025 Sumaye: Hakuna anayeweza kuongoza hii nchi zaidi ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri mkuu Mstaafu na mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Kanda ya Mashariki amesema hakuna mtu mwingine anayeweza kuongoza nchi hii ya Tanzania zaidi ya Dr Samia

Sumaye alikuwa anamueleza Katibu mkuu wa CCM Dr Nchimbi
---
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema hakuna anayeweza kuongoza Tanzania zaidi ya Samia Suluhu Hassan.

Sumaye aliyasema hayo leo wilayani Hanang, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, anayetembelea mikoa mitano.

“Hakuna mtu mwingine anayeweza kuongoza hii nchi zaidi ya Samia Suluhu Hassan, acha nje ya CCM hata ndani ya CCM, hakuna mtu atakayeiongoza hii nchi, atayeiendesha kama inavyokwenda zaidi ya Samia Suluhu Hassan.

“Hata ndani ya CCM hayupo, sembuse nyie nje kuna nini! Husikii wenyewe wameparura hovyo hawajapata madaraka wanaparurana,wakipata si tutakoma, amesema Sumaye.

Source: Nipashe
 
Waziri mkuu Mstaafu na mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Kanda ya Mashariki amesema hakuna mtu mwingine anayeweza kuongoza nchi hii ya Tanzania zaidi ya Dr Samia

Sumaye alikuwa anamueleza Katibu mkuu wa CCM Dr Nchimbi

Source: Nipashe
Maana halisi ya Wazee wa hovyo.
Anazeeka vibaya na atakufa vibaya huyu namhurumia huyuuuu...
 
Hata ambaye hakupaswa kujikomba anajikomba umri ule anataka nini awam hii?

Warioba huwa namuelewa sana hajui kusifia walio juu
Kwa Magu aliweweseka kidogo. Watu wetu kwenye siasa ni changamoto.

Tunahitaji wananchi wenye uwezo na uzalendo kabla ya kuwa viongozi.

Wanaoweza kuishi kiuchumi na kifikra bila kutegemea serikali.

Changamoto nyingine ni serikali kuwa tayari kuwavumilia na kuwajenga raia wa aina hiyo.
 
Hahahah, Walisema hivyo hivyo Magufuli alipowaita ikulu akawanyamazisha wote. "Tunawalipa stahiki zenu halafu kila siku mnatukosoa kwenye vyombo vya habari, jiungeni upinzani mkose stahiki zenu mtukosoe sana".
Wakaufyata. Leo wanaimba mapambiao.
 
Back
Top Bottom