Sumbawanga: Mtoto auawa kwa kuliwa na nguruwe

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2019
Posts
1,885
Reaction score
3,227
#HABARI Mtoto aitwaye Haruna Mwanakatwe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi (10) mwenye ulemavu wa viungo na mkazi wa mtaa wa Edeni B Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa kuliwa na Nguruwe nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea jana Juni 25, 2023, baada ya mtoto huyo kubaki ndani peke yake na kwamba alijisaidia na kukosa msaada hivyo inadaiwa Nguruwe aliposikia harufu ndipo alipoenda kuvamia chumba alichokuwepo mtoto huyo na kuanza kumshambulia miguuni, tumboni na sehemu za siri.

1687792801043.png

#EastAfricaTV
 
View attachment 2669540

#EastAfricaTV
Mmmh
Mungu ampokee mja wake.

Pole sana kwa familia
 
Maumivu yake

Kilio alichotoa alipokuwa akinyofolewa nyama

Inauma sana kuliwa na mnyama ukiwa waona

Inauma sana ukijua unakufa na huna msaada

Inauma mtoto kulia Mama nakufa, mama nakufa

Nisaidieni nisaidieni

Hakuna msaada hadi kifo kinamkuta anakufa bila msaada wa mama au baba au mtu yeyote yule.

Hayo madude ndo maana Yesu aliagiza yasiliwe.

Hapo limekula mtu afu litaenda liwa na watu
 
Nguruwe wameanza lini kula watu? Au ni mgonjwa?
Nguruwe akiwa na njaa huwa hajielewi kabisa, kitu chochote kinachopita mbele yake anachoweza kuua basi anakula. Iwe kuku, nyoka na sometimes hata watoto wake mwenyewe.

Mtoto ni rahisi kumkwepa nguruwe, huyo aliyeuawa alikuwa na ulemavu kwahiyo inawezekana hata kukimbia hakuweza.
 
Duuh hatar sana bas
 
Back
Top Bottom