KERO Sungusungu Chamazi wanakuja kudai fedha usiku bila vitambulisho

KERO Sungusungu Chamazi wanakuja kudai fedha usiku bila vitambulisho

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kikundi cha watu kilichojitambulisha kuwa ni Sungu Sungu wa Chamazi Msufini kinadaiwa kuwafuata wananchi usiku wa manane kudai fedha za ulinzi bila kuwa na vitambulisho wala barua kutoka kwa mamlaka husika.

Wanadaiwa kufika wakiwa zaidi ya watu 10, wakiwa na marungu, kugonga milango ya wananchi wakiwa wamelala na kudai malipo ya ulinzi. Pia wanadaiwa kutumia lugha chafu za matusi na kuwakamata baadhi ya watu usiku kwa madai ya kutolipa fedha hizo.

PXL_20260719_210607308.jpg
 
hapana hiyo siyo sawa, tena wanakosea


karibu sana bwana Anonymous hapa jamii forums. wewe ni rafiki yangu kule fb
 
Daah ili taifa ni bure kabisa.
Pesa zao wafate kwa mjumbe/serikali ya mtaa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hao ni wezi kama wale panya road
mara nyingi wakikutana na watu usiku wanawapa adhabu, viboko na wale walevi wanawasachi pesa wanachukua
wakikuta nguo au vya thamani vipo nje watachukua

Kwa ushauri na tahadhari, upo utaratibu wa polisi shirikishi amboa mtaa wanaweza kukubari kulipa kiasi fulani kwa kikundi cha watu fulani ambao wanatambulika na walipitia mgambo
 
Back
Top Bottom