Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kuna tofauti kubwa kati ya Jini na shetani ..."Majini ni viumbe kama sisi tena wanamuabudu Allah" alisikika ustadh mmoja akisema
Ukishamuita na ukamtumia huyo keshakuwa shetani ... Yale majini yanoyopanda vichwani mwa watu ni mashetani .. jini ana mipaka yake amewekewa hatakiwi kuingilia maisha ya binadamu..basi pale anapoingilia ameshakuwa shataniNataka kuyatumia majini wazuri
Wako baadhi ya mashehe wanawatumia majina kwa kazi zaoUkishamuita na ukamtumia huyo keshakuwa shetani ... Yale majini yanoyopanda vichwani mwa watu ni mashetani .. jini ana mipaka yake amewekewa hatakiwi kuingilia maisha ya binadamu..basi pale anapoingilia ameshakuwa shatani
So zile amri kumi aliandika nani.Je biblia ni kitabu cha Allah ? Ama unatumia biblia kama excuse ya jini kuwekewa sura yake kwenye Quran ?
Pia tambua Biblia haijaandikwa na Mungu wala Allah.
Biblia ni muunganiko wa vitabu 66. Ambavyo vimeandikwa na waandishi tofauti tofauti zaidi ya 40.. kila mtu alijiandikia kwa muda wake.. Mungu hajashusha biblia na wala hajaandika biblia.
Hayo ni mashetani yamemuasi Allah na kupetuka mipaka yaoWako baadhi ya mashehe wanawatumia majina kwa kazi zao
Yame-asi vip nawakati wana aya zao kwenye quran kwamba wako wazuri na wabayaHayo ni mashetani yamemuasi Allah na kupetuka mipaka yao
Tatizo kubwa mlilonalo nyinyi ni uelewa! unaamini umefahamu kitu wakati umeifunga milango yako ya ufahamu. Huwezi kumfahamu jirani uliyenaye sasa kwa kutumia taarifa za jirani yako wa zamani. Hii ni sawa na ile hadithi ya yule kipofu aliyeona mara moja tu maishani mwake na alichokiona ni jogoo tu, sasa kila kizuri anachoambiwa yeye anabakia "kama jogoo!?" "kama jogoo!?"Jini tena yupo kwenye kitabu cha Allah ?
Minataka jini ili nipate utajiri nisaidie tafadhali niko tayari kuyafugaTatizo kubwa mlilonalo nyinyi ni uelewa! unaamini umefahamu kitu wakati umeifunga milango yako ya ufahamu. Huwezi kumfahamu jirani uliyenaye sasa kwa kutumia taarifa za jirani yako wa zamani. Hii ni sawa na ile hadithi ya yule kipofu aliyeona mara moja tu maishani mwake na alichokiona ni jogoo tu, sasa kila kizuri anachoambiwa yeye anabakia "kama jogoo!?" "kama jogoo!?"
Kitu mnachopaswa kuelewa ni kwamba kile mlichofundishwa kanisani kwamba jini ni malaika walioasi ni tofauti na kile kinachofundishwa msikitini. Sisi waislamu hatuamini kama jini aliwahi kuwa malaika hata siku moja. Jini ni kiumbe, malaika ni kiumbe, na Binadamu ni kiume na wote hawa watatu ni viumbe wa tofauti baina ya mmoja na mwengine. Ukishaliingiza hili akilini sasa ndo utaanza kuelewa mafundisho ya Uislamu yanasema nini kuhusu hivi viumbe vinaitwa majini.
kama umeelewa hapo juu sasa tuendelee.
Ukishangaa kuwepo majini wema na waovu pia naomba ushangae kuwepo wanadamu wema na waovu, kwa kuwa wote hawa ni viumbe dhalili kabisa wa Allah na yeye ndo aliyewaumba, na wote wameumbwa ili wamuabudu yeye tu. Tofauti ya malaika na hawa viumbe wawili ni kwamba malaika hawatendi dhambi na ndo maana hujawahi kusikiwa malaika watakuwa rewarded kwa matendo yao mema au labda wataadhibiwa iwapo watafanya madhambi (hii haipo kwenye mjadala kabisa), hakuna malaika anatenda maovu.
Turudi katika hiyo Suratul Jinn. kwanini msisome kitu na kukijua kinasemaje kabla ya kuchangia mada ukiwa bado ni mjinga wa unachokichangia? mmeaminishwa kwa kutishwa na mambo ya ajabu sana.
Hii sura anaambiwa mtume yale waliokuwa wakisema majini baada ya kumsikia yeye akisoma Quran, na kwamba kutokana na hiyo Quran walioisikia wameongoka baadhi yao kutoka katika maovu waliyokuwa wakitenda. Na pia Allah anamuelezea Mtume (pamoja na wasomaji wote wa Quran) pale majini waliposema na kushangaa juu ya upotevu wa baadhi ya watu waliojikinga kwa kuwatumainia hao majini ilhali hakuna wanachopata zaidi ya kuongezewa mzigo na upotofu.
Mi niwaombe ndugu zetu wakristo mujielimishe kwanza. Acheni hadithi za kuogopa jinamizi usiku kama watoto wadogo.
Aliyetaka Surat Jinn hiyo imeshawekwa kazi kwake kusoma,KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.
4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.
11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.
12. Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
13. Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.
14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.
15. Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.
16. Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi,
17. Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.
18. Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.
19. Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!
20. Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote.
21. Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.
22. Sema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.
23. Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.
24. Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.
25. Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu.
26. Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,
27. Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.
28. Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.
Hakuna mtu anafuga majini, mnadanganywa! hao mnaodhani wanafuga majini wao ndo watumwa wa hao majini!Minataka jini ili nipate utajiri nisaidie tafadhali niko tayari kuyafuga
Kwahiyo wewe hapo hujawahi kumuasi Allah? kwahiyo wewe ni shetani.kwahiyo kumbe hakuna shetani kama shetani ila kila tu anayefanya dhambi ndio anageuka na kuwa shetaniNi kweli kuna tofauti kubwa kati ya Jini na shetani ...
Jini anaweza kuwa shetani kama vile binadamu anaweza kuwa shetani ukimuasi Allah
Aya zao zinasemaje?Yame-asi vip nawakati wana aya zao kwenye quran kwamba wako wazuri na wabaya
Jini tena yupo kwenye kitabu cha Allah ?
Kuna shehe wa msikiti sitautaja jina ameniambia atanisaidia ni kazi ndogo sanaHakuna mtu anafuga majini, mnadanganywa! hao mnaodhani wanafuga majini wao ndo watumwa wa hao majini!
Sasa basi kama unataka kuwa mtumwa wa majini basi nenda katafute washirikina wakuongezee mzigo (Surah Jinn aya ya 6)
Kuna bibi jirani alikua anapandisha majini mpaka shehe anakuja kuyatulizaHakuna mtu anafuga majini, mnadanganywa! hao mnaodhani wanafuga majini wao ndo watumwa wa hao majini!
Sasa basi kama unataka kuwa mtumwa wa majini basi nenda katafute washirikina wakuongezee mzigo (Surah Jinn aya ya 6)
Wajinga ndio waliwao, hata Muhimbili pia kuna matapeli huvaa makoti kama madaktariKuna shehe wa msikiti sitautaja jina ameniambia atanisaidia ni kazi ndogo sana
Mwambie huyo bibi jirani yako atafute shekhe wa kweli amtoe hayo mashetani! kama yanatulizwa sio shekhe huyo ndo walewale wavaa makoti ya kidaktari Muhimbili kumbe matapeli.Kuna bibi jirani alikua anapandisha majini mpaka shehe anakuja kuyatuliza
Nikukumbushe wako waislamu ni ndugu zetu mambo mengine tunaona hatuadisiwi
Shehe ambaye ni imam wa msikitini unasema tapeli ndo aliyeniambia kuna namna ya kuwatumiaMwambie huyo bibi jirani yako atafute shekhe wa kweli amtoe hayo mashetani! kama yanatulizwa sio shekhe huyo ndo walewale wavaa makoti ya kidaktari Muhimbili kumbe matapeli.
Huyo ni shekhe wa kweli na ni imamu wa msikiti sitaki niutaje kwa sababu sio vizuriMwambie huyo bibi jirani yako atafute shekhe wa kweli amtoe hayo mashetani! kama yanatulizwa sio shekhe huyo ndo walewale wavaa makoti ya kidaktari Muhimbili kumbe matapeli.