jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Tatizo kubwa mlilonalo nyinyi ni uelewa! unaamini umefahamu kitu wakati umeifunga milango yako ya ufahamu. Huwezi kumfahamu jirani uliyenaye sasa kwa kutumia taarifa za jirani yako wa zamani. Hii ni sawa na ile hadithi ya yule kipofu aliyeona mara moja tu maishani mwake na alichokiona ni jogoo tu, sasa kila kizuri anachoambiwa yeye anabakia "kama jogoo!?" "kama jogoo!?"
Kitu mnachopaswa kuelewa ni kwamba kile mlichofundishwa kanisani kwamba jini ni malaika walioasi ni tofauti na kile kinachofundishwa msikitini. Sisi waislamu hatuamini kama jini aliwahi kuwa malaika hata siku moja. Jini ni kiumbe, malaika ni kiumbe, na Binadamu ni kiume na wote hawa watatu ni viumbe wa tofauti baina ya mmoja na mwengine. Ukishaliingiza hili akilini sasa ndo utaanza kuelewa mafundisho ya Uislamu yanasema nini kuhusu hivi viumbe vinaitwa majini.
kama umeelewa hapo juu sasa tuendelee.
Ukishangaa kuwepo majini wema na waovu pia naomba ushangae kuwepo wanadamu wema na waovu, kwa kuwa wote hawa ni viumbe dhalili kabisa wa Allah na yeye ndo aliyewaumba, na wote wameumbwa ili wamuabudu yeye tu. Tofauti ya malaika na hawa viumbe wawili ni kwamba malaika hawatendi dhambi na ndo maana hujawahi kusikiwa malaika watakuwa rewarded kwa matendo yao mema au labda wataadhibiwa iwapo watafanya madhambi (hii haipo kwenye mjadala kabisa), hakuna malaika anatenda maovu.
Turudi katika hiyo Suratul Jinn. kwanini msisome kitu na kukijua kinasemaje kabla ya kuchangia mada ukiwa bado ni mjinga wa unachokichangia? mmeaminishwa kwa kutishwa na mambo ya ajabu sana.
Hii sura anaambiwa mtume yale waliokuwa wakisema majini baada ya kumsikia yeye akisoma Quran, na kwamba kutokana na hiyo Quran walioisikia wameongoka baadhi yao kutoka katika maovu waliyokuwa wakitenda. Na pia Allah anamuelezea Mtume (pamoja na wasomaji wote wa Quran) pale majini waliposema na kushangaa juu ya upotevu wa baadhi ya watu waliojikinga kwa kuwatumainia hao majini ilhali hakuna wanachopata zaidi ya kuongezewa mzigo na upotofu.
Mi niwaombe ndugu zetu wakristo mujielimishe kwanza. Acheni hadithi za kuogopa jinamizi usiku kama watoto wadogo.
Pia kuna malaika wema na waovu,shetani mwema na muovu,ala mwema na muovu.