Super Market za Tanzania ni ghali sana kuliko za Marekani. Mzungu huyu anasema ukweli

Super Market za Tanzania ni ghali sana kuliko za Marekani. Mzungu huyu anasema ukweli

Super Market za Tanzania ni ghali sana kuliko za Marekani. Mzungu huyu anasema ukweli.

View attachment 2857270
Shida ni ushamba na ulimbukeni, supermarket ni duka km maduka mengine. WaTZ wanachukulia maduka ya wenye nazo wakati kwa wenzetu hata pale Estwani hata mahindi ya kuchoma huuzwa supermarket
 
Kuna kufikiri kimsawaziko (Rationale) kitu ambacho ni tatizo kwa watanzania.

Mzungu anajua kwa mfano bidhaa fulani Marekani inauzwa Dollar Moja, Sasa anaikuta Tanzania inauzwa kwa dollar sita.

Hapo mjadala wa kimsawaziko usiwe gharama ya usafiri maana mantiki itakataa gharama ya usafiri kuzidi Dollar Moja kwa bidhaa inayouzwa Dollar moja Marekani.

Jee tunapoweka Kodi si huwa tunaweka Kodi kubwa kwenye bidhaa tunazosema zisizo za lazima??

Tunasahau Kuna bidhaa tumeweka Kodi kubwa kwakuwa tunasema tunalinda viwanda vyetu vinavyozalisha bidhaa kama hizo?

Ghafla tumeshasahau kuwa hizo "Super Market" ziko yale maeneo ambayo bila ya Uhalisia Kodi zake za Kupanga ni kubwa sana bila ya sababu za Msingi?

Jee Kodi kubwa ya Kupanga haiwezi kupandisha bei ya bidhaa??

La mwisho ambalo halisemwi sana na hao "wazungu" wanaolalamika wanatakiwa waambiwe ni kuwa, wateja wakubwa wa kwenye hizo Supermarket ni wakwapuaji wa Hela za umma kwa ivo Hela kwao siyo tatizo.
 
Shida ni ushamba na ulimbukeni, supermarket ni duka km maduka mengine. WaTZ wanachukulia maduka ya wenye nazo wakati kwa wenzetu hata pale Estwani hata mahindi ya kuchoma huuzwa supermarket
Umeongea issue sahihi sana..kwa wa Tz wengi mindset ni kua supermarket ni sehemu ya watu wa status flani, ni kama prestige kununua vitu .

Kumbe kwa wenzetu huku ndio sehemu ambapo watu wa vipato vyote wana enjoy wigo mpana wa bidhaa na huduma.
 
Halafu bidhaa zote zinazo tengenezwa na zikauzwa kwenye hayo Maduka ya super Market hazifai kuliwa na binadamu zinaleta maradhi ya Kansa, Kisukari, Unene, wa kupitiliza Presha na maradhi mengine mbalimbali kiafya bidhaa zinazouzwa katika hayo Maduka ya super Market hazifai kuliwa kabisa.
Sasa ingekuwa hivyo Wamarekani wote si wangekufa?
 
Supamaket tunaenda kuuza sura tu.... Mahitaji mengi kwa mangi
Upo sahihi kwa mangi, muha, mgosi mtaani ndio mwokozi. Yaani super market ni kama eneo la anasa bongo, vitu Bei juu wakati wao wananunua kwa jumla madukani makuu au viwandani. Nchi za Kusini mwa Afrika wananchi wao wote wamezoea supermarkets nenda tu hapo Tunduma Mpakani ukivuka duka unakuta ni kubwa, bidhaa chee.
 
Nadhani usafirishaji wa bidhaa kutoka nje ndio unaongeza bei ya bidhaa.

HIZO BIDHAA ZOTE NI IMPORTED GOODS

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Mkuu torch fake ya mchina unaikuta supermarket inauzwa 15,000 ukienda Kariakoo au kwa machinga unaikuta ileile 5,000 tu.
Kuna shida flani labda gharama za wafanyakazi, nyinginezo zinasababisha bei aghali.
 
Halafu bidhaa zote zinazo tengenezwa na zikauzwa kwenye hayo Maduka ya super Market hazifai kuliwa na binadamu zinaleta maradhi ya Kansa, Kisukari, Unene, wa kupitiliza Presha na maradhi mengine mbalimbali kiafya bidhaa zinazouzwa katika hayo Maduka ya super Market hazifai kuliwa kabisa.
Za wapi zinafaa kuliwa? Unajua kwa mangi ni hatari zaidi maana kule viki expire wanafuta tarehe.
 
Super Market za Tanzania ni ghali sana kuliko za Marekani. Mzungu huyu anasema ukweli.

View attachment 2857270
alitaka vitu viwe cheap wakati hatutengenezi sisi weneywe hapa? nilishawahi kuishi nchi moja kubwa huko magharibi, nilikuwa nakula samani kwa bei rahisi kuliko hawa ninaonunua hapa.au labda ilikuwa nchi ya kisiwa. nyama bei rahisi, iwe ya sungura, ng'ombe, mbuzi.makuku ndio huwa siyapendi.
 
Mkuu torch fake ya mchina unaikuta supermarket inauzwa 15,000 ukienda Kariakoo au kwa machinga unaikuta ileile 5,000 tu.
Kuna shida flani labda gharama za wafanyakazi, nyinginezo zinasababisha bei aghali.
Tupe huo mfano wa hiyo tochi..then angalia pia na location na masuala ya kodi..usifananishe bei ya chinga na bei ya supermarket
 
Nadhani usafirishaji wa bidhaa kutoka nje ndio unaongeza bei ya bidhaa.

HIZO BIDHAA ZOTE NI IMPORTED GOODS

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Hata mkate na sabuni Mbuni pia imported?
Mbona pia bei juu.

Shida ni kwamba kwa Tanzania Super Markets inakuwa kama ni kwa ajili ya watu wenye maisha ya juu,,na wanaojiweza wakati wenzetu inchi zilizoendelea Super Markets ni soko la kaiwada sana tena ni kwa kila mtu na bei zake zipo chini sana..

Mfano,, super markets..
--Shoprite
--Spars
--Checkers
--Boxers
--Pick and pay
Ect.

Zote hizi wanauza bei rahisi kuliko viduka vya kawaida mitaani.
 
Back
Top Bottom