Sumbawanga: Madereva Bajaj waandamana kisa CHADEMA kushindwa kuwalipa baada ya kukodishwa kumpokea Freeman Mbowe

Sumbawanga: Madereva Bajaj waandamana kisa CHADEMA kushindwa kuwalipa baada ya kukodishwa kumpokea Freeman Mbowe

1. Habari imeandikwa wameenda Ofisini kwa MWENYEKITI. Sasa kama unaona hapo ofisini kwa MWENYEKITI WA CHADEMA ni Kijiweni sawa.
2.Hoja yako ya pili nenda Sumbawanga ukafanya confimation
3. Hongera sana mtaalamu wa kujua wadai na wadaiwa kwa kuangalia mionekano
Hapo ofisi iko wapi?
 
Pamoja na video Bado unasema ya kutunga? [emoji2957][emoji2957]
Video kitu gani mzee? Mbona mpumbavu hivi? Enzi za propaganda za Makonda kuliwahi kuwa na video eti za Lowasa kumtelekeza mtoto. Tumia akili. Hicho ni kikundi cha wahuni. Si waende mahakamani?
 
Madereva Bajaj wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wameandama hadi kwenye ofisi za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA aitwaye Cedrick Malila almaarufu IKUWO WAKIDAI MALIPO YAO waliyoahidiwa wakati wamekodishwa kwenda kumpokea Mwenyekiti cha CHADEMA Freeman Mbowe huko Katumba.

Akizungumza mmoja wa madereva aliyejitambulisha kwa jina la Kelvin Nobert anaeleza kuwa walikodiwa na CHADEMA ili wampokee Mbowe kutoka eneo la Katumba hadi Nduwa kwa malipo shilingi 10,000 lakini pamoja na ukweli kwamba walizidisha muda wa kufanya kazi kutoka saa 4 hadi 10 bado CHADEMA haijawalipa hata shilingi moja

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
View attachment 2531555
Hivi kwanini Nchi hii watu wamekosa Imani kiasi hicho? Yaani pamoja na video watu HAWAAMINI! Tumefikaje hapo? Aliyespost anajisikiaje ikiwa Umma unamwambia ni uongo pamoja na kuwa na evidence? Ina maana aliyespost haaminiki kiasi hicho?
 
Na mimi nawachukia wajinga kama nyie. Ambao mkiambiwa jambo mnakubali bila kufanya uchunguzi.
Ww ndo mjinga kwani haujaona nilichokiandika,au ww ulitaka nijaze ukurasa humu,inakuingia akilini kwamba madereva wa bajaji wanakufa njaa wao na family yao kisa hiyo ten waliambiwa kupewa na hawakupewa tena kwa siku moja tu?
 
Back
Top Bottom